FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA MAUMIVU KABLA YA HEDHI(PREMENSTRUAL SYNDROME )NA MAUMIVU YANAYOTOKEA KIPINDI CHA HEDHI(DYSMENORRHEA)

FAHAMU CHANZO CHA MAUMIVU KABLA YA HEDHI (PREMENSTRUAL SYNDROME) NA MAUMIVU YANAYOTOKEA KIPINDI CHA HEDHI(DYSMENORRHEA)



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul
Nina imani sote tuko salama Ashukuriwe Mwenyezimungu kwa kutupa pumzi
Wiki iliyopita tulijadili tatizo la kukosa  hedhi kwa muda,leo Katika mfululizo wa mada zetu,tutazungumzia matatizo yanayoambatana na hedhi. Wanawake wengi hupata matatizo kabla ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi na mara ya baada ya kukoma hedhi.
 Katika kila moja ya hayo, tutajaribu kuona sababau za tatizo na jinsi ya kuepuka tatizo hilo.
Tunaanza kwa kulitazama tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi (Premenstrual syndrome).

MAUMIVU KABLA YA HEDHI(PREMENSTRUAL SYNDROMES)

Ni hali ambayo humwathiri mwanamke kihisia, afya yake na mwili na tabia yake katika kipindi fulani cha mzunguko wake wa hedhi, kwa kawaida kabla tu ya kuingia mwezini. Tatizo hili ni la kawaida kwa wanawake na huathiri karibu asilimia 85 ya wanawake wanaopata hedhi. Maumivu huanza siku 5 hadi 11 kabla ya kuanza hedhi.

Kuna mlolongo wa dalili za tatizo hili la maunmivu kabla ya hedhi, lakini mwanamke anaweza kupata baadhi ya dalili zifuatazo:

Dalili Za Kihisia Na Kitabia

shida za hedhi
. Kuwa na msongo wa mawazo au wasiwasi
. Kuwa na mfadhaiko
. Kulialia
. Madadiliko ya mara kwa mara ya kihisia na hasira
. Mabadiliko ya ulaji na kupenda sana kula
. Matatizo ya kupata usingizi
. Kujitenga na jamii
. Kushindwa kutuliza mawazo



Dalili Na Mabadiliko Katika Maumbile ya Mwili


. Maumivu kwenye maungio ya mifupa na misuli
. Kuumwa kichwa
. Uchovu
. Kunenepa
. Maumivu kwa mbali maziwa yakiguswa
. Kuchipuka kwa chunusi
. Kukosa choo au kuharisha

Kwa baadhi ya wanawake, mabadiliko haya ya kitabia na maumivu ya mwili yanaweza kuwa makubwa kiasi cha kuathiri shuguli zao. Pamoja na kuwa wengine huathirika sana, matatizo haya huisha ndani ya siku nne baada ya kuanza hedhi.

Kwa wanawake wachache, maumivu haya ya kabla ya hedhi huwafanya washindwe kabisa kuendelea na shughuli zao za kila siku, na huwatokea kila mwezi. Aina hii ya PMS huitwa premenstrual dysphoric disorder (PMDD).

Dalili za premenstrual dysphoric disorder ni pamoja na mfadhaiko, hisia za ghafla zinazobadilika, hasira, wasiwasi, kushindwa kufikiri, hasira za ghafla na kuwa na msongo wa mawazo.


CHANZO CHA MAUMIVU KABLA YA HEDHI (PREMENSTRUAL SYNDROME)


Chanzo kamili cha tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi hakijathibitika, lakini sababu zifuatazo zimeonyesha kuwa na mchango mkubwa:

. Mabadiliko Katika Mzunguko Wa Homoni. Dalili za maumivu kabla ya hedhi zinabadilika na mabadiliko ya homoni katika mzunguko wa hedhi. Viwango vya homoni ya estrogen na progesterone huongezeka wakati fulani katika mwezi. Mwongezeko huu husababisha mabadiliko ya mara kwa mara ya namna mwanamke atakavyojisikia, kuleta wasiwasi na kusababisha hasira za haraka.

. Mabadiliko ya viwango vya kemikali katika ubongo. Mabadiliko katika viwango vya serotinin katika ubongo vinaaminika kusababisha premenstrual syndrome. Viwango vya Serotinin huathiri namna mwanamke atakavyojisikia. Serotinin ni kemikali katika ubongo inayoamsha namna ya kujisikia, hisia na mawazo. Kuwa na kiwango kidogo cha serotinin kunasababisha mfadahiko, uchovu, kupenda kula sana na kukosa usingizi.

. Mfadhaiko. Wanawake wengine waliobanika kuwa na matatizo mazito ya maumivu kabla ya hedhi, walikuwa na mfadhaiko, ingawa mfadhaiko huo haukuwa sababu ya matatizo yao yote.

Mambo Ya Kufanya Kupunguza Maumivu Ya Kabla Ya Hedhi

Mpendwa msomaji unaweza kuondokana au kupunguza makali ya tatizo la maumivu kabla ya hedhi kwa kufanya mabadiliko katika namna ya kula, kufanya mazoezi na namna unavyoishi kwa ujumla. Unaweza kujaribu yafuatayo:

Badili Namna Ya Kula

. Punguza mlo, kula mara nyingi zaidi kuzuia tumbo kuvimba na hali ya kujisikia tumbo limejaa

. Punguza chumvi na chakula chenye chumvi nyingi kuzuia tumbo kujaa
. Chagua chakula chenye complex carbohydrates, kama matunda, mboga za majani na nafaka nzima

. Chagua chakula chenye uwingi wa calcium
. Jizuie kutumia kahawa na pombe

Jipangie Ratiba Ya Mazoezi Ya Mwili

Panga ratiba ya kutembea angalau kwa dakika 30, kuendesha baiskeli, kuogelea au mazoezi mengine ya kukutoa jasho siku kadhaa kwa wiki. Mazoezi ya kila  siku yataboresha afya yako na kukuondolea baadhi ya dalili, kama uchovu na mfadhaiko.

Punguza Msongo Wa Mawazo

. Pata usingizi wa kutosha
. Fanya mazoezi ya misuli au upumuaji mzito ili kuondoa maumivu ya kichwa, wasiwasi na matatizo ya kukosa usingizi
. Jaribu kufanya yoga au massage ili kuondoa msongo wa mawazo.

TIBA YA MAUMIVU KABLA YA HEDHI


Kwa wanawake walio wengi, kubadli mtindo wa maisha kunaweza kuwasaidia kuondokana na PMS. Kulingana na ukubwa wa tatizo, daktari anaweza kukuandikia dawa moja au zaidi ya dawa za kusaidia PMS. Utendaji kazi na msaada wa dawa hizi hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine. Dawa ambazo hutolewa ni pamoja na:

. Antidepressants
. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs)
. Diuretics

Tiba Mbadala Ya Maumivu Kabla Ya Hedhi
Kuna vitu vinafahamika kuondoa au kupunguza makali ya tatizo la maumivu kabla ya hadhi:

. Calcium. Kupata calcium ya kutosha katika mlo au matumizi ya vidonge vya calcium kunaweza kuondoa dalili za maumivu kabla ya hedhi – premenstrual syndrome.
. Magnesium. Kutumia magnesium kila siku kutasaidia kuondoa maumivu ya kwenye maziwa na kujaa kwa tumbo kunakoambatana na premenstrual syndrome.

. Vitamin E. Matumizi ya vitamini E ya kila siku yanaweza kuondoa PMS kwa kuzuia utengenezaji wa prostaglandins, namna ya homoni inayosababisha mkakamao wa misuli na maumivu kwenye maziwa.

. Tiba ya mimea. Baadhi ya wanawake wameeleza kupata nafuu ya PMS kwa kutumia mimea kama ginkgo, tangawizi, chasteberry na mingine ingawa njia hii haijathibitishwa na vyombo vya kusimamia chakula na dawa.

Mpendwa msomaji hapo juu tumeona Maumivu yanayotokea kabla ya hedhi hivi sasa tutazungumzia maumivu wakati wa hedhi ambayo huitwa menstrual cramps au kitaalamu Dysmenorrhea.

MAUMIVU YANAYOTOKEA KIPINDI CHA HEDHI (MENSTRUAL CRAMPS/DYSMENORRHEA)

 ni maumivu ya kukakamaa kwa misuli ya eneo la chini ya tumbo. Wanawake wengi hupata maumivu haya kabla kidogo au wakati wakiwa kwenye siku zao. Kwa baadhi ya wanawake, maumivu haya huwa ni ya kuwakosesha raha. Kwa wengine, huwa ni makubwa kiasi cha kuwafanya washindwe kuendelea na shughuli zao za kila siku kwa siku kadhaa kila mwezi.
Maumivu haya yamegawanyika katika makundi mawili nayo ni  yafuatayo ;

Primary dysmenorrhea ni maumivu ya wakati wa hedhi ambayo hujirudiarudia kila mwezi na ambayo hayatokani na magonjwa mengine ya mwili. Maumivu haya ya wakati wa hedhi ambayo hayana sababu za kueleweka, hupungua kadri mwanamke anavyozidi kuwa na umri mkubwa na mara nyingi hupungua sana mara baada ya kuzaa.

Secondary dysmenorrhea ni maumivu ya wakati wa siku za mwanamke ambayo yanatokana na dosari katika viungo vya uzazi vya mwanamke, kama endometriosis, adenomysis, uterine fibroids au maambukizi ya wadudu.

CHANZO CHA MAUMIVU YANAYOTOKEA KIPINDI CHA HEDHI(DYSMENORRHEA)


Wakati wa hedhi, nyumba ya uzazi hujiminya ili kuondoa utando wake wa juu. Vitu vilivyo mfano wa homoni – prostaglandins – vinavyohusika na maumivu na uvimbe, huchagiza kujiminya kwa misuli ya nyumba ya uzazi (uterus). Uwepo wa prostaglandins kwa wingi kunahusishwa na maumivu makali ya hedhi.
Kujiminya kwa misuli yangu uterus kukiwa kwa kiwango kikubwa mno, kunaweza kuziba mishipa ya damu inayoilisha nyumba ya uzazi (uterus). Maumivu yatokanayo yanaweza kulinganishwa na maumivu ya kifuani wakati mishipa ya damu ikiziba na kusababisha baadhi ya sehemu za moyo kukosa chakula na oksijeni.
Maumivu ya wakati wa hedhi yanaweza pia kusababishwa na:
. Endometriosis. Hii ni hali ambapo tishu ambazo kwa kawaida hujenga ndani ya uterus, zinajenga nje , hasa kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes), kwenye ovari au juu ya tishu zinazofunika pelvis.
. Uterine fibroids. Uvimbe usio wa saratani juu ya ngozi ya nyumba ya uzazi waweza kuleta maumivu.
. Adenomyosis. Hali hii ni pale tishu zinazofunika uterus zinapojijenga kwenye misuli ya kuta za uterus.
. Pelvic inflammatory disease (PID). Maambukizi kupitia ngono ya bakteria kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.
. Cervical stenosis. Baadhi ya wanawake wana vijitundu vidogo mno vya kwenye cervix vinavyozuia mtiririko wa damu wakati wa hedhi na kusababisha maumivu kutokana na msukumo wa ndani ya nyumba ya uzazi.

Dalili Za Maumivu Ya Hedhi (Menstrual Cramps)

. Maumivu ya kukakamaa kwa misuli sehemu ya chini ya tumbo yanayoweza kuwa makali
. Kichwa kizito na maumivu ya kichwa endelevu
. Maumivu yanayoenea sehemu za mgongoni na kwenye mapaja
Wanawake wengine hupata:
. Kichefuchefu
. Haja kubwa mara kwa mara
. Maumivu ya kichwa
   Kizunguzungu

Tiba Ya Maumivu Ya Hedhi

Maumivu ya wakati wa hedhi yana tiba tofauti. Daktari anaweza kukupa:
. Dawa za kupunguza maumivu.
Daktari anaweza kukushauri kutumia dawa za kupunguza maumivu unapoanza siku zako au mara unapoanza kusikia dalili za maumivu na kuendelea kuzitumia dawa hizo kwa siku 2 au 3, hadi dalili zinapoondoka.
. Hormonal birth control. Vidonge vya kunywa vya uzazi wa mpango vina homoni inayozuia upevushwaji wa yai na kuondoa maumivu ya hedhi. Homoni hizi zinaweza kutolewa kwa njia nyingine kama sindano, kitu cha kuvaa juu ya ngozi, kitu kinachowekwa chini ya ngozi ya mkono au namna ya pete laini inayoingizwa ukeni.
. Upasuaji. Kama matatizo yako yanasababishwa na kitu kinachoeleweka kama endometriosis au fibroids, upasuaji unaweza kuondoa matatizo ya maumivu ya hedhi. Upasuaji kuondoa nyumba ya uzazi (uterus) unaweza kuwa ni chaguo endapo hufikirii kuendelea kuzaa.

Mambo Ya Kufanya Kuondoa Maumivu Ya Wakati Wa Hedhi

Unaweza kufanya yafuatayo kujaribu kuondoa au kupunguza maumivu ya wakati wa hedhi:
. Mazoezi. Utafiti umeonyesha kuwa mazoezi ya mwili yanapunguza maumivu ya hedhi.
. Joto. Kutumbukia kwenye bafu la maji ya moto au kutumia chombo cha kupasha moto sehemu za chini ya tumbo kunaweza kupunguza maumivu ya wakati wa hedhi. Upashaji huu wa moto sehemu za tumboni unaweza kufanya kazi vizuri sawa na kutumia dawa za kuondoa maumivu haya.
. Chakula. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa matumizi ya vitamini E, omega-3 fatty acids, vitamini B-1 (thiamine), vitamini B-6) na magnesium yanaweza kuondoa maumivu ya wakati wa hedhi.

. Kuacha pombe na tumbaku. Vitu hivi vinaweza kuongeza makali ya maumivu ya wakati wa hedhi.
. Kupunguza msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unaweza kuongeza uwezekano wa kupata maumivu ya hedhi au kuongeza makali ya maumivu hayo.

MATIBABU YA MATATIZO YA MAUMIVU YA HEDHI NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo lolote linalohusu hedhi,uzazi na magonjwa mbalimbali na umejaribu njia hizo kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la  hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre