FAHAMU CHANZO CHA TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA HEDHI KWA MUDA MREFU, DALILI NA MATIBABU YAKE(AMENORRHEA)


CHANZO CHA MWANAMKE KUKOSA HEDHI KWA MUDA MREFU NA MATIBABU YAKE (AMENORRHEA)



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul nina imani wewe ndugu yangu msomaji wa makala hii unaendelea vyema nami nakuombea MWENYEZIMUNGU akujaze afya iliyo njema zaidi na baraka katika maisha yako

Katika mfululizo wa mada zetu za mzunguko wa hedhi wiki iliyopita tulijadili maana ya mzunguko wa hedhi na jinsi ya kujua siku za hatari
 leo tutajadili tatizo la kukosa hedhi kwa muda mrefu ambapo kitaalamu huwa tunaita amenorrhea.
Mwanamke anakuwa na tatizo hilo pale ambapo anakosa hedhi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo, au msichana ambaye hajaanza kupata hedhi akiwa na umri wa miaka 15.

Sababu ya kawaida ya kukosa hedhi ni ujauzito. Sababu nyingine ya kukosa hedhi ni dosari katika viungo vinavyojenga mfumo wa uzazi au tezi zinazosaidia kudhibiti viwango vya homoni katika mwili. Tiba ya chanzo cha tatizo mara nyingi huondoa tatizo hili la mwanamke kukosa hedhi.

Amenorrhea hugawanywa katika aina mbili ambazo ni  Primary amenorrhea na Secondary Amnorrhea

. Primary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi na mabadiliko ya kijinsia (kama kuota maziwa na kuota mavuzi) kwa msichana wa miaka 14 au kukosekana kwa hedhi kukiwa na mabadiliko ya kijinsia kwa msichana wa miaka 16.

. Secondary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi kwa mwanamke ambaye awali alikuwa anapata hedhi lakini baadaye akasimama kwa miezi 3 au zaidi bila ya kuwa na ujauzito, bila ya kuwa na maziwa ya kunyonyesha, bila kuzuia mzunguko wa wa hedhi kwa vidonge, au kukoma hedhi.

Ili mwanamke awe na mzunguko wa hedhi mzuri, hypothalamus, tezi ya pituitary, ovari, na uterus vyote vinatakiwa vifanye kazi ipaswavyo. Hypothalamus huiamuru tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating (FSH) na luteinizing (LH). FSK na LH husababisha ovari kutoa homoni za estrogen na progesterone. Estrogen na progesterone zinahusika katika mzunguko wa mabadiliko katika endometrium (utando unaofunika uterus), pamoja na hedhi. pamoja na hayo yote, mkondo wa uke lazima uwe wazi ili kuruhusu damu ya hedhi.


 VISABABISHI VYA KUKOSA HEDHI KWA MUDA MREFU(AMENORRHEA)


Amenorrhea inaweza kutokea kwa sababu nyingi. Baadhi zikiwa ni za kawaida katika maisha ya mwanamke, wakati nyingine zikisababishwa na matumizi ya madawa au zikiwa ni ishara ya tatizo la kiafya. Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababishwa na dosari yo yote kwenye hypothalamus, pituitary, ovari, mkondo wa uke au ya kiutendaji kimwili.

Sababu za kawaida

. Ujauzito
. Kunyonyesha
. Kukoma hedhi

Dawa za Kuzuia Mimba

Wanawake wengine wakitumia vidonge vya kuzuia mimba hukosa hedhi. Hata baada ya kuacha matumizi ya vidonge hivyo, huwachukua muda miili yao kurudi kwenye hali za kawaida na kuanza kuona hedhi zao. Njia za sindano au kupandikiza zaweza pia kuleta tatizo la kukosa hedhi.

Mitindo Ya Maisha

Baadhi ya mitindo ya maisha huweza kuchangia mwanamke kukosa hedhi. Kwa mfano:

. Kuwa na uzito mdogo sana. Kuwa na uzito mdogo kupita kiasi – asilimia 10 chini ya uzito wa kawaida – husimamisha shughuli nyingi za homoni ndani ya mwili, hivyo kusimamisha uzalishaji wa mayai

. Mazoezi zaidi ya kawaida. Wanawake wanaoshiriki shughuli zinazodai mazoezi ya juu, hujikuta wakipoteza hedhi zao. Baadhi ya sababu zinachangia kwa wanariadha, ikiwa ni pamoja na uzito mdogo, kuwa na mafuta kidogo ndani ya mwili, msongo wa mawazo na matumizi makubwa ya nishati ya mwili.

. Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo huweza kubadilisha kwa muda utendaji kazi wa hypothalamus – sehemu ya ubongo inayosimamia homoni zinazoratibu hedhi. Uzalishaji wa mayai na hedhi, hivyo vyaweza kusimama. Hedhi za kawaida hurudi baada ya msomgo wa mawazo kupungua.

Kukosa Uwiano Wa Homoni

Matatizo kadhaa katika viungo vya mwili huweza kuvuruga mpangilio wa homoni katika mwili, ikiwa ni pamoja na:


Sababu Zinazotokana Na Hypothalamus
. Uvimbe karibu na tezi ya pituitary (Craniopharyngioma)
. Kallman syndrome (upungufu wa gonadotropins, homoni zenye uwezo wa kusimamia ukuaji na ufanyaji kazi wa viungo vya uzazi )
. Upungufu wa lishe
. Uzito mdogo au kuchelewa kukua

Sababu Za Tezi Ya Pituitary
. Uwingi wa homoni ya prolactin, homoni inayosimamia utoaji wa maziwa wakati mama ananyonyesha, katika damu. Hali hii kitaalamu huitwa prolactilemia na husababishwa na uvimbe (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.

. Dosari zinazoanzia kwenye uvimbe wa aina nyingine wa kwenye pituitary (kama, cushing syndrome, acromegaly, au thyroid-stimulating hormone)
. Kufa kwa seli za pituitary baada ya mwanamke kujifungua

. Seli za pituitary kufa baada ya kushambliwa na kinga za mwili (autoimmune hypophysitis)

. Uvimbe ndani ya tezi ya pituitary

. Ugonjwa ambao hushambulia pituitary (sarcoidosis)

Sababu Zinazotokana Na Ovari

. Kutozalishwa kwa mayai (anovulation)

. Kuwa na uwingi wa homoni za kiume ndani ya damu (hyperandrogenemia)

. Kuvurugika kwa homoni (Polycystic ovary syndrome)

amenorrhea polycystic ovarian syndrome

. Kufeli kwa ovari mapema

. Ugonjwa wa kurithi unaodumaza ovari,  kuzuia hedhi (Turner syndrome)

. Seli za ovari kushambuliwa na kinga za mwili (Autoimmune oophoritis)

. Mionzi au tiba za chemotherapy

. Ugonjwa wa kurithi unaojaza galactose ndani ya damu (Galactosemia)

. Dosari za kimaumbile katika mkondo wa njia ya uzazi

Sababu za Kiutendaji

. Kuwa na uzito mdogo kwa sababu ya kuogopa kula (anorexia)/kula kupita kiasi (bulimia)

. Magonjwa sugu kama TB

.Kunenepa au kukonda kupita kiasi

. Utapiamlo

. Mfadhaiko au matatizo mengine ya kiakili

. Msongo wa mawazo wa kupitiliza

Matatizo Ya Kimaumbile

Matatizo katika viungo vya uzazi yanaweza kusababisha amenorrhea. Mifano ni kama:

Makovu kwenye tumbo la uzazi. Tatizo lilitwalo Asherman’s syndrome – kujenga kwa makovu juu ya ngozi ya juu ya uterus – huweza kutokea baada ya oparesheni ya uzazi, au baada ya tiba ya fibroids. Makovu kwenye uterus huzuia ujenzi wa kawaida na kujibandua kwa ngozi hiyo ya juu.

Kukosa Viungo Vya Uzazi. Wakati mwingine matatizo yanaanzia kwenye ukuaji wa mtoto tumboni yanayosababisha msichana azliwe bila baadhi ya viungo vya uzazi, kama uterus, cervix au uke. Kwa sababu viungo vyake havikukua vizuri, haweza kupata hedhi.

Dosari Za Kimamumbile Za Uke. Kitu kitakachoziba njia ya uke kinaweza kusababisha kuonekana kwa hedhi ya wazi. kunaweza kukatokea utando au ukuta katika uke ambao utazuia utokaji wa damu kutoka kwenye uterus na cervix.


DALILI ZITAKAZOKUJULISHA KAMA UNA AMMENORRHEA

Amenorrhea ni dalili ya kuwa kuna tatizo lililochificha na si ugonjwa Wenyewe. Dalil nyingine huweza kutokea kulingana na chanzo cha tatizo hilo la kukosa hedhi.

. Kutoka maziwa kwa mwanamke ambaye hana ujauzito, hali ambayo kitaalamu huitwa Galactorrhea, maumivu ya kichwa, kutokuona vizuri kingo za vitu vinaweza kuwa dalili za uvimbe ndani ya fuvu la kichwa.

. Kuongezeka kwa uotaji wa nywele kwa mtindo wa kiume (hirsutism), sauti nzito, chunusi kunaweza kusababishwa na kuzidi kwa androgen (homoni inayochangaia ujenzi wa tabia za kiume).

. Uyabisi wa uke, vipindi vya mwili kuwa na joto, kutoa jasho usiku, kukosa usingizi mzuri vinaweza kuashiria dasari katika ovari au kufeli kwa ovari.

. kuongeza kwa mwili au kukonda.
. Kuwa na wasiwasi kunaweza kujitokeza kwa mwanamke mwenye matatizo ya kiakili

VIPIMO NA UCHUNGUZI WA TATIZO LA AMENORRHEA



Msichana yeyote aliyefikia umri wa kubalehe na kuvunja ungo na ambaye bado hajaanza kupata mabadiliko yeyote ya kubalehe katika mwili wake hana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aidha msichana aliyefikia umri wa miaka 16 na ambaye bado hajaanza kupata hedhi anatakiwa pia kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa wanawake waliokuwa wakipata hedhi kama kawaida lakini ghafla wakaacha kupata kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi nao pia hawana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hili.
Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:
  • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.
  • Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.
  • CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.
  • Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid
  • Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
  • Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.
Matibabu ya kukosa hedhi
Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kufanyika nyumbani bila kuhitaji dawa, ingawa pia, kutegemeana na chanzo cha tatizo, yanaweza kuhitaji dawa na hata upasuaji wakati mwingine.
Matibabu yasiyohitaji dawa
  • Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo la kukosa hedhi kwa sababu ya kujinyima kula (wanaofanya dieting) na hivyo kupata upungufu wa virutubisho mwilini, wanashauriwa kula lishe bora.
  • Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo hili la kukosa hedhi kwa sababu ya kuongezeka uzito kupitiliza, wanashauriwa kuwa makini katika aina ya vyakula wanavyokula ili kuwa na uzito unaotakiwa.
  • Wanawake wanaokosa hedhi kwa sababu ya kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi wanashauriwa kujiwekea kiasi katika ufanyaji wao wa mazoezi.
  • Iwapo kukosa hedhi kumesababishwa na msongo wa mawazo, ni jambo jema kutafuta njia za kushughulikia matatizo hayo na kuyatatua ili kuondoa msongo wa mawazo
  • Inashauriwa kutokuvuta sigara na kuacha kunywa kunywa pombe.
Matibabu yanayohitaji dawa
Matibabu ya kukosa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo. Matibabu huelekezwa katika kutibu chanzo, na iwapo chanzo cha tatizo ni matatizo ya kimaumbile, upasuaji unaweza kufanyika.
Kwa wanawake wenye matatizo ya kuwa na kiwango kingi cha prolactin, daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa aina ya bromocriptine au pergolide.
Kwa wanawake wenye upungufu wa homoni ya estrogen au wale wenye matatizo katika ovary zao, dawa zenye kurejesha homoni hiyo zaweza pia kutumika. Wakati mwingine dawa za uzazi wa mpango zaweza kutumika kurejesha mzunguko wa hedhi na pia kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.
Upasuaji
Upasuaji unaweza kufanywa iwapo kuna
  • Uvimbe katika ubongo unaoathiri tezi ya pituitary na hypothalamus
  • Matatizo katika njia ya uzazi ya mwanamke
 MADHARA YA KUKOSA HEDHI YANAWEZA KUSABABISHA KUKOSA MTOTO
Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa

MATIBABU YA MATATIZO YA KUKOSA HEDHI NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo lolote linalohusu hedhi,uzazi na magonjwa mbalimbali na umejaribu njia hizo kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la  hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako Pia tutakuelimisha vyakula vinavyohitajika kurekebisha homoni mwilini 
Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI


KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre