FAHAMU MATIBABU YA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/CHUNJUA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO/WARTS SEHEMU ZA SIRI NA MAENEO MBALIMBALI KATIKA MWILI(WARTS & GENITALS WARTS)

FAHAMU MATIBABU NA AINA MBALIMBALI ZA CHUNJUA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO/VINYAMA VINAVYOOTA SEHEMU MBALIMBALI KATIKA MWILI (WARTS&GENITALS WARTS)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul
Mpendwa msomaji nina imani kuwa unaendelea vyema wewe na familia yako nami niko salama Sifa na utukufu tumrudishie Mwenyezimungu ambaye katujaalia neema ya uzima na tuwaombee wagonjwa waliopo majumbani ama hospitalini Mwenyezimungu awape nafuu ya maradhi yao na wenye shida pia watatuliwe shida zao Ameen!

Nimepokea emals nyingi week hii za watu wenye matatizo ya kuota vinyama juu ya ngozi(chunjua/vigwaru/masundosundo/warts)
kwa muda mrefu tatizo hili limekua linasumbua vichwa vya madaktar na wagonjwa wengi kiujumla.
Nimeamua kulielezea tatizo hili kwa kina ili kila mmoja afahamu ugonjwa huu na namna ya kuepukana nao pia jinsi ya kupata matibabu


Chunjua/masundosundo/vigwaru ni ugonjwa wa kutokewa na vioteo/viuvimbe au vinyama vidogovidogo juu ya ngozi unaosababishwa na kirusi aitwaye human papillomavirus (HPV). Mathalani Kuna aina tofauti zaidi ya 150 za human papiloma viruses.
Aina nyingine ya kirusi huyu hushambulia sehemu za siri na sehemu za mdomo na kujenga uvimbe mkubwa , ambao mara nyingine huendelea na kuwa saratani.
Pia zipo aina nyingine za virus wa HPV hushambulia ngozi na kujenga uvimbe ambao hauhusishwi na saratani. Pamoja na kuwa chunjua huambukiza, si ajabu kuona kuwa mtu mmoja tu ndani ya familia ndiye aliyeathirika. Vile vile chunjua hushambulia sehemu moja tu ya mwili (kama vile mikono au miguu), ingawa huweza kuenea hadi sehemu nyingine za mwili. Aina ya chunjua inayotokea huendana na aina ya kirusi wa chunjua na kiungo kilichoshambuliwa. Kwa mfano, kirusi wa aina moja huweza kusababisha chunjua za aina ya ‘common warts’ kwenye mikono na vile vile akasababisha chunjua za aina ya plantar.


Virusi vya HPV(Human papiloma viruses)vimethibitika kuwa ni chanzo katika kukua kwa kansa za viungo vya uzazi kama kansa ya shingo ya kizazi na kansa za mkundu.
 HPV vile vile wamehusishwa na ukuaji wa kansa za kichwa na shingo zinazoanzia kwenye findo (tonsils).

Wapo pia virusi wa HPV wasio na madhara makubwa sana wenyewe huleta uvimbe sehemu za siri, genital warts. Wengine hushambulia ngozi na kuleta warts sehem mbalimbali za mwili.
Halikadhalikla kuna virus vya HPV wanaosababisha uvimbe kwenye viungo vya sauti (vocal cords).
Mathalani aina za chunjua zinazoonekana kwa wingi ni common warts, flat warts, plantar warts, periungual warts, filiform warts na genital warts.
Hapa chini tutaona aina hizo za warts na matibabu Yake.

CHUNJUA AINA YA FLAT WARTS

Flat warts ni viuvimbe/vigwaru/chunjua/warts/vinyama vinavyotokea juu ya ngozi iliyo laini, bapa, wenye rangi ya ngozi au kahawia ya
njano wenye ukubwa wa ncha ya sindano.
Mara nyingi hupatikana usoni, maeneo ya nyuma ya mikono au miguu na huwa kwenye kikundi cha chunjua 20 hadi 200 kwa pamoja. Chunjua hizi huwapata zaidi watoto wadogo na vijana. Flat warts husababishwa na kirusi ambaye anaambukiza, lakini asiye na madhara wala maumivu.

Pia Flat warts huingia kupitia majeraha ya kwenye ngozi. Wanaume hupata chunjua hizi baada ya kunyoa ndevu, wakati wanawake huwa na chunjua hizi miguuni.

Kama ilivyo kwa chunjua za aina nyingine, husababishwa na human papillomavirus (HPV). Flat warts husababishwa na HPV wa koo za 3, 10, 28 na 49. HPV hawa hawana madhara, tofauti na wengine, kama genital warts, wanaosababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake. Flat warts wanaweza kuenezwa kwa kugusana na ngozi yenye chunjua au kutumia taulo au chombo ambacho kimetumika na mwathirika. Unaweza pia kueneza chunjua hizi kutoka sehemu moja ya mwili wako hadi nyingine.

Flat warts kwa kawaida huondoka zenyewe bila kuhitaji tiba. Unaweza kupata tiba ili kupona haraka zaidi. Daktari anaweza kukuandikia cream, lakini cream hizi huchubua ngozi ili kuondoa chunjua. Cream hizi ni kama:

. retinoic acid 0.05 percent cream
. Imiquimod 5 percent cream (Aldara, Zyclara)
. Topical 5-fluorouracil (Carac, Efudex, Fluoroplex, Tolak), 1 percent or 5 percent cream

Daktari anaweza pia kukuandikia 5 percent benzoyl-peroxide (Del Aqua, NeoBenz Micro, au Clearskin, EFFACLAR). 

CHUNJUA AINA YA PLANTAR WARTS

Plantar warts ni vijiuvimbe/vigwaru/warts/vijinyama vidogo vinavyotokea kwenye kisigino au sehemu ambazo zinabeba uzito za kwenye mguu. Mgandamizo kwenye maeneo hayo kunaweza kusababisha plantar warts kuota kuelekea ndani, chini ya tabaka nene la ngozi (callus).
Plantar warts husababishwa na HPV. Kirusi huyu huingia mwilini kupitia sehemu ndogo ulizojikata, au sehemu nyingine dhaifu za maeneo ya chini ya mguu.

Plantar warts nyingine hazihatarishi afya na hujiondokea zenyewe baada ya muda bila tiba yoyote.

Plantar warts zinasababishwa na HPV anapoingia kwenye tabaka la juu la ngozi ya kwenye unyayo kupitia vijijeraha vidogo au maeneo mengine yaliyo dhaifu yaliyo maeneo ya chini ya mguu.

HPV hupatikana kwa wingi, na kuna aina tofauti zaidi ya 100 ya kirusi huyu. Lakini ni aina chache tu ambazo zinaweza kuleta chunjua kwenye mguu. Aina nyingine zinaweza kuleta chunjua kwenye maeneo mengine ya ngozi au kwenye utando telezi.

Kila mtu ana kinga zake za mwili zenye uwezo tofauti wa kupambana na HPV. Si kila mtu atakayegusana na kirusi huyu atapata chunjua. Hata watu wa familia moja watahimili kirusi huyu kwa viwango tofauti.

HPV wanaoeneza plantar warts hawaambukizi kirahisi. Kwa hiyo chunjua hizi haziambukizi kwa kugusana. Lakini wanapenda kuishi kwenye mazingira ya vuguvugu, yenye unyevu. Kwa hiyo unawea kumpata kirusi huyu kwa kutembea peku kwenye mabwawa ya kuogelea. Kirusi akipenya sehemu moja, anaweza kuenea hadi maeneo mengine na kusababisha chunjua.

CHUNJUA AINA YA PERIUNGUAL WARTS


Chunjua za aina hii ya periungual warts hutokea kwa kujifunzajenga kuzunguka kucha za vidoleni au kwenye dole gumba. Zikikua huweza kukukosesha raha au kuleta maumivu na huweza kuathiri ukuaji wa kucha. Watoto na vijana wa umri wa balehe wana nafasi kubwa zaidi ya kupata periungual warts na hasa kama wana tabia ya kung’ata kucha zao.

Periungual warts huwa ndogo sana mwanzoni, ukubwa wa ncha ya sindano, zikiwa laini na za kung’aa. Katika wiki au miezi michache, huweza kufikia ukubwa wa njegere zikiwa na umbo la kaliflawa.

Periungual warts huweza kuwa na rangi ya kahawia, kujivu, au nyeusi. Baadaye hujijenga na kuwa nyingi kwa pamoja. Zikiwa kubwa huweza kuleta maumivu.

Periungual warts huletwa na baadhi ya koo za human papillomavirus (HPV). Kirusi  huyu huambukiza kupitia kugusana na mtu mwenye ugonjwa huu au kupitia mataulo. Kirusi huyu hupitia sehem zenye majeraha, na hii ndiyo sababu watu wanaopenda kutafuna kucha zao huwa kwenye hatari zaidi. Watu wenye upungufu wa kinga za mwili au wenye magonjwa ya ngozi nao huathirika kirahisi zaidi.

CHUNJUA AINA YA COMMON WARTS

Common warts ni chunjua ndogo zinazojengwa na uvimbe wa chambechembe ndogo za ngozi ambazo mara nyingi hutokea kwenye vidole au mikono. Chunjua hizi ambazo hukwaruza ziguswapo, mara nyingine huja kama vijidoa vyeusi, ambavyo ni mishipa midogo ya damu yenye damu iliyovia.

Common warts husababishwa na kirusi anayeenezwa kwa kugusana. Inaweza ikachukua miezi 2 hadi 6 chunjua kuanza kujijenga baada ya kugusa kitu chenye kirusi huyu. Chunjua hizi hazina madhara makubwa na baadaye hupotea zenyewe. Watu walio wengi huamua kuziondoa kwa sababu huona kama ni bughudha kwao.

Common warts kwa kawaida hutokea kwenye vidole au mikono na huwa:

Kama uvimbe mdogo uliojengwa kwa chembechembe ndogo za nyama
Zenye rangi ya nyama, nyeupe, pinki au hudhurungi
Zenye mikwaruzo zikiguswa
Zenye alama nyeusi zilizojitawanya, ambazo ni mishipa midogo ya damu.

Pia Common warts husababishwa na human papillomavirus (HPV). Kirusi huyu anapatikana kwa wingi sana na kuna aina tofauti zaidi ya 150 za kirusi huyu, lakini ni aina chache sana zinazoweza kuleta chunjua kwenye mikono. Aina nyingine za HPV hupatikana kwa kushiriki ngono. Aina nyingi zaidi hupatikana kwa kugusana ngozi au kuchangia vitu , kama taulo au vifaa vya kujioshea. Kirusi huingia mwilini kupitia michubuko kwenye ngozi. Kukata kucha kwa meno kwa weza kusababisha kusambaa kwa kirusi huyu kwenye ncha za vidole au kuzunguka kucha.
zaidi.

CHUNJUA AINA YA FILIFORM WARTS


Chunjua za aina hii zina mwonekano wa tofauti kabisa na nyingine. Filiform warts ni  michomozo mirefu myembamba yenye urefu wa kati ya milimeta 1 hadi 2 juu ya ngozi. Zinaweza kuwa na rangi ya njano, kahawia au rangi ya ngozi, na haijijengi kwa vikundi. Kwa vile hupenda kutokea kwenye kope au mdomoni, chunjui hizi huitwa pia facial warts. Chunjua hizi huweza kutokea pia kwenye shingo, kwenye vidole na miguuni. Zinaweza kusambaa kwa haraka sana kwenye sehemu nyingine za mwili.

Filiform warts husababishwa na human papillomavirus (HPV), ambaye huambukiza. Anaweza kuambukizwa kwa kugusana ngozi, na hasa kama kuna jeraha kwenye ngozi. Pamoja na kuwa haziwezi kusababisha saratani, huwa ni bughudha.


Dalili Za chunjua za filiform warts

Kwa kawaida chujua za filiform hazina maumivu na hazina dalili zo zote. Chunjua hizi hutambulika kwa macho. Dalili zinaweza kuonekana kama chunjua zitaota sehemu za ngozi zenye mikunjo. Na dalili zaweza kuwa:

. Kuwasha
. Kutoka damu
. Maumivu

Chanzo Cha Chunjua Za Filiform

Filiform warts husababishwa na HPV. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 za HPV. HPV wa ukoo 1,2,4,27 na 27 ndiyo wanaojulikana kusababisha chunjua za filiform.

Tiba Ya Filiform Warts

Tiba nyingi zinalenga kuondoa chunjua, lakini hazimwondoi kirusi. Hakuna dawa ya HPV kwa sasa hivi, ispokuwa sindano ambazo zinalenga baadhi ya koo za HPV. Hadi sasa hakuna sindano kwa ajili ya filiform warts.

Kwa walio wengi, filiform warts huondoka zenyewe baada ya muda kwa msaada wa kinga zao za mwili.

CHUNJUA AINA YA GENITALS WARTS

Genital warts ni viuvimbe/vigwaru/chunjua/ vinyama vidogovidogo vinavyotokea sehemu za siri.
Chunjua hizi huenezwa sana kwa njia ya ngono.
Karibu watu wote wanaofanya mapenzi wamepata kuambukizwa na angalau aina moja ya human papillomavirus (HPV), kirusi anayeeneza genital warts, katika maisha yao. Wanawake kwa namna fulani wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata chunjua za sehemu za siri.
Genital warts hushambulia maeneo yenye unyevunyevu sehemu za siri. Chunjua hizi huweza kuonekana kama vijiumbile vidogo vya nyama au vikawa na umbo kama la koliflawa. Mara nyingi genital warts ni ndogo mno kuonekana kwa macho na wakati wengine hutokewa kubwa zenye kuonekana kwa urahisi

Kama ilivyo kwa chunjua za aina nyingine, genital warts husababishwa na human papilloma virus (HPV). Koo nyingine za HPV husababisha genital warts, wakati nyingine huleta saratani. Sindano zinaweza kusaidia kujikinga na baadhi ya koo za genital HPV.

Chanzo Cha Genital Warts

Genital warts au chunjua za sehemu za siri husababishwa na human papilloma virus. Kuna koo tofauti zaidi ya 40 zinazoshambulia sehemu za siri. Genital warts huenezwa kwa kufanya tendo la ndoa. Wakati mara nyingine kinga zako za mwili huua virusi hawa na hupati athari zozote.


Madhara Yatokanayo Na Genital Warts

. Saratani
Saratani ya shingo ya kizazi inahusishwa sana na maambukizi ya genital HPV. Aina nyingine za genital warts zinahusishwa na kansa ya sehemu za nje ya uke, saratani ya kwenye mkundu, saratani ya dhakari, na saratani za mdomo na koo. Si kweli kwamba maambukizi yote ya HPV yanaleta saratani.

. Matatizo wakati wa ujauzito
Genital warts huweza kuleta matatizo wakati wa ujauzito. Chunjua hizi huweza kukua na kuwa kubwa kiasi cha kuziba mkojo usitoke vizuri. Chunjua hizi za kwenye kuta za uke huweza kupunguza mnyumbuko wa tishu za uke wakati wa kuzaa. Chunjua kubwa za nje ya uke au ndani ya uke zinaweza kutoa damu zikipanuliwa wakati wa kuzaa.

Yaweza tokea mara chache sana kwamba kichanga cha mama mwenye chunjua za ukeni kikawa na chunjua kwenye koo lake ambapo upasuaji utahitajika kuhakikisha njia zake za hewa hazijazibwa.


Matibabu
Hospitali kuna tiba nyingi zinazotumika, lakini hakuna yenye uhakika wa asilimia 100 katika kuondoa chunjua za sehemu za siri na kuzizuia zisirudie tana. Genital warts huweza kuondoka zenyewe kutoka asilima 10 hadi 20 ya watu walioathirika katika kipindi cha miezi 3 hadi 4.

. Cryotherapy: Njia hii hugandisha chunjua kwa kutumia naitrojeni ya maji (liquid nitrogen). Ni njia bora sana kwa sababu imetoa matokea mengi mazuri ikiwa na side effects chache sana.

. Laser treatment: Njia hii hutumika kwa chunjua za sehemu za siri zilizoenea au zinazojirudirudia. Mionzi ya laser huharibu kabisa uvimbe  uliotokana na HPV. Dosari ni bei yake kubwa, muda mrefu wa tiba, na kuacha makovu.

. Elecrodesiccation: Njia hii hutumia peni ya umeme kuua chunjua.

Dawa zinazotumika kutibu genitals warts

Kuna dawa kadhaa zinazotumika kutibu chunjua za sehemu za siri na unaweza kuzitumia kama mbadala wa tiba nyingine.

. Podophyllum resin ni dawa inayotolewa na mtaalamu wa tiba
. Podofilox (Condylox) ni dawa unayoweza kuitumia nyumbani na ina uwezo mkubwa wa kutibu kuliko podophyllum resin. Dawa hii pia hutumika kwa kinga.
. Trichloroacetic acid au bichloroacetic acid haina uhakika sana na chunjua huweza kurudi, inaweza kusababisha maumivu na kujisikia kama unaungua.
. 5-Fluorouracil (Efudex) hutumika kama cream, huchukua muda mrefu kutibu, na ina madhara mengine mengi ya kiafya.
. Interferon alpha -n3 (Alferon N) ni sindano inayotumika kwa chunjua ambazo hazisikii dawa nyingine, lakini ina madhara mengine mengi.
. Imiquimod (Aldara) hutumika kama cream na maumivu wakati ukipaka hutokea.

MATIBABU YA UGONJWA WA CHUNJUA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO/VINYAMA VINAVYOOTA SEHEMU MBALIMBALI KATIKA MWILI(WARTS & GENITALS WARTS)CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kutokewa na chunjua/vinyama vidogovidogo vinavyotokea katika ngozi (warts/genitals warts) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam 
Tutakufanyia uchunguzi wa kujua ni aina gani ya chunjua ulizonazo pia tutakupatia dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya pasipo kukuunguza
Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la vinyama sehemu mbalimbali katika mwili,tatizo la hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre