FAHAMU SABABU ZA UGONJWA/TATIZO LA MTU KUTAPIKA DAMU (HEMATEMESIS/VOMITING BLOOD)
Ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya siku nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya ugonjwa au tatizo la kutapika damu (hematemesis/vomiting blood).
Tatizo la kutapika damu limekua kubwa na endelevu katika jamii kwa sasa ambapo pia imekua ni dalili/ishara ya kuwepo moja ya matatizo kadhaa katika mwili wa binadamu.
Mpendwa msomaji tatizo hili kwa lugha zingine hujulikana pia kwa jina la HEMATEMESIS au VOMITING BLOOD ambapo huashiria kuwepo kwa ugonjwa ndani ya mwili wa binadamu ambapo pia ishara hii ya kutapika damu haitakiwi kuchukuliwa kimasihara au kupuuza kwani ni ishara kwamba kuna tatizo lenye kuhitajika msaada katika mfumo wa njia ya chakula au ndani katika viungo vingine hivyo uchunguzi wa kina na haraka unahitajika,
Kadhalika tatizo linaweza kuwa dogo, hivyo mgonjwa kutapika damu kidogo, au iliyo ganda kidogo pia tatizo linaweza kuwa kubwa kiasi cha mgonjwa akatapika damu nyingi, tena mbichi mfulululizo na kutishia uhai ikiwa hatapelekwa hospitali kwa matibabu rasmi pia kutapika damu huku kunaweza kuambatana na maumivu ya tumbo kwa juu au kutanguliwa na maumivu ya mara kwa mara ya tumbo upande wa juu, katika hali hii ya awali mgonjwa akifanyiwa uchunguzi ni rahisi kujua chanzo cha tatizo na kupatiwa matibabu haraka.
Lakini pia iwapo mgonjwa atatapika damu mbichi na wakati huo huo anatoka damu mbichi katika njia ya haja kubwa humaanisha hali ni hatarishi na inatakiwa apelekwe hospitali mara moja kwani damu inayovuja inachuruzika kupitia kwenye utumbo na kutokea katika njia ya haja kubwa.
Kadhalika pia rangi ya damu iliyotapikwa mara nyingine huweza kutuonyeshea chanzo cha tatizo,
Kwa mfano, mtu akitapika damu nyekundu sana mithili ya kutaka kua nyeusi kwa ujumla inaonyesha kuwa kutapika kwake damu kunatokana na kuwepo kwa hitilafu au tatizo katika sehemu za juu za tumbo (upper gastrointestinal source) kama vile tumboni.
Pia damu nyekundu mpauko mara nyingi huonyesha kuwepo kwa hitilafu au tatizo ndani ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa katika utumbo.
Mpendwa msomaji wakati mwingine rangi ya damu inayotapikwa huweza isionyeshe usahihi wa tatizo linalokusumbua hivyo daktari wako atalazimika Kukufanyia vipimo kwa ajili ya kuchunguza/kubaini tatizo.
CHANZO/VISABABISHI
Kuna vyanzo na sababu nyingi zinazofanya mtu kutapika damu.
Sababu hizi zinapatikana kutokana na ukubwa na udogo wa tatizo,sababu hizo za kutapika damu ni
°michubuko katika koo la chakula
°kutokwa na damu puani
°vidonda vya tumbo
°maambukizi katika umio la chakula
°saratani ya kongosho
°madhara ya matumizi ya dawa ya vidonge ya aspirin
°uvimbe katika tumbo na koo la chakula
°saratani ya utumbo
°michubuko katika umio na koo kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kifua au kutapika kwa muda mrefu
°saratani ya koo
°magonjwa sugu ya ini (cirrhosis)
DALILI
Dalili kuu ya tatizo hili ni KUTAPIKA DAMU japo pia kuna dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza pamoja na kutapika damu. Dalili hizi ni
°kuhisi kichefuchefu
°maumivu ya tumbo au kukosa utulivu tumboni
°kutapika yaliyomo katika tumbo hasa vipande vya damu.
VIPIMO NA UCHUNGUZI
Mpendwa msomaji daktari wako ili aweze kujua tatizo hili limesababishwa na nini!
Vipimo kadhaa huweza kufanyika kujua chanzo cha kutapika damu, vipimo vya awali ni muhimu pia kufanyika kama vile, kufahamu wingi wa damu (hemoglobin), kuangalia chembechembe zinazosaidia damu kuganda (platelets).
Kadhalika daktar wako atakuhoji juu ya dalili unazopata.
Atauliza tatizo la kutapika damu limekuanza lini hivyo utawajibika kufafanua kiasi cha damu uliyotapika, na ikiwa ilikuwa nyekundu mpauko au ilionekana kama rangi nyekundu sana mithili ya rangi nyeusi,pia utapaswa kumueleza iwapo kuna ugonjwa wowote wa hivi karibuni unaokusumbua, au ikiwa una magonjwa ya muda mrefu yanayokusumbua kama vile vidonda vya tumbo,nk.
Pia utapaswa kumwambia iwapo umemeza dawa aina ya aspirin na ni kiasi gani umemeza.
Kadhalika daktari wako anaweza pia kukuuliza iwapo wewe ni mnywaji wa pombe mara kwa mara.
Maswali yote haya husaidia kujua chanzo cha tatizo,pia vipimo vifuatavyo huweza kutumika ili kubaini chanzo cha tatizo kwa usahihi.
°Endoscopy kipimo ambacho kitatumika kuchunguza sehemu ya juu ndani ya tumbo (GI).
°ultrasound
°MRI
°CT Scan au x-ray vipimo hivi vinaweza kuonyesha chanzo cha kutapika damu. Picha za vipimo hivi zinaweza kuonyesha michubuko,vidonda na uvimbe ambao ndio sababu ya watu wengi kutapika damu.
MATIBABU
Mpendwa msomaji matibabu ya ugonjwa au tatizo la kutapika damu yanategemea zaidi chanzo chake, kila ugonjwa au tatizo linalosababisha kutapika damu lina matibabu yake tofauti hivyo ni muhimu kwa mgonjwa kwenda hospitali bila kuchelewa.
Iwapo mgonjwa ametapika damu nyingi kiasi cha kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu basi huhitajika kuwekwa katika chumba maalumu, kuongezewa damu na maji mwilini ili kuokoa maisha yake.
Pia kuna aina kadhaa za matibabu ambazo daktari wako anaweza kukupatia ili kutibu tatizo hili kama vile ÷
MATIBABU YA DAWA
Dawa zinaweza kutolewa ili kupunguza kiasi cha asidi ambayo huzalishwa tumboni mwako,dawa hizi husaidia iwapo tatizo lako la kutapika damu(hematemesis) husababishwa na kuwepo kwa vidonda tumboni.
OPARESHENI
Kufanyiwa oparesheni kunaweza kuhitajika ikiwa unaendelea kutapika damu nyingi na matibabu mengine uliyopatiwa hayajafanya kazi hivyo oparesheni huweza kutumika kurekebisha michubuko kwenye maeneo ya ndani ya tumbo lako au utumbo.kadhalika hufanyika oparesheni ili kuondoa viuvimbe tumboni.
Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kutapika damu (hematemesis/vomiting blood) kwa muda mrefu na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tunatoa huduma ya matibabu ya ushauri na dawa za kuondoa magonjwa mbalimbali katika mwili kama vile matatizo ya figo,mapafu,Moyo,macho, hedhi mbovu,uzazi, magonjwa ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa na kadhalika karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako
GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
0 comments: