FAHAMU CHANZO NA TIBA YA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI






FAHAMU CHANZO NA TIBA YA TATIZO LA kUTOKA HARUFU MBAYA UKENI


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,leo tutajadili mada hiyo hapo juu ambayo ni miongoni mwa matatizo yanayotusumbua katika jamii tunayoishi
Tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni ni moja ya matatizo yanayowasumbua wanawake wengi nchini na ni tatizo linalokera na gumu kuongeleka kutokana na wanawake wengi kuona aibu na kuhisi ni hali mbaya kwa mtu mwingine kuifahamu. 
Kutunza uke na kulinda afya ya uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke, kutokwa na harufu mbaya ukeni ni kiashiria kwamba unaumwa na hayuko sawa. Hali hii inaweza kuathiri heshima ya mwanamke na pia mahusiano na mwenza wake.
Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na bacteria wa vaginosis japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke. Kama wewe muhanga wa tatizo hili basi tambua kwamba kuna njia za asili unaweza kuzitumia ikiwemo lishe na ukarudi katika hali ya kawaida,kama tatizo litazidi kuendelea basi itatakiwa uende hospitali ili upate uchunguzi.
Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo ya samaki basi ujue kuna tatizo kubwa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaji au uchafu kama mtindi ukeni.

VISABABISHI NA VYANZO VYA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI

UKUAJI WA BACTERIA WA VAGINOSIS

Miongoni mwa sababu kuu ya kupata harufu mbaya ukeni ni ukuaji wa bacteria wa vaginosis,ukuaji wa bacteria usio wa kawaida kwenye uke husababishwa na kubadilika kwa mazingira ya ukeni na kushuka kwa kinga
 bacteria vaginosis ni chanzo namba moja kinachosababisha uke kutoa harufu mbaya.
Inawezekana ukawa msafi mpaka mwisho lakini ukisumbuliwa na hili tatizo basi lazima uke wako utatoa harufu mbaya.
Kila uke una bacteria ambao wapo naturally kwa ajili ya afya njema ya uke wako,Lakini kama ikitokea hawa Bacteria wakazidi na kuwa wengi kupita kiasi ambacho uke wako unaweza kuhimili ndipo tatizo hili hutokea

Sababu zinazosababisha bacteria vaginosis hazijulikani kwa usahihi lakini madaktari wanasema inaweza ikasababishwa na kitendo cha kupeana Raha na Utamu bila condom na hasa  kama vitu vilivyoingia kwenye uke wako wakati wa kupeana Raha na Utamu vilikuwa vichafu(mfano vidole au uume au dildo nk),lakini pia tatizo hili la ukuaji wa bacteria vaginosis hutokea bila sababu.

Ukitaka Kujua kuwa unasumbuliwa na bacterial vaginosis utajikuta unapata Dalili zifuatazo;

Uke kutoa maji maji mazito au mepesi yenye rangi ya njano au brown yenye harufu mbaya
Maumivu kwenye maeneo ya kiuno au nyonga
Unaweza usipate au ukapata maumivu ya kichwa.
Uke wako unaweza ukawa unawashwa au usiwashwe
Pia Ukuaji wa bacteria wa vaginosis ndani ya uke wanaweza kupelekea mimba kutoka, kujifungua kabla ya wakati na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine ya ngono. dalili mojawapo ya kwamba tayari una maambukizi ya bacteria ni kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali mfano wa harufu ya samaki wabichi


UGONJWA WA TRICHOMONIASIS

Trichomoniasis ni moja ya ugonjwa wa ngono unaosababisha harufu kali ukeni. Ugonjwa huu husababishwa vimelea na huambatana na kutokwa na uchafu ukeni,kuwasha, na maumivu makali wakati wa kukojoa. trichomoniasis inaweza kuwaathiri wajawazito na kuleta hatari ya mimba kutoka. Kama utagundua una Trichomoniasisi basi wewe na mwenza wako mnatakiwa kutibiwa. Hakikisha pia unatumia condom vizuri kila unapofanya ngono kama kinga dhidi ya magonjwa

MABADILIKO YA HOMONI

Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi huweza kuchangia harufu mbaya ukeni,wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wako kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana hivyo kusababisha tishu kuwa na tindikali kidogo

YEASTS INFECTIONS

Hili Pia ni Tatizo,lipo kama la Bacterial Vaginosis.tofauti yake ni kuwa kwenye Bacterial Vaginosis waliokuwa wamezidi ni bacteria lakini huku wanaozidi ni fungus candida albicans.
Ni wanawake wachache huwa wanapata Bacterial Vaginosis lakini wanawake wengi lazima wapate Yeast infection japo mara moja katika maisha yao.

Mara nyingi yeasts infection hutokea tu au inaweza kusababishwa na aina ya vyakula au vinywaji unavyokula au kunywa hasa kama vimejaa yeast(vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe etc)
Ukitaka kujua kama unasumbuliwa na yeast infection utajikuta unapata Dalili zifuatazo;

Uke wako ukawa unawashwa au usiwashwe
Maumivu kama uke unaungua pale unapokuwa unajisaidia haja ndogo
Uke kutoa maji maji mazito yenye rangi nyeupe kama jibini


KUTOZINGATIA USAFI 

Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya. Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (apocrine sweat glands )hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo kama kwapa, pua, ndani ya sikio, uke, na kwenye chuchu, bacteria waliopo maeneo hayo huchakata mafuta haya na hivo kuzalisha harufu kali. Uvaaji wa nguo zilizobana na uzito kupita kiasi huchangia kuhifadhiwa kwa jasho kwenye mikunjo ya ngozi na hivo kuleta harufu.

VAGINAL/CERVICAL CANCER(KANSA YA UKE/KANSA YA MLANGO WA KIZAZI)

Unapokuwa una kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi ni kawaida kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya ambayo ni sehemu ya dalili za kansa ya uke,.Unapojiona kuwa una tatizo la uke kutoa harufu mbaya,ni heri na itakuwa busara ukienda hospitali,kupima na kama ni kansa ya mlango wa kizazi itakuwa sio ngumu kuitibu kama ukiwahi mapema kuanza matibabu


  • KUVAA PEDI MOJA MUDA MREFU

Pedi inapovaliwa kwa muda mrefu husababisha ngozi kucharuka,kututumka na kuwasha na pia kuchangiwa kukua kwa bacteria na fangasi wabaya ambao ni chanzo cha harufu..

MATIBABU 
Matibabu ya tatizo hili hupatikana katika hospital zote nchini na matibabu hutolewa baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktar au nesi mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake
Dawa za kupaka(ointment/cream) na Dawa za kumeza (pills) huweza kumaliza tatizo hili
 Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari au nesi

MAMBO 6 UNAYOWEZA KUFANYA KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI

  1. Siku zote vaa nguo za ndani zisizobana sana na za pamba
Nguo zilizobana zinazuia kupita kwa hewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.
2.Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi
Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.
  1. Punguza uzito kama Inawezekana
Uzito mkubwa unakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na kama tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu  inaleta fangasi na bacteria wabaya.
  1. Epuka Kuflash Uke Kila Mara (Douching)
Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bacteria wazuri ambao ni walinzi, na hivo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bacteria wabaya pamoja na bacteria wa vaginosis
  1. Epuka Kutumia Spray na Marashi ili Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni au Kuweka Harufu Nzuri Ukeni.
    Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray kuingia kwenye damu. Usiingie kwenye mtego huu, kumbuka miili yetu imeumbwa kujisafisha yenyewe, Pale unapoongeza kitu cha ziada basi unaharibu normal flora na kuharibu kinga ya mwili.
  2. Epuka Baadhi ya Vyakula Ambavyo ni Adui wa afya yako
    Kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vinaweza kukuathiri wewe kama mwanamke kwenye swala la uzazi, vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bacteria wzuri na kubadili PH. Vyakula vyenye sukari, Pombe, ngano na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa bacteria wa vaginosis.

MAMBO YA KUFANYA ILI KUKATA HARUFU MBAYA UKENI

Harufu kali kwenye uke mara nyingi inagundulika zaidi baada ya kufanya ngono na pia kwenye hedhi. kwahiyo badala ya kukimbilia spray na kujisafisha ukeni ili kuondoa harufu tumia njia zifuatazo kwa muda kabla hujamuona dactari wako ama kupata Dawa za kutumia

APPLE CIDER VINEGAR (SIKI YA TUFAA

Vinegar imejaa viini ambavyo ni antibacterial na antiseptic ambavyo vitakusaidia kupambana na harufu hii kali. Chukua kiasi kidogo cha vinegar changanya na maji kwa uwiano wa 1/10  na uoshe eneo la uke. Tumia pia kiasi kingine kwa uwiano huo huo changanya na maji ya kunywa chukua glass moja kwa vijiko viwili vya apple cider vinegar na unywe kila siku.... NB siyo kila vinegar itakusaidia hakikisha unatumia Apple cider vinegar. 

MBEGU ZA UWATU(FENUGREEK SEEDS)
Loweka kijiko kidogo cha mbegu za uwatu (fenugreek seeds) ndani ya maji glasi moja na uache kwa usiku mzima. Kesho yake asubuhi maji haya yaliyolowekwa mbegu za uwatu kabla ya kula au kunywa chochote.
Uwatu husaidia kuweka sawa homoni za mwili na kuweka sawa mzunguko wa hedhi.

BAKING SODA(MAGADI SODA)
Baking soda inaweza kutumika ili kubalansi pH kwenye mwili. Kumbuka mwanzo tulivosoma kuhusu madhara ya kubadilika kwa pH. Ukibalansi pH basi tatizo la harufu kali linakuwa limeisha. Unaweza kutumia pia baking soda kama body spray na ukaepuka kujaza sumu mwilini. Chukua nusu kikombe cha baking soda weka kwenye beseni kubwa la maji ya kuoga kisha kaa tulia kwa dakika 15 mpaka 20 kwenye maji. Baada ya hapo Jifute kwa taulo sehemu zote usiache unyevu kabla ya kuvaa nguo

MAZIWA MTINDI
Chukua mtindi ujazo wa kijiko kidogo cha chai na tumbukize ndani ya uke wako na uache huko usiku mzima. Mtindi una bakteria wazuri wanaohitajika ukeni kuweka sawa usawa wa PH (alikalini na asidi) na hivyo kuondoa maambukizi,Pia unashauriwa kunywa maziwa mtindi mara mbili kwa siku kuongeza kinga ya mwili wako kwa ujumla dhidi ya magonjwa mbalimbali

MATUNDA NA MBOGAMBOGA

Matunda yenye uchachu mfano machungwa, mapera na strawberries yana Vitamn C kwa wingi sana ambayo huimarisha kinga ya mwili na kusaidia utoaji wa sumu mwilini. Chakula kama Parachichi na mboga za kijani ina Vitamn B6 na madini ya potasium ambayo huongeza hamu ya tendo la ndoa na kujenga kuta za uke hivo kuzuia hatari ya kushambuliwa mara kwa mara

KITUNGUU SAUMU
Kitunguu saumu kinafahamika tokea miaka ya zamani kwa uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kinga na kupambana na maambukiz ya bacteria na fangasi. Unaweza kula punje 6-10 za vitunguu saumu kwa siku ama ukatengeneza juice ya vitunguu saumu ukawa unakunywa asubuhi kabla ya kula chochote

KARANGA/ALIZETI NA MBEGU ZA MABOGA
Matumizi ya karanga na mbegu kwenye mlo wako wa kila siku huzuia kukauka kwa uke kwa sababu kuna Vitamin E kwa wingi. Unaweza kutafuna mbegu za maboga,karanga, na alizeti kila siku kuweza kujitibu na kujikinga dhidi ya tatizo hili


MATIBABU YA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo la kutoa harufu mbaya ukeni na umejaribu njia hizo hapo juu bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

1 comment:

  1. Habari samahani mimi nina mpenzi wangu Ana hilo tatizo la kutoka harufu ukeni naomba ushauri nini cha kufanya au nitumie njia gani ili aweze kuondokwa na tatizo hili?

    ReplyDelete

Copyright © 2017 Green health consultation centre