FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA WANAWAKE KUTOKWA NDEVU NA VINYWELEO MWILINI(HIRSUTISM)


MATIBABU YA TATIZO LA WANAWAKE KUTOKWA NDEVU NA VINYWELEO MWILINI (HIRSUTISM) 



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji
Kwa upande wangu namshukuru Allah kariim kwa kunikirimu afya njema mimi pamoja na familia yangu na kuniwezesha kupata wasaa wa kuwajibika katika majukumu yangu

Naam ni jambo la kumshukuru Allah kuiona siku mpya kila siku haijalishi unaumwa ama una magumu unapitia USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE hivyo mshukuru Allah kwa kila kitu katika maisha yako

Leo ninakumbushia kuelezea suluhisho la tatizo ambalo nilishawahi kulielezea miaka ya nyuma kidogo ambalo hadi sasa limekua likiendelea kusumbua vichwa vya wanawake wengi juu ya upatikanaji wa tiba sahihi


TATIZO LA HIRSUTISM NI NINI?


Ni tatizo ambalo huwatokea  wanawake kwa kupatwa na mabadiliko ya  kuotwa manyoya/vinyweleo sehemu ambazo kikawaida wanawake huwa hawaoti au hawapendezi kuwa na manyoya/vinyweleo maeneo hayo.

mfano wa maeneo hayo ambayo mwanamke hafai kuotwa na vinyweleo ni kupata manyoya kidevuni yani anaonekana kuwa na ndevu kama mwanaume,au kuotwa na manyoya kifuani, usoni, na mgongoni wakati mwingine manyoya magumu kama ya kiume miguuni na mikononi kitu ambacho sio cha kawaida kutokea kwa mwanamke

Kikawaida wingi wa manyoya mwilini mwa binadamu hutegemea sana vimelea vya ukoo husika, kitaalamu kama genetics lakini mwanamke anapokua na manyoya mengi sehemu ambazo haifai au haipendezi  kwa mwanamke kua vinyweleo mfano mwanamke kuwa na ndevu kuna mambo makuu mawili kwamba anaumwa au ukoo wake uko hivyo japokua waathirika wengi wa shida hii wengi ni wagonjwa wa matatizo ya homoni.

Kuna imaani nyingi zimejengeka juu ya mwanamke kuota ndevu na manyoya mwilini lakini sio katika uhalisia kuwa eti mwanamke akiotwa na ndevu ATAKUA TAJIRI NA MANENO MENGINE MENGI MENGI YASIYO NA UKWELI


CHANZO CHA TATIZO



Kawaida mwanamke akibaleghe huanza kutengeneza homoni za kiume na za kike ndio maana manyoya huota kwapani na maeneo ya uke lakini sasa inapotokea homoni za kiume zikiwa nyingi kitaalamu kama adrogens mwanamke hupata hali hii ya kuota manyoya sehemu ambazo hazihusiki kama nilivyotaja hapo juu
 lakini pamoja na hali hii ugonjwa huu una vyanzo vingine kama vifuatavyo.

POLYCYSTIC OVARY SYNDROME: 
huu ni ugonjwa unaowasumbua wanawake kwa kutokuwa na uwiano sawa wa homoni za kike ambapo kitaalamu tunasema mwanamke kuwa na tatizo  la homornal imbalance hivyo mwanamke hupata mzunguko wa damu ambao sio wa kawaida, kua mgumba,  kunenepa na kupata uvimbe kadhaa kwenye ovari za kutengeneza mayai yake na kupata shida mbalimbali za kuhusu uzazi

MATUMIZI YA DAWA NA VIPODOZI VYENYE KEMIKALI
Chanzo hiki huenda pia ndio kikawa chanzo kikuu cha wanawake wengi kuota ndevu na manyoya  kwa tabia ya kutumia dawa fulani bila maelekezo ya daktari pia siku hizi kuna maduka ya urembo yanauza dawa hizi na kuzigeuza dawa za urembo wakati ni hatari  sana kiafya kwa watumiaji.
kuna dawa kitaalamu zinaitwa steroids huingilia mfumo wa kiungo kinachohusika na utengenezaji wa homoni (Adrenal gland) hivyo zikitumika kwa muda mrefu huleta manyoya ambayo sio ya kawaida kwa wanawake
mfano wa dawa hizi za steroids ni PREDINISOLONE vidonge na cream, SONADERM, CANDIDERM, GENTALINE, na dawa zingine zote zenye mchanganyiko huu kwani zipo nyingi ila mchanganyiko ni uleule ila majina tofauti ya viwanda.
 Dawa hizi hutakiwa zitumike kwa angalau wiki moja tu kutibu ugonjwa wa ngozi lakini wengine wamezigeuza kama mafuta ya kujipaka hivyo kama na wewe unapaka hizo aina za dawa ujue Umejitengenezea mazingira hatarishi ya kuweza kupatwa na tatizo hili la kuotwa vinyweleo

UVIMBE WA KANSA
kansa za kiungo hichi kilichopo juu ya figo[adrenal gland] huongeza wingi wa homoni hizi kwenye mfumo wa binadamu na kuleta ndevu na manyoya magumu ya mwili.

CONGENITAL ADRENAL HYPERPLASIA:
huu ni ugonjwa wa tezi ya adrenal ambao mtu huzaliwa nao na kuanza kutoa homoni nyingi za uzazi na matokeo yake mtu huota ndevu na manyoya mengi mwilini..

CUSHING SYNDROME:
hali hii hutokea baada ya mgonjwa kupata matibabu ya dawa zenye homoni ya  cortisol mwilini mwake kwa muda mrefu. Mfano matumizi ya dawa ya prednisolone vidonge  kwa wagonjwa wa allergy na asthma.

Wakati mwingine ugonjwa huu hutokea bila sababu yeyote hasa kwa jamii za kiarabu na kihindi




DALILI ZA TATIZO


Kawaida mgonjwa wa hirsutism huwa na dalili za kua na manyoya mengi kama nilivyotaja hapo juu lakini pia mgonjwa huweza kua na sauti nzito kama mwanaume, kuota kipara, kinembe kua kikubwa, chunusi na kupungua ukubwa wa matiti


VIPIMO


Mgonjwa anashauriwa kufika hospital kuonana na daktari na kupata vipimo kuangalia wingi wa homoni mwilini wake hasa testosterone kama zitakua zipo juu Au kupiga picha ya ultrasound ya ovary kuangalia kama kuna tatizo lolote au kupima kuangalia uvimbe wa adrenal gland  mara nyingi ni moja ya vyanzo vikuu.


MATIBABU

Matibabu ya tatizo hili hujulikana mara baada ya kutafuta chanzo cha ugonjwa na ni moja ya matibabu bora zaidi kutibu kwa kudhibiti chanzo cha tatizo lakini pia pale ambapo  chanzo hakionekani dawa za uzazi wa mpango na zinginezo hutumika kutatua tatizo hilo kwa hisia ila jambo lenye ubora ni kujua chanzo cha tatizo
Baadhi ya dawa zingine ni zifuatazo ;

SPIRONOLACTONE
Dawa hizi hutumika kuzuia homoni za kusababisha manyoya lakini ukitumia dawa hizi lazima utumie uzazi wa mpango kwani zinasababisha madhara makubwa sana kwa mtoto ikitokea  ukibeba  mimba wakati unaendelea na dozi hiyo.

DAWA YA KUPAKA YA EFLORNIRITHINE;
 Dawa ya  Eflornithine  kitaalamu hutumika kupakwa maeneo yalioathirika na nywele nyingi kuzuia kasi ya kukua lakini hazitoi manyoya yaliyopo.

LASERS THERAPY
 hii ni miale ya mwanga ambayo inapita ndani ya ngozi kuzuia vyanzo vya ngozi{hair follicles} kuota tena mara nyingi hufanya kazi vizuri lakini gharama yake ni kubwa mno na huenda haipatikani kirahisi.

VEET CREAM :
 hii ni cream inayopatikana madukani kwa bei za kawaida ukipaka inanyoa manyoya yote japokua baada ya muda yataota tena lakini inasaidia sana hasa ukipaka mara mara kwa mara au mara moja au mbili kwa wiki.

 ELECTROLYSIS:
hii inahusisha kuweka sindano ndogo  maalumu kwa kila shimo la unywele na kuharibu chanzo chake ni moja ya matibabu mazuri ila ina maumivu makali sana na dawa za nganzi za kupakwa hutumika kupunguza maumivu hayo.

NOTED; kama wewe ni mwanamke una ndevu au manyoya ambayo sio ya kawaida na huenda mwanzoni hayakuepo angalia kwa makini vipodozi vyako huenda ndio vinasababisha lakini pia nenda hospitali ukachunguzwe wingi wa homoni na upigwe picha ya viungo vya uzazi kama viko salama. ushauri wa bure ni kwamba serikali imekua ikipiga marufuku baadhi ya vipodozi na kuvichoma moto lakini watu wanahisi wanaonewa na kuvitafuta kwa magendo, ukiona kitu kimepigwa marufuku acha kutumia kiepuke



HATUA ZA KUFATA KUTIBU NA KUDHIBITI KUENDELEA KWA TATIZO LA WANAWAKE KUOTWA NDEVU NA VINYWELEO

Kuna hatua kadhaa za kiasili ambazo zimethibitishwa kuonyesha matokeo baada ya watumiaji kuleta mrejesho wa matokeo mazuri
Hatua hizi zimegawanyika katika utaratibu mzuri ambapo ukizingatiwa na kutekelezwa ipasavyo inaleta matokeo mazuri na kudhibiti kuendelea kuota kwa ndevu na vinyweleo
Hatua za kufuata ili kudhibiti tatizo ni

1) BADILISHA MFUMO WAKO WA CHAKULA

Utafiti unaeleza waathirika wengi wanaopatwa na tatizo hili ni wale waliothirika na lishe mbovu ambao wanasumbuliwa na uzito mkubwa sana na uzito mdogo sana hali inayopelekea watu hao husumbuliwa na tatizo la homoni kutokua katika uwiano sawia PCOS.
kama yalivyo magonjwa mengine yanayohusiana na lishe bora hivyo hivyo ili mtu aweze kujitibia na kudhibiti kuendelea kuota ndevu na vinyweleo na chanzo cha tatizo lake ni kutokua na uwiano sawa wa homoni atatakiwa kubadilisha mfumo wake wa chakula ili kuweza kutatua matatizo hayo kwa kupungKup uzito mkubwa au kubalansi uzito wake kuwa katika uwiano wa usawa na umri wake

Hapa chini kuna vidokezo vichache vya lishe bora ili kupambana na tatizo hili

Unashauriwa kujitahidi kula mboga mboga za majani kwa wingi na vyakula vilivyomo katika kundi la PROTEINS kama vile nyama,kuku,samaki,mayai,karanga,korosho nk kila siku itasaidia kusawazisha sukari iliyopo katika damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini na hivyo kusaidia kurekebisha mfumo wa homoni

Epuka kabisa kula vyakula vilivyopo katika kundi la Carbohydrates kama vile ugali,wali,viazi,chips,chapati,maandazi,mihogo nk 

Pendelea kunywa maji na maziwa kwa wingi na Epukana na sukari sababu sukari ndio adui yetu namba moja katika kusababisha magonjwa mengi

 Ukizingatia hiyo lishe utapungua mwili wako ikiwa wewe ni mnene na itakusaidia kupambana na tatizo la PCOS na kudhibiti kuendelea kuota kwa ndevu na vinyweleo.


2)ONDOA NA EPUKANA NA MAWAZO AU MFADHAIKO

Huenda ukashangaa hili ukajiuliza  mawazo yanahusiana vipi na tatizo la kuota ndevu, lakini ukweli ni kwamba tezi zetu za adrenal hushughulika Sana kuzalisha homoni ya adrenal mtu anapopatwa na mfadhaiko pia. Tunapokuwa na mawazo sana kuhusu watoto, mambo ya kifedha au mahusiano na hata kitu kingine chochote, tunaunda homoni za mfadhaiko zaidi.
Homoni za mfadhaiko kama cortisol huathiri vibaya udhibiti wa sukari katika damu ambapo huathirika katika hali tofauti na mfadhaiko usio dhibitiwa huweza kusababisha kuongezeka kuzalishwa kwa  homoni za androjeni, haswa DHEAS.
Homoni za Adrojeni kama hizi zinaweza kubadilishwa kuwa DHT, fomu yenye nguvu zaidi ya homoni ya testosterone katika kiwango cha tishu ambayo huchochea chunusi, kuotwa na ndevu na vinyweleo na kupuputika kwa nywele kichwani

Mambo unayoweza kufanya kuondokana na mfadhaiko na mawazo

Fanya mazoezi ya yoga ya kila siku

Pendelea kutafakari na kutambua utukufu na ukubwa wa mwenyezimungu ambaye amekuumba wewe na viumbe vyote vilivyopo ulimwenguni.

Kunywa chai ya kutuliza mfadhaiko na mawazo kama lavender, chamomile, lemon, tulsi nk
Changanyikana na marafiki zako epuka kujitenga
Shiriki tendo la ndoa mara kwa mara ikiwa tayari umeolewa
Pendelea kula vyakula vyenye Omega 3 na vitamins nyingi

3)EPUKA KUJIDHURU NA KEMIKALI TUMIA VITU VYA ASILI KUDHIBITI VINYWELEO

Badala ya kuhangaika kutafuta dawa zenye kemikali  kuondoa ndevu au vinyweleo usoni
Faham tiba rahisi na nzuri za nyumbani zinazoweza kukusaidia kuondoa vinyweleo usoni

1)PAPAI NA MANJANO


Tengeneza mchanganyiko wa papai na manjano ili kudhibiti kuendelea kuota kwa ndevu na vinyweleo mwilini
Chukua bakuli andaa vipande vinne vya papai,vijiko viwili vya unga wa manjano(tumeric powder) vichanganye vizuri upate uji mzito wa mchanganyiko huo kisha jipake mahali palipoota vinyweleo visivyohitajika
Acha kwa dakika 20 hadi ukauke na kubakia mkavu kisha jibandue kwa kusugua ili kuzuia kuota kwa vinyweleo tena
Kupata matokeo mazuri fanya hili zoezi kwa week mara 3

2)LIMAO NA ASALI

Kamua juisi ya limao changanya na asali  vijiko viwili koroga hadi upate uji mzito kisha paka sehemu iliyoota vinyweleo na kaa kwa dakika 15_20 ujibandue kwa kusugua ili kuondoa nywele zilizopo na kudhibiti kuendelea kuota vinywele
Kupata matokeo mazuri fanya hili zoezi kila siku kabla hujaingia kulala

3) KITUNGUU THAUMU NA CHUMVI

Chukua punje kumi za kitunguu thaumu ziponde pamoja na kitunguu thaumu kisha jisugulie mahali penye vinyweleo na kaa kwa dakika 15 kisha nawa na maji safi na jikaushe kwa kitambaa
Kitunguu thaumu kinasaidia kuzuia kuendelea kuota kwa vinyweleo na kufanya ndevu na vinyweleo kupotea
Kupata matokeo mazuri fanya zoezi hili kila siku

4)MSHUBIRI (ALOE VERA) NA PAPAI

 Chukua vipande vinne vya papai liloiva kisha changanya na ute ute wa mshubiri (aloe vera)
Visage hadi upate uji mzito kisha paka sehemu iliyoota vinyweleo na sugua taratibu ili kuzuia kuendelea kuota vinyweleo hivyo kisha kaa kwa dakika 15 nawa na maji safi kisha jifute kwa taulo safi
Kupata matokeo mazuri fanya zoezi hili kila siku kabla hujaingia kulala

Mpendwa msomaji hizo hapo juu ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kujitibia au kudhibiti kuendelea kuota ndevu na vinyweleo mwilini

Noted;

Matibabu ya tatizo hili huchukua muda mrefu kidogo takriban miezi 3 hadi miezi 6 kulingana na vyanzo vya tatizo hili kutofautiana uzito katika matibabu


MATIBABU YA TATIZO HILI LA HIRSUTISM NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER


Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la hirsutism na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia dawa za kuondoa hirsutism na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud ) 

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre