FAHAMU MATIBABU NA CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI YA NYAYO NA KISIGINO (PLANTAR FASCIITIS/POLICEMAN HEELS)
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya wiki nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya matibabu ya tatizo au ugonjwa wa maumivu ya nyayo na kisigino ambapo tatizo hili hujulikana kwa lugha ya kitaalam kama PLANTAR FASCIITIS/POLICEMAN HEELS.
Tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino(Plantar fasciitis /policeman heels)ni moja ya sababu/chanzo kilichozoeleka juu ya tatizo la maumivu ya kisigino hivyo tatizo hili au ugonjwa huu tunaweza kusema kwa maana moja ni maambukizi yanayojumuisha kuvimba kwa bendi nene ya tishu ambayo hupatikana katika nyayo zetu miguuni ambayo inaunganisha mfupa wa kisigino na vidole vya miguu (Plantar fascias).
Kadhalika tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino(Plantar fasciitis) husababisha maumivu makali ambayo mara nyingi hutokea asubuhi pale muhusika anapoamka na anapoweka miguu yake chini na kuanza kupiga hatua zake za kwanza asubuhi maumivu huwa makali sana ambayo hupungua kadri anavyopiga hatua lakini pia hali ya maumivu huweza kurudi baada ya muda mrefu wa kusimama au unaposimama baada ya kukaa.
Tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino (Plantar fasciitis)huweza kuwapata watu wa rika zote ingawa hutokea zaidi kwa watu wanaofanya mazoezi ya kukimbia sana kadhalika watu ambao ni wenye uzito mkubwa sana na wale ambao huvaa viatu visivyo na visigino na wale wanaovaa viatu vyenye visigino virefu mara kwa mara.
CHANZO/VISABABISHI
Inakadiriwa kuwa wanawake na wanaume walio katika umri wa miaka 40_70 wapo katika hatari kubwa ya kupata tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis), kadhalika wanawake wameonekana ndio wahanga wa kubwa wa tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino ( plantar fasciitis)kuliko wanaume pia wanawake wajawazito nao wamekua wakisumbuliwa na tatizo hili vipindi vya mwisho vya ujauzito.
Lakini pia Mpendwa msomaji ili uweze kuelewa chanzo cha tatizo hili napenda kukujuza kua katika miguu yetu kuna tishu nyembamba ndefu inayopatikana katika maunganio ya nyayo na kisigino ambayo iko moja kwa moja chini ya miguu yetu,tishu hii inasaidia upinde wa mguu wako na kutusaidia hasa wakati tunapotembea au kusimama.
Lakini Iwapo kutatokea mvutano na msukumo mkubwa juu ya mishipa, mvutano au msukumo huo mkubwa huharibu tishu hiyo na kupelekea kupatikana maambukizi ambayo ndio chanzo cha kupata maumivu makali ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis).
DALILI
Mpendwa msomaji dalili zinazoweza kukujulisha kua una ugonjwa huu wa plantar fasciitis ni kupata maumivu makali chini ya miguu yako hasa eneo la kisigino.
Mgonjwa anapoamka na anapoweka miguu yake chini na kuanza kupiga hatua zake za kwanza asubuhi hupata maumivu makali sana ambayo hupungua kadri anavyopiga hatua lakini pia hali ya maumivu huweza kurudi baada ya muda mrefu wa kusimama au unaposimama baada ya kukaa.
VIPIMO NA UCHUNGUZI
Mpendwa msomaji uchunguzi wa tatizo hili kawaida hufanywa na daktari ama mtaalamu aliyebobea katika magonjwa ya mifupa hivyo baada ya kumuelezea daktari dalili zinazokusumbua daktari wako atachunguza mguu wako kwa umakini ambapo atalenga kutafuta ishara hizi:
Upinde wa juu au muelekeo wa juu ya kisigino chako
Eneo unalohisi maumivu chini ya mguu wako, iwapo ni mbele tu ya mfupa wa kisigino au la
Kuchunguza kujua maumivu makali unayapata wakati gani hasa hivyo daktari atajaribu kukupa mazoezi ili kuweza kubaini tatizo
Kadhalika daktari wako anaweza kukuagiza vipimo vifuatavyo
X_Ray na MRI_SCAN
Ili kujiridhisha kua hakuna chochote kingine kinachosababisha maumivu ya kisigino, kama vile kupasuka kwa mfupa(bone fractured)
MATIBABU
Mpendwa msomaji kuna aina kadhaa za matibabu ambazo daktari wako anaweza kukupatia ili kupunguza maumivu na kupunguza ukubwa wa tatizo.
Kadhalika Daktari Anaweza kupendekeza kutumia matibabu kadhaa kwa wakati mmoja kama ifuatavyo;
MATIBABU YA DAWA
Daktari huamua kukupatia dawa za kumeza aina ya Nonsteroidal anti inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen,naproxen sodium nk kwaajili ya kupambana na maambukizi pamoja na kusaidia kupunguza maumivu katika kisigino.
MATIBABU YA SINDANO
Daktari huamua kukupatia matibabu ya sindano zenye steroids iwapo maumivu ni makali na matibabu ya dawa nilizoelezea hapo juu kushindwa kupunguza maumivu,
Hivyo daktari wako atakuchoma sindano ya steroid sehemu ambayo unahisi maumivu makali zaidi katika kisigino chako hii itakusaidia kupunguza maumivu kwenye kisigino kwa muda angalau wa mwezi mmoja au zaidi.
MATIBABU YA TIBA MWILI(PHYSICAL THERAPY)
Ndugu mpendwa msomaji iwapo matibabu ya dawa,sindano na hata mazoezi kushindwa kusaidia kuondoa tatizo hili daktari atakupendekezea uende kwa mtaalamu wa viungo (physical therapist),Ambapo Utajifunza mazoezi ya kunyoosha na kuimarisha tishu zilizopo miguuni na misuli ya miguu ya chini. Kadhalika Mtaalam wako wa mwili anaweza pia kukupatia huduma zingine kama kukufanyia massage,kukushauri kutumia night splint,foot pads, na hata ultrasonography kusaidia kupona kwa muda mrefu.
Lakini pia Iwapo hauonyeshi maendeleo baada ya miezi kadhaa, daktari wako anaweza kupendekeza utaratibu mwingine kama vile Shockwave therapy, tenex na hata kushauri ufanyiwe upasuaji.
OPARESHENIDaktari hufikia maamuzi ya kukufanyia upasuaji mara baada ya njia zote zilizotumika kushindwa kukusaidia yani kufanyiwa upasuaji kwa tatizo hili kawaida ni njia ya mwisho ikiwa una maumivu makali au jeraha la muda mrefu ambalo matibabu mengine hayakusaidia.
Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kupata maumivu makali chini ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis/policeman heels) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tunatoa huduma ya matibabu ya ushauri na dawa za kuondoa magonjwa mbalimbali katika mwili kama vile matatizo ya hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na kadhalika karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako
GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
0 comments: