FAHAMU SULUHISHO LA UGONJWA/TATIZO LA TINDIKALI TUMBO KURUDI KWENYE KOO LA CHAKULA (GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE) NA TATIZO LA KUWA NA KIUNGULIA (HEARTBURN) MUDA MREFU
TATIZO LA TINDIKALI TUMBO KURUDI KWENYE KOO LA CHAKULA(GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE) NA KIUNGULIA (HEARTBURN)
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul
Ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wa makala hii
Kwa upande wangu namshukuru Allah kwa kunijaalia uzima na nafasi ya kuwajibika katika majukumu yangu
Kutokana na harakati na shughuli kuwa nyingi leo nimepata nafasi ya kuandaa somo hili ambalo watu wengi wamenitumia email na meseji kwa ajili ya kupata suluhisho la kudumu
Ila kabla ya kutoa suluhisho nimeona kuna haja ya kupata elimu ya matatizo haya na jinsi ya kujiepusha na kupata Matibabu.
Je, TATIZO LA TINDIKALI TUMBO KURUDI KWENYE KOO(GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE) ni tatizo gani?
Hili ni tatizo linalotokea katika mfumo wa mmeng'enyo ambapo hutokea hitilafu ya chakula au maji kurudi katika koo la chakula(umio)mara baada ya kuwa chakula Hiko kimeshamezwa.
Au
Ni kitendo cha kupanda kwa acids (tindikali) ya tumbo hadi kwenye umio la chakula kwa muda mrefu na matokeo yake husababisha kiungulia(HEARTBURN)
Ili kuelewa vizuri tatizo hili linavyotokea tunatakiwa kujua vizuri jinsi chakula kinavyofika tumboni.
Kawaida Mara baada ya mtu kutafuna chakula au kunywa maji,chakula husafirishwa kupitia mrija wa chakula (Esophagus) hadi tumboni lakini juu kidogo kati ya tumbo na mrija huu wa chakula kuna kizuizi kilicho na sura ya bangili ( lower esophageal spincher )
kibangili hiki hufanya kazi ya kuzuia chakula kisurudi mdomoni au kwenye koo baada ya kuwa kimeshamezwa pia kibangiri hiki ndicho kinacho mfanya mtu aweze kula chakula huku amening'iniza kichwa chini miguu juu na chakula kisirudi tumboni.
baada ya chakula kuingia tumboni huchanganyikana na vimeng'enya pamoja na tindikali ambayo hufanya kazi ya kuua vimelea vyote vilivyoingia tumboni pamoja na chakula
mchanganyiko huu husababisha chakula kupata chachu(acids) ambayo matokeo yake huwa ni rahisi sana kuweza kurudi katika koo la chakula endapo kizuizi cha juu ya tumbo kitakua kimepata hitilafu au maambukizi.
Je, Kiungulia (HEARTBURN)NI NINI?
Ni hali ya kukera inayoweza kumtokea mtu yoyote na husababisha maumivu makali kwenye kifua na upande wa juu wa tumbo.Hali hii inaendana kwa ukaribu wa kupanda kwa tindikali(acid reflux).
Lakini pia Kuna utofauti kati ya acid reflux na heartburn.
Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa acid reflux ni kitendo cha kupanda kwa tindikali kutoka tumboni kurudi juu kwenye umio la chakula na kusababisha maumivu ya kifua ambayo tunaita ni kiungulia (Heartburn)
Kwahiyo acid reflux ndio inayoweza kusababisha Kiungulia (HEARTBURN)
Hali ya kiungulia ni kitendo cha kawaiada kutokea kwa watu wengi na inatokea kwa kila mtu, lakini kama tu haiambatani na maumivu makali ya kifua, kama maumivu yakizidi kuwa makali na yanatokea mara kwa mara hapo ndipo tatizo huanza. Kama tatizo likiendelea zaidi basi hufikia hatua ya tatu na kuitwa gastroesophageal reflux disease(GERD), kwa hiyo kadiri kiungulia kinachukua muda mrefu mpaka kuathiri tishu za umio GERD ni hatari zaidi kwasababu inaweza kupelekea uwezekano wa kupata Saratani ya Koo
CHANZO CHA MATATIZO
1. Kudhohofika kwa utendaji kazi wa kizuizi cha juu ya tumbo ( Lower esophageal sphincter)
kudhohofika kwa kizuizi hiki husababishwa na utumiaji wa madawa kama nitrates,bisphosphonates,estrogen,oral contraceptives,progesterone,alpha adrenergic agents,theophyline,calcium channel blockers,benzodiazepines,anticholinergics, na tricyclic antidepressants nk baadhi ya dawa zimeonekana kuharibu sana utendaji kazi wa kizuizi hiki.
2.Mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula
Mfumo wa mmeng'enyo huwa dhaifu kutokana na lishe kuwa mbovu
watu wanaokula zaidi vyakula vilivyosindikwa, sukari, chocolate, vyakula vyenye caffeine kama kahawa wapo kweye hatari zaidi ya kupata matatizo haya
3.Tindikali ( Hydrochloric acid) kuzidi tumboni.
4.Upungufu wa madini kama Magnesium na Potassium
5.Uzito mkubwa na kitambi na msongo wa mawazo kupita kiasi ni chanzo cha kupata matatizo haya.
6.Wamama wajawazito na wazee wenye umri mkubwa wako kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo haya
7.Wenye historia ya kuwa na ugonjwa wa hernia(ngiri) pia wapo katika hatari zaidi ya kupata matatizo haya
DALILI ZA KUKUJULISHA UNA TATIZO LA GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE
Kiungulia hiki huanza baada ya lisaa limoja na kuisha baada ya masaa mawili baada ya kula.
Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula
Dalili zingine ni kama;
Tumbo kuunguruma na
Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.
Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali
Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula
Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka.
Mdomo kuwa mchachu muda mwingi
Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu
Mdomo kukauka
Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
Tumbo kujaa na kujamba sana baada ya kula
UCHUNGUZI NA VIPIMO
Uchunguzi wa matatizo haya hufanyika kwa njia kipimo cha x-ray,ambapo mgonjwa hupewa kimiminika maalumu ambacho hukimeza ili kuonesha utendaji kazi wa mfumo wa chakula pindi atakapofanyiwa x-raylakini iwapo tatizo linapokua kubwa zaidi kipimo aina ya Endoscopy hutumika,hiki ni kimrija chenye kamera ni kadogo sana huingizwa kupitia koo la chakula hadi tumboni kisha kuonesha kwenye screen jinsi mfumo ulivyo.
MATIBABU
Mara nyingi baada ya vipimo na uchunguzi kufanyikaUshauri wa lishe na dawa za antiacids hutolewa juu ya kupambana na magonjwa haya pia ukubwa wa tatizo hupelekea watu kufanyiwa upasuaji baada ya kutumia dawa za kupunguza tindikali ( antacid) na zingine kama cholinergic agenys,Hestimamine H2 Antagonists,Prokinetic Agents na proton Pump Inhibitors.
Lakini pia wapo baadhi ya wagonjwa kadiri wanavyoendelea kutumia dawa hizi huongeza magonjwa mengine ya mfumo wa chakula na kuharibu bacteria wazuri walioko tumboni, matumizi ya dawa za antiacid zinaweza kusababisha kukosa choo ama kupata choo kwa shida, kuharisha, matatizo kwenye figo na kushuka kwa kinga ya mwili
MAMBO YA kUFANYA KUJITIBU KIUNGULIA CHA MARA KWA MARA UKIWA NYUMBANI ILI KUJIEPUSHA NA TATIZO LA GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASES
Badilisha mfumo wako wa chakula jitahidi kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
Punguza au jiepushe kuwa na uzito mkubwa
Epuka aina ya vyakula vyote unavyohisi vinaweza kuchangia kukupa Kiungulia
Sitisha unywaji wa vinywaji vyenye caffein vyote.
Kula kwa mpangilio ili chakula kiweze kumeng'enywa taratibu tumboni,sio kila wakati unakula tena kwa kuchanganya changanya.
Acha sigara na pombe.
Punguza msongo wa mawazo
Lala masaa matatu mpaka manne baada ya kula.
Hakikisha unalala kichwa chako kiwe juu,yaani weka mto kichwa pindi unapolala.
Pia wakati unayafanya yote hayo hapo juu tumia baadhi ya vyakula kujitibu kiungulia
TANGAWIZI(GINGER)
Tangawizi ina vitamin A, C, E, B complex, chuma,zinki, magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta carotene hivyo hutumika kutibu tatizo la gesi na acids kuwa nyingi
Chemsha kikombe kimoja cha maji ya tangawizi kunywa kila siku asubuh kabla ya kula kitu na usiku lisaa limoja kabla ya kwenda kulala kwa muda wa siku 14 au zaidi
JUISI YA MSHUBIRI (ALOEVERA JUICE)
Kama utainywa, hutibu vidonda vya tumbo na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng’enyo wa chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya kawaida nusu kikombe tena kupata ujazo wa robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo ya Kiungulia,tumbo kuuma, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.
KITUNGUU THAUMU NA ASALI (GARLIC AND HONEY)
Kitunguu swaumu ni miongoni mwa tiba za asili kwa miaka mingi hasa katika maswala ya kuua fungals hutoa majibu haraka sana kwa upande wa Kiungulia
Chukua punje 3 hadi 4, menya na ukate vipande vidogo vidogo lakini siyo vidogo sana na uchemshe kwenye moto na maji kikombe kimoja (robo lita), ongeza kijiko kikubwa kimoja chaasali mbichi ndani yake na uache kwenye moto kama dakika 5. Ipua na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 hadi utakapopona Kiungulia lakini pia utakua umejitibu baadhi ya maradhi mengine mwilini mwako
SIKI YA TUFAHA (APPLE CIDER VINEGAR)
Imeonekana kuwa ni msaada miongoni mwa maradhi mengi ya mfumo wa mmeng'enyo hivyo inashauriwa kunywa walau vijiko viwili kwa siku
MATIBABU YA TATIZO LA GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASES NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER
Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASES na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tutakupatia dawa za kuondoa tatizo la GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASES na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako
NOTED;
Kutopata matibabu mapema ni hatari kwa afya yako kwa vile huweza kusababisha magonjwa makubwa zaidi kama vile;Uvimbe joto sehemu za koo la chakula ambapo uvimbe huu huharibu koo la chakula kwa vile huweza kusababisha vidonda na koo kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
Kutengenezwa kwa kovu katika koo la chakula ambako kunapelekea koo la chakula kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
Kubadilika kwa seli za koo la chakula kunakopelekea koo la chakula kupoteza asili yake ambapo tatizo hili kitaalamu huitwa Barrett's esophagus na mwishowe ukapata saratani ya Koo na magonjwa ya Moyo
Tunawaombea wahanga wa ugonjwa huu wapate Matibabu mapema na waepukane na maradhi makubwa zaidi
AMEEN.
Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA
GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
0 comments: