FAHAMU MATIBABU YA TATIZO LA KUTOKWA DAMU KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI,MAANA YA KUKOMA HEDHI,MATATIZO YANAYOTOKEA KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (POSTMENOPAUSE)

FAHAMU MAANA YA KUKOMA HEDHI,MADHARA YANAYOTOKEA KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI NA MATIBABU YAKE


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatuli nina imani sote hatujambo
Sifa na utukufu tumrudishie Mwenyezimungu na atujaalie khery zaidi katika maisha yetu
Ameen!
Naam kama ilivyo ada yetu rejea kichwa cha habari hapo juu kinaelezea mada ya kukoma kwa hedhi
Nina imani posti zangu nilizoanza Kuchambua mada hii ya mambo yote yanayohusu hedhi uliziona na ukasoma
Mpendwa msomaji kama hukusoma nakuomba urejee posti za nyuma ili upate faida za kufahamu mambo yanayohusu hedhi kiundani zaidi
Kutokana na mfululizo wa mada hii ya hedhi leo tun toahitimisha kwa kuelezea hatua ya mwisho kabisa katika mlolongo wa mada ya hedhi,tuanze kwa kujadili maana ya Kukoma HEDHI na matatizo yanayopatikana pia naatibabu yake

 MAANA YA KUKOMA HEDHI (MENOPAUSE)
Kukoma hedhi ni hali ya kawaida ambayo wanawake wote huipitia umri ukiwa mkubwa. Neno kukoma hedhi linaweza likaelezea mabadiliko yoyote yanayomtokea mwanamke muda mfupi kabla au baada ya kuacha kupata siku zake, ikiwa ni ishara ya mwisho wa kuzaa.

Mwanamke huzaliwa akiwa na idadi kamili ya mayai, ambayo hutunzwa ndani ya ovari. Ovari hizi pia hutengeneza homoni za estrogen na progesterone, ambazo husimamia hedhi na upevushwaji wa mayai hivyo tunaposema kukoma hedhi maana yake ovari kukoma kuachia yai kila mwezi na kusimama kuingia mwezini(kuona damu ya hedhi kila mwezi)

Kukoma hedhi ni sehemu ya kawaida ya mwili wa mwanamke kuzeeka na hutokea baada ya kufikia umri wa miaka 40. Lakini baadhi ya wanawake wangine wanaweza kukoma hedhi mapema zaidi, ikiwa ni matokeo ya upasuaji, kama hysterectomy, au uharibifu kwenye ovari, kama baada ya tiba ya chemotherapy hivyo Kukoma hedhi kabla ya miaka 40, kwa sababu yoyote ile huitwa premature menopause.

Tuelewe kuwa kukoma hedhi kwa kawaida hakusababishwi na upasuaji au madawa.
 Ni mabadiliko ya taratibu yaliyo kwenye hatua tatu:

. Perimenopause.
Hatua hii huanza miaka michache kabla ya kukoma hedhi (menopause), wakati ovari taratibu zinaanza kupunguza utengenezaji wa estrogen. Kipindi hiki huenda hadi unapokoma hedhi, pale ovari zinapokoma kuachia mayai. Katika mwaka 1 au 2 kabla ya kukoma hedhi, utengenezaji wa estrogen hupungua kwa kasi. Ni katika kipindi hiki, wanawake wengi huona dalili za kukoma hedhi.

. Menopause.
 Hapa ni wakati mwanamke anapona kuwa umepita mwaka mmoja tangu alipopata hedhi ya mwisho. Sasa ovari zilishaacha kutoa mayai na kutengeneza estrogen.

. Postmenopause.
Hatua hii ni miaka ya baada ya kukoma hedhi. Katika kipindi hiki, dalili za kukoma hedhi kama hot flashes hupungua kwa wanawake walio wengi. Lakini madhara ya kiafya yatokanayo na ukosefu wa estrogen huongezeka kadiri umri wa mwanamke unavyoongezeka.

VISABABISHI VYA MWANAMKE KUKOMA HEDHI MAPEMA

Kukoma hedhi mapema (premature menopause) kunaweza kusababishwa na urithi,
matatizo ya kinga za mwili (autoimmune disorders), au kutokana na tiba za
afya. Sababu nyingine zaweza kuwa:

. Premature ovarian failure.
Kwa kawaida, ovari hutengeneza vyote, estrogen na progesterone. Mabadiliko katika viwango vya homoni hizi mbili hutokea, kwa sababu zisizoeleweka, na kusababisha mayai kusimama kutengenezwa mapema. Hali hii ikitokea kwa mwanamke aliye chini ya miaka 40, huitwa premature ovarian failure. Tofauti na premature menopause, premature ovarian failure si lazima iwe ya kudumu.

. Induced menopause.
Hii hutokea pale ovari zinapoondolewa kwa upasuaji kwa sababu za kiafya, kama uterine cancer au endometriosis. Induced menopause huweza pia kutokea baada ya uharibifu wa ovari kwa tiba za mionzi au chemotherapy.

DALILI ZITAKAZOKUJULISHA MWANAMKE UPO KATIKA KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI

Wanawake wengi wanaokaribia kukoma hedhi wanapata hot flashes, yaani  ghafla kusika joto linalosambaa sehemu ya juu ya mwili, vikiambatana na hali ya kutahayari na kutokwa jasho. Hali hii huwa si kali sana kwa wanawake wengi lakini kwa wengine huwa mbaya.

Dalili nyingine zinazotokea mwanamke anapokaribia kukoma hedhi ni pamoja na:

. Hedhi zisizo na mpangilio au zinazorukaruka
. Kukosa usingizi
. Kusikia hasira mara kwa mara
. Uchovu
. Mfadhaiko
. Moyo kwenda mbio
. Maumivu ya kichwa
. Maumivu ya joints na misuli
. Mabadiliko katika kusikia hamu ya tendo la ndoa
. Uyabisi wa uke
. Shida kudhibiti haja ndogo

Si wanawake wote wanaopata dalili hizi zote.

MADHARA YANAYOPATIKANA MWANAMKE AKIKOMA HEDHI

Matatizo Ya Muda Mrefu Yanaweza kutokea baada ya Kukoma Hedhi kwa
Kukosekana kwa estrogen ndani ya damu kunakosababishwa  na kukoma hedhi kumethibitika kusababisha baadhi ya matatizo ya kiafya yanayowapata wanawake wanapokuwa na umri mkubwa.
Matatizo hayo ni
. Maumivu ya nyonga kwa muda mrefu
. Magonjwa ya moyo
. Kibofu cha mkojo kutofanya vizuri na matatizo ya haja kubwa
. Hatari ya kupata ugonjwa wa kupotteza kumbukumbu
. Mikunyanzi ya ngozi
. Kukosa nguvu za mikono
. Kupungua kwa nguvu ya kuona.
. maumivu ya miguu

TATIZO LA KUTOKWA DAMU KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI(POSTMENOPAUSE BLEEDING)

Kawaida mwanamke akiwa ameshaingia kipindi cha kukoma hedhi hapaswi kuona tena damu ikitoka kwakua kukoma hedhi maana yake, kutotokwa na damu kwa kipindi kizima cha mwaka mmoja hivyo Ukiona damu hata kama ni vijitone tu unashauriwa kumwona daktari, ili ajiridhishe kuwa si tatizo kubwa, kama vile saratani ya kizazi nk

 CHANZO CHA KUTOKWA DAMU KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI(POSTMENOPAUSE BLEEDING)

Mambo mengi yanaweza kuwa sababu ya damu Kutoka wakati wa postmenopause nayo ni
Polyps
Hivi ni vivimbe vya tishu vinavyoota ndani ya nyumba ya uzazi au mkondo wa shingo ya uzazi, au kwenye cervix. Kwa kawaida si saratani, lakini vinaweza kusababisha vitone vya damu, kutoka damu nzito, au damu baada ya tendo la ndoa.



. Endometrial atrophy (thinning of the uterine lining):
Endometrium ni tishu inayotanda juu ya nyumba ya uzazi (uterus). Hupokea ishara za homoni kama estrogen na progesterone. Viwango vidogo vya homoni wakati wa postmenopause huweza kuifanya isinyae na kuwa nyembaba sana. Hii inaweza kusababisha kutoka damu.

. Endometrial hyperplasia (thickening of the uterine lining):
Baada ya kukoma hedhi, unaweza kuwa na estrogen nyingi zaidi na progesterone kidogo sana. Hali hiyo inaweza kupelekea endometrium kuwa nene zaidi na kutoa damu. Wakati mwingine seli ndani ya endometrium zinaweza kugeuka na kuwa si za kawaida. Hii inaweza kuleta saratani.

. Vaginal atrophy (thinning of vaginal tissue): Estrogen husaida katika afya ya uke. Baada ya kukoma hedhi, upungufu wa estrogen unaweza kusababisha
kuta za uke kusinyaa, kuwa kavu, na kuvimba. Hali hii mara nyingi husababisha kutoka damu baada ya tendo la ndoa.

. Cancer:
 Kutoka damu ni dalili inayoashiria zaidi uwepo wa saratani ya endometrium au uterus. Inaweza pia kuwa ishara ya saratani ya uke au saratani ya shingo ya kizazi.

. Sexually transmitted diseases:
 Baadhi ya magonjwa, kama ya chlamydia na gonorrhea, yanaweza kusababisha kutoka matone ya damu na damu baada ya tendo la ndoa.

. Madawa:
 Kutoka damu mara nyingi ni madhara yanayotokana na matumizi ya madawa, kama dawa za hormone therapy, tamoxifen, na dawa za kuifanya damu kuwa nyepesi.


MATIBABU YA TATIZO LA KUTOKWA DAMU KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (POSTMENOPAUSE BLEEDING)

Matibabu ya tatizo hili hutegemea chanzo kilichosababisha mgonjwa kutokwa damu.
Hivyo matibabu hutolewa kama ifuatavyo
. Estrogen therapy: Homoni hii hutolewa ili kutibu kusinyaa kwa uke au utando wa juu ya nyumba ya uzazi (vaginal and endometrial atrophy.) Daktari anaweza kushauri matumizi ya:

. Vidonge vya kunywewa
. Cream ya ukeni: Kifaa maalumu kitatumika kuingiza cream hii mwilini
. Vaginal ring: Namna ya pete ambayo daktari ataiweka kwenye uke. Pete hii hutoa estrogen kwa miezi 3.
. Vaginal tablet: Utakiweka ukeni kutumia kifaa maalumu. Utatakiwa kuweka kila siku, au mara chache katika wiki.

. Progestin therapy: Hii ni namna ya progesterone iliyotengenezwa kwenye maabara inayotumika kutibu endometrial hyperplasia. Dakatri anaweza kukuandikia vidonge au sindano, cream ya ukeni , au kifaa cha kuweka kwenye nyumba ya uzazi.

. Hysteroscopy: Njia hii huweza kuondoa polyps. Madaktari huitumia kuondoa sehemu zilizovimba za utando wa nyumba ya uzazi kutokana na endometrial hyperplasia. Ataingiza hysteroscope kupitia uke na kupitisha vifaa vidogo vya upasuaji kupitia kijibomba.


. D&C (dilation and curettage): Katika upasuaji wa aina hii, madaktari huipanua cervix. Kisha hutumia kifaa chembamba kuondoa polyps au sehemu zilizotuna za uterus zilizosababishwa na endometrial hyperplasia.

. Hysterectomy: Upasuaji huu huondoa sehemu au tumbo lote la uzazi. Hii ni tiba kwa saratani ya endometrium au cervix. Wakati mwingine, daktari ataamua kuondoa ovari zako, mirija ya uzazi, au sehemu za karibu (lymph nodes).

. Radiation, chemotherapy, and hormone therapy: Unaweza kupewa tiba zaidi ya kansa baada ya upasuaji. Daktari ataamua cha kufanya kutokana na aina ya kansa uliyo nayo na ipo katika hatua gani.

. Madawa: Daktari anaweza kukuandikia dawa kama za antibiotics kwa magonjwa ya ngono. Dawa hizi zinaweza pia kutibu maambukizi kwenye cervix au tumbo la uzazi.

MAMBO YA KUZINGATIA ILI UEPUKANE NA MADHARA YA KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI

Kuna mambo ya kuzingatia na  hatua za kuchukua ili mwanamke uliye kwenye postmepause ujisikie vizuri na kuwa mwenye afya nzuri.

. Epuka kuvuta sigara, kafeini (kiambato ndani ya kahawa na chai), pombe, chumvi nyingi, na sukari
. Kula mlo kamili (balanced diet)
. Tumia calcium kuweka imara mifupa yako na kuepukana na ugonjwa wa osteoporosis
. Tumia pia vitamini D kuimarisha mifupa
. Fanya mazoezi, kila siku, angalau dakika 30(zingatia swala la uzito)
. Tumia chakula chenye mafuta kidogo (low saturated fat and cholesterol.)

 MAMBO YA KUFANYA KUPUNGUZA HOT FLASHES

Hot flashes ni dalili inayojionyesha zaidi kwa mwanamke aliyekoma  hedhi. Mwanamke hupatwa na vipindi vya joto la ghafla, sehemu za juu za mwili likiambatana na jasho. Hapa chini ni vidokezi vya namna ya kukabiliana hali hiyo:

. Epuka kuvaa nguo nyingi na lala sehemu zenye ubaridi
. Epuka kula chakula cha moto na chenye viungo vingi
. Epuka kunywa pombe
. Punguza mawazo
. Kula chakula chenye soya


MAMBO YA KUFANYA KUPUNGUZA UKAVU UKENI 

. Mwanamke akikoma hedhi asilimia kubwa huwa wakavu ukeni hivyo tunawashauri kutumia vilainishi na vitu vya kuongeza unyevunyevu (moisturizers.)ukeni
. Mwombe daktari akuongoze kuhusu vitu vinavyoongeza estrogen.


MAMBO YA KUFANYA KUPUNGUZA TATIZO LA MIFUPA

Ili kuweza kuepukana na matatizo ya mifupa inashauriwa kutumia calcium na vitamini D ya kutosha Pamoja na kufanya mazoezi


YA MAMBO YA KUFANYA ILI KUPUNGUZA MATATIZO YA MAGONJWA YA MOYO 

Yamkini ya kupata magonjwa ya moyo huongezeka umri unapokuwa mkubwa,mambo muhimu ya kuzingatia kulinda moyo wako ni pamoja na:

. Chukua vipimo vya cholesterol na blood pressure kila wakati
. Chukua hatua za kupunguza cholesterol na kunguza blood pressure kama vimepanda.
. Kama una kisukari, iweke sawa sukari yako kila wakati
.udhibiti uzito wako

MATIBABU YA MATATIZO YA HEDHI NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo lolote linalohusu hedhi,uzazi na magonjwa mbalimbali na umejaribu njia  kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa matatizo mbalimbali ya  hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre