FAHAMU MATIBABU YA UGONJWA WA MKANDA WA JESHI/MOTO WA MUNGU (SHINGLES/HERPES ZOSTER) NA MADHARA YA UGONJWA HUU

 

Ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya ugonjwa wa mkanda wa jeshi/moto wa mungu (shingles/herpes zoster).

Kwa miaka mingi sasa  ugonjwa huu umekua mkubwa na endelevu katika jamii kwa sasa ambapo pia imekua ikichukuliwa kwa dhana au fikra mbovu kua ugonjwa huu ni kipimo cha dalili/ishara ya kuwepo kwa virusi vya ukimwi katika mwili wa mgonjwa huyo kitu ambacho sio cha kweli kua na ugonjwa wa mkanda wa jeshi/moto wa mungu(shingles/herpes zoster) haimaanishi kua una ugonjwa wa ukimwi.

Mkanda wa jeshi/moto wa mungu kwa lugha ya kitabibu  shingles au zoster ni ugonjwa unaosababishwa na virus wabaya aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa maarufu  unaotokea hasa kwa watoto unaoitwa tetekuwanga(chickenpox).

ugonjwa huu umekua ukiwapata watu ambao waliwahi kuugua tetekuwanga huko kipindi cha nyuma,kwani mtu anapougua tete kuwanga na baadae akapona virusi hawa hujificha kwenye mishipa ya damu kwa miaka mingi hadi pale kinga ya mwili inapokua ndogo sana mwilini ndipo virusi hawa hujitokeza kwa mara nyingine na kusababisha ugonjwa mwingine mpya ambao ndio huu ugonjwa wa Mkanda wa jeshi/moto wa mungu (shingles).

Ugonjwa huu hatari ambao huathiri ngozi  huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali kulinganisha na ugonjwa wa tete kuwanga ambapo huathiri sana neva za kwenye ngozi.

Kwa kawaida shambulio la mkanda wa jeshi hutokea mara moja maishani ingawa laweza kujirudia kulingana na kinga ya mwili kua katika kiwango cha chini.

Kadhalika ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi unaweza kumpata mtu wa umri wowote ule ingawa watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi:

• Wenye umri wa zaidi ya miaka 60

• Mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya umri wa mwaka mmoja

• Watu ambao kinga yao ya mwili imepungua kwa sababu mbalimbali kama vile matumizi ya aina fulan za dawa, magonjwa kama vile maambukizi ya VVU (HIV/AIDS), saratani na utapiamlo(unyogofu)

Pia ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine! Lakini iwapo itatokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga maishani mwake na ambaye pia hajawahi kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo akakutana na mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto au mtu huyo atapatwa na ugonjwa wa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.


CHANZO/VISABABISHI

Mpendwa msomaji kama nilivyokwisha tangulia kueleza hapo juu kuwa ugonjwa huu husababishwa na virus aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga hivyo baada ya mtu kupatwa na tetekuwanga, virus hawa hubaki katika hali ya kupooza/kutokuwa na madhara (dormant) katika neva fulani za mwili lakini baada ya miaka kadhaa, iwapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu yoyote ile, virus hawa hupata tena nguvu/kuwa na madhara (active), kuibuka na kusababisha ugonjwa mpya ambao ndio huu ugonjwa wa mkanda wa jeshi.


DALILI


Dalili kuu kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yakiambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi. Maumivu pamoja na hisia za kuungua huwa makali sana na hutokea kabla ya vipele/michubuko kutokea kwenye ngozi. 

Kadhalika vipele au michubuko hiyo hutokea eneo fulani la mwili kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, mdomo au masikio.

Pia dalili nyingine ni pamoja na

• Maumivu ya tumbo 

• Homa 

• Maumivu ya mwili mzima 

• Vidonda sehemu za siri 

• Maumivu ya kichwa 

• Maumivu ya viungo 

• Kuvimba kwa mitoki/ matezi 

Pia iwapo  neva za maeneo ya uso zitaathiriwa, mgonjwa anaweza kupatwa na matatizo ya kutoona, kutohisi ladha na au kutosikia.


Vipimo na UCHUNGUZI


Hakuna vipimo maalum kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea pekee kadhalika daktari mzoefu anaweza kuutambua ugonjwa huu bila vipimo kabisa kwa kuchukua historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa. 

Pia huweza kutumika vipimo vya damu yaani FBP Kwa ajili ya kuonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu na antibodies dhidi ya virus wa tetekuwanga.


Matibabu

Mpendwa msomaji kwa bahati mbaya ugonjwa huu hauna dawa maalumu hospitalini hivyo matibabu ya mkanda wa jeshi  hujumuisha matumizi ya dawa tofauti kama vile Acyclovir, Famciclovir na Valacyclovir kwa ajili ya kuua virus wanaosababisha ugonjwa huu na kusaidia kupunguza maumivu, kuzuia madhara zaidi ya ugonjwa huu.

Dawa hizi hutolewa angalau saa 72 baada ya mgonjwa kuanza kuhisi maumivu na hali ya kuungua. Ni vema dawa zianze kutumika kabla ya vipele/michubuko kujitokeza.

Pia jamii ya dawa za corticosteroids kama vile prednisolone husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwa badhi ya wagonjwa. 

Kadhalika dawa nyingine zinazofaa kutumika ni pamoja na jamii ya antihistamines kwa ajili ya kupunguza muwasho hasa calamine lotion ambayo mara nyingi hutumika  kwa ajili ya kupunguza muwasho,pia mgongwa hushauriwa kupata mapumziko ya kutosha kwa kutulia nyumbani kwa muda kadhaa hata hivyo pia mkanda wa jeshi kwa kawaida huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu kupona.


MADHARA

Mpendwa msomaji napenda kukufahamisha licha ya kuwepo madhara mengi ya ugonjwa huu ila ni nadra sana kwa ugonjwa huu kujirudia tena iwapo ukatumia dawa ukapona hivyo ondoa hofu.

Lakini Iwapo neva zinazothibiti mwendo katika mwili zitakuwa zimeathirika, mgonjwa anaweza kupatwa na kupooza kwa muda au kwa kudumu kwa sehemu ya mwili iliyoathiriwa. Wakati mwingine, maumivu yanayosababishwa na mkanda wa jeshi yanaweza kudumu kwa miezi mpaka mwaka hata baada ya mgonjwa kupona kabisa. Maumivu haya yanayojulikana kama postherpetic neuralgia kwa kawaida huwakumba wagonjwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na husababishwa na uharibifu katika neva za mwili,

Kadhalika madhara mengine ya mkanda wa jeshi ni pamoja na kupatwa na shambulio jingine la ugonjwa huu, maambukizi ya bakteria, upofu iwapo eneo la jicho litahusika, ukiziwi, maambukizi katika utando wa ubongo (encephalitis), uwepo wa vimelea kwenye damu (sepsis) au ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt Syndrome iwapo utahusisha neva za uso, kadhalika kupatwa na homa ya uti wa mgongo na kubakia na makovu kama vile umeungua na moto.


NAMNA UNAVYOWEZA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA MAUMIVU UKIWA NYUMBANI

Mpendwa msomaji wetu kuna njia tatu ninazoziamini anazoweza kuzitumia mgonjwa kujitibia kwa kupunguza maumivu na kupona haraka tatizo hili akiwa nyumbani lakini pia ni muhimu na ni lazima kufika hospital na kutumia dawa ili kupata matokeo ya kupona kwa haraka.


PATA MLO WENYE VIRUTUBISHO VYOTE



Mpendwa msomaji napenda kukusisitiza kuwa lishe kamili ni muhimu kwa kutibu,kuzuia na kupigana na magonjwa ndani ya miili yetu.

Miongozo ya Lishe kwa Wamarekani inapendekeza kula lishe kamili inayojumuisha mboga nyingi, matunda, na nafaka nzima pamoja na kunde, karanga,nyama na samaki.

Kadhalika watu wenye kusumbuliwa na ugonjwa  wa mkanda wa jeshi(shingles/herpes zoster) wanashauriwa sana kula machungwa,nyama nyekundu, na mboga za kijani kibichi na matunda mekundu ambayo yamesheheni viambata vya  lycopene,carotenoids, lutein, zeaxanthin, na proitamin A.

Kiambata cha Carotenoids ni muhimu sana kwenye miili yetu  kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya kinga zetu.

kadhalika vyakula vifuatavyo vimeonekana kuwa na kiambata cha Carotenoids kwa wingi zaidi ni

vyakula vya rangi ya machungwa(orange foods): Vyakula hivyo ni karoti, maboga, na apricot.

vyakula vya rangi nyekundu(red foods): Vyakula hivyo ni tikiti, pilipili nyekundu, zabibu, na cherry

vyakula vya  rangi ya kijani(green foods): Vyakula hivyo ni parsley, mchicha, limao, lettuce, na broccoli.

Wakati unakula mlo kamili unashauriwa kuacha kutumia sukari tumia chumvi pekee katika milo yako pia epuka kahawa na vilevi hii itakusaidia kuboresha kinga yako ya mwili na kupunguza maumivu na kupona kwa haraka sana.


KUOGA MAJI BARIDI/VUGUVUGU MARA KWA MARA

Inashauriwa kuoga maji ya baridi au vuguvugu  walau mara 3_4 kwa siku hii itasaidia kupunguza maumivu na kuondoa umoto na homa zinazotokana na ugonjwa huo na kuzuia maambukizi mapya.


ACHA KUVUTA SIGARA/ACHA KUNYWA POMBE

Uvutaji sigara hautoi faida za kiafya na huwa hatari kila wakati. Ni muhimu kuacha sigara kwani inaongeza hatari ya saratani ya ngozi na magonjwa mengine.

Kadhalika uvutaji wa sigara na kunywa pombe hupunguza kinga kwa ajili ya kupambana dhidi ya maambukizi haswa kwa watu wazee, na kinga ikiwa ndogo ni sababu ya kutokupona haraka.


MATIBABU YA UGONJWA WA MKANDA WA JESHI (SHINGLES/HERPES ZOSTER) CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama unasumbuliwa na ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi(shingles/herpes zoster) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha kabla hujapata madhara makubwa tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam tuweze kushughulikia tatizo lako.
Tutakufanyia uchunguzi  kwa kina pia tutakupatia ushauri na dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya kabisa.

Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tunatoa huduma ya matibabu ya ushauri na dawa za kuondoa magonjwa mbalimbali katika mwili kama vile matatizo ya figo,mapafu,Moyo,macho, hedhi mbovu,uzazi, magonjwa ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa  na kadhalika karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre