FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA CHUNJUA/VIJIUVIMBE/VIGWARU/VIOTEO VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI(PLANTAR WARTS/FOOT WARTS)

CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA CHUNJUA/vijiuvimbe/VIGWARU/VIOTEO VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI(PLANTAR WARTS/FOOT WARTS)


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya siku nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya matibabu ya tatizo la chunjua/vijiuvimbe/vigwaru/vioteo vinavyoota kwenye visigino/nyayo na sehemu za miguuni.

JE, TATIZO LA CHUNJUA/VIGWARU/VIOTEO VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI (PLANTAR WARTS/FOOT WARTS) ni Nini?

Ni viuvimbe/vigwaru/warts/vioteo vidogovidogo vinavyotokea kwenye kisigino au sehemu ambazo zinabeba uzito za kwenye miguu. Mgandamizo kwenye maeneo hayo huweza kusababisha vichunjua hivyo vya miguuni(plantar warts) kuota kuelekea ndani, chini ya tabaka nene la ngozi (callus).
Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya HPV(Human papilloma Viruses),Kirusi huyu huingia mwilini kupitia sehemu ndogo ulizojikata, au sehemu nyingine dhaifu za maeneo ya chini ya mguu.
Kwa maana hiyo ugonjwa huu unasababishwa na virusi hivyo anapoingia kwenye tabaka la juu la ngozi ya kwenye unyayo kupitia vijijeraha vidogo au maeneo mengine yaliyo dhaifu yaliyo maeneo ya chini ya mguu.

Kadhalika virusi hivi hupatikana kwa wingi, na kuna aina tofauti zaidi ya 100 ya virusi hawa Lakini ni aina chache tu ambazo zinaweza kuleta chunjua kwenye mguu. Aina nyingine zinaweza kuleta chunjua kwenye maeneo mengine ya ngozi au kwenye utando telezi.

Pia ifahamke kutokana na kua kila mtu ana kinga zake za mwili zenye uwezo tofauti wa kupambana na Virusi basi  Si kila mtu atakayegusana na kirusi huyu atapata chunjua. Hata watu wa familia moja wana uwezo wa kustahimili kirusi huyu kwa viwango tofauti.

Kadhalika virusi  wanaoeneza chunjua za miguuni (plantar warts) ni wenye kuambukiza japo kua hawaambukizi kirahisi. Kwa hiyo chunjua hizi haziambukizi kwa kugusana.
 Lakini wanapenda kuishi kwenye mazingira ya vuguvugu, yenye unyevu. Kwa hiyo unaweza kumpata kirusi huyu kwa kutembea peku kwenye mabwawa ya kuogelea,kuvaliana soksi au viatu na kuchangia taulo na muathirika wa tatizo hili,kirusi akipenya sehemu moja, anaweza kuenea hadi maeneo mengine na kusababisha chunjua.

CHANZO/VISABABISHI

Mpendwa msomaji hapo juu nimeelezea kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi vinavyoitwa HUMAN PAPILOMA VIRUSES (HPV)
Kadhalika kuna aina 120 za virusi hivi vya human papiloma viruses Ila kuna aina chache ambazo husababisha chunjua za miguuni,aina nyingine husababisha chunjua sehem nyingine tofauti za mwili.
Aina za HPV 57, 27 na 1a zimeonekana zaidi kusababisha chunjua za miguuni.
Mtu hupata maambukizi ya virusi hawa kwa njia ya ngozi kwa kupitia magusano ya moja kwa moja.
 Kadhalika imeonekana kuwa maambukizi huingia katika ngozi kutoka maeneo yanayoweza kuenezwa kwa virusi hivi kama katika mabwawa ya kuogelea ya jamii.
Mara baada ya mtu kuambukizwa virusi vya HPV, maazimio ya kusambaza maambukizi mwilini hutegemea maendeleo ya lymphocyte za kinga ambazo huharibu seli zilizoambukizwa na virusi. 
Lakini pia kuna chanjo zinazopatikana kwa ajili ya  kujilinda dhidi ya maambukizo ya virusi hawa wa HPV wanaosababisha vinyama sehemu za siri lakini hakuna chanjo dhidi ya HPV zinazosababisha vichunjua miguuni.
Hivyo ni wajibu wetu kujiepusha kupata maambukizi na hata kuepusha wengine kuambukizwa kwakua ugonjwa huu huonekana katika makundi yote ya umri ingawa huathiri sana vijana kuliko wazee

DALILI


Mpendwa msomaji wetu dalili zinazoweza kukujulisha kua unasumbuliwa na tatizo hili ni kupata maumivu makali ya miguu kutokana na shinikizo kwenye miguu yako wakati unatembea au kusimama.
Kadhalika utaona sehemu ya mviringo au duara kwenye ngozi ama kioteo chenye gamba gumu.
Kinyama au kioteo kinaweza kuonekana kuwa na rangi ya manjano au kutu, au hata kuwa na madoa madogo meusi katikati.
Kukosa utulivu kwa kuhisi kutekenywatekenywa ndani ya kichunjua  pale unapokanyaga chini au kutembea.


VIpimo na uchunguzi


Mpendwa msomaji uchunguzi wa tatizo hili kawaida  hufanywa na daktari ama mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa kutizama na kuchunguza kwa umakini kugungua kama kweli  ni chunjua(warts)au  ni tatizo lingine. Iwapo kutakua na mashaka daktari anaweza kutuma sampuli ya tishu ya chunjua(warts)kwa mtaalam wa uchunguzi ili kuweza kujiridhisha.
Mathalani Daktari anaweza kuhisi ni matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha kuonekana sawa na tatizo la chunjua miguuni , kama vile calluses, corn's au black heels(ruptured capillaries).

MATIBAbu

Mpendwa msomaji wetu licha ya kuwepo kwa matibabu ya chunjua za miguuni (plantar warts),tatizo hili mara nyingine huondoka lenyewe bila matibabu. Karibu asilimia 65-78% ya watu wenye tatizo hili hupona bila ya kutumia dawa ndani ya miaka 2.
Kadhalika  baada ya vipimo na uchunguzi kugundulika ugonjwa huu,daktari wako anaweza kukuchagulia matibabu kulingana na hali uliyonayo.
Matibabu haya yapo ya aina tofauti kama ifuatavyo

prescription creams

Daktari anaweza kukuagiza kutumia dawa ya kupaka yenye asidi ya salicylic kutibu chunjua za miguuni, Kemikali hii ni chaguo la kwanza la matibabu kwa kuondoa chunjua za miguuni (plantar warts)

Waathirika wa tatizo hili wameonesha kupona kwa kutumia dawa ya asidi ya salicylic kwa muda mchache.

 Cryotherapy


Daktari huweza pia kushauri njia hii ya matibabu ambayo hugandisha chunjua kwa kutumia naitrojeni ya maji (liquid nitrogen). Ni njia bora sana kwa sababu imetoa matokea mengi mazuri ikiwa na madhara machache sana tofauti na matibabu mengine licha ya kuwa na maumivu makali lakini pia matibabu haya hayafai kutumika kwa watoto.

Laser treatment

Daktari huamua kutumia njia hii ya matibabu ambayo hutumika kuondoa chunjua  zilizoenea au zinazojirudirudia. Mionzi ya laser huharibu kabisa uvimbe  uliotokana na HPV hivyo kuondoa uwezekano wa viruses hivi kuendelea kuwepo
Matibabu haya ni yenye ufanisi kwa asilimia kubwa ingawaje gharama yake ni bei kubwa, muda mrefu wa matibabu, na kuacha makovu.

Immunotherapy

Njia hii ya matibabu hutumika Mara ambapo njia nyingine za matibabu zimeshindwa kufanya kazi ipaswavyo.
Tiba hii (immunotherapy)hufanya kazi ya kuchochea mfumo wa kinga ya mwili kupigana na virusi vya HPV ambavyo vinaendelea kusambaza ugonjwa ndani ya mwili

Fluorouracil (5-FU) ni dawa ya Kemikali yenye matumizi mengi ambayo pia kinyume na matumizi yaliyowekwa na mamlaka ya dawa na chakula  watu wanaweza  kutumia kupaka kama cream kwa chunjua za miguuni.
Kadhalika  Jumuiya ya matibabu haipendekezi  matumizi ya dawa hii kwa wanawake ambao ni wajawazito au wanaopanga kuwa wajawazito siku za karibuni.
Watu wanaweza pia kuchukua dawa ya kumeza kama vile cimetidine, kinyume na matumizi(off labels)kuongeza mwitikio wa kinga mwilini, ingawa kuna ukosefu wa ushahidi wa kutosha.
Watafiti wengine wamependekeza kwamba matumizi ya vidonge vya zinc husaidia sana kuongezeka kwa kinga mwilini na hivyo husaidia waathirika wa vichunjua(warts) kupona haraka.

NAMNA UNAVYOWEZA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA CHUNJUA UKIWA NYUMBANI

Mpendwa msomaji wetu kuna njia nyingi anazoweza kuzitumia mgonjwa kujitibia tatizo hili akiwa nyumbani lakini pia licha ya kuwa baadhi ya njia ninameziorodhesha hapa chini zimewasaidia wengi ila unahitajika kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya kabla hujatumia njia yoyote ili akupatie ushauri ni njia gani inaweza ikakufaa bila ya kukuathiri iwapo utakua una maradhi mengine kama vile kisukari,matatizo ya mzio nk.

1.KITUNGUU SAUMU, BAKINGS SODAS NA LIMAO

Kitunguu saumu kimekua kikitumika katika matibabu kwa muda mrefu sana,kutokana na uwezo wake wa kupambana na aina tofauti za magonjwa.
Ili kuweza kutibu vichunjua  menya vitunguu saumu punje 10,kisage kiwe laini changanya na  baking soda kijiko kimoja kisha changanya na limao.Paka mchanganyiko huu kwenye chunjua pia ukiweza funga na  plasta,kaa kwa masaa mawili hadi matatu osha. Paka mara 3 kwa siku. Ni vizuri usiku ukilala nayo. Baada ya muda mfupi utapata matokeo mazuri.

2.SIKI YA TUFAHA NA VITUNGUU MAJI (APPLE CIDER VINEGAR AND ONIONS)
Siki ya tufaha (Apple cider vinegar) imejizoelea umaarufu kutokana na uwezo wake wa kutibu magonjwa mengi tofauti.
Hapa unatakiwa kuchukua vitunguu maji viwili kata vipande weka kwenye bakuli ,changanya na apple cider kisha viache vilowane usiku kucha,asubuhi chukua vitunguu bandika kwenye visunzua kisha funga vizuri na plasta visitoke acha kwa masaa 4 hadi matano.Fanya hivi kila siku kwa muda wa wiki moja utajionea utofauti.

3.ASPIRIN
Vidonge aina ya aspirin ambayo ni dawa maarufu humezwa Kwa ajili ya kutuliza maumivu, hapa hutumika kinyume na matumizi (off labels)huimezi bali unaiponda upate  unga kisha changanya na matone ya mafuta ya  maji ilainike.paka kwenye chunjua Mara tatu hadi nne kwa siku. Baada ya wiki utajifurahia na kuona matokeo mazuri

4.RANGI YA KUCHA

Unaweza kushangaa juu ya jambo hili kwakua imezoeleka rangi ya kucha ni kwa ajili ya urembo pekee wa
kucha,jambo ambalo si la kweli kwani hapa rangi inafanya kazi nyingine ya kuondoa chunjua miguuni.
Unachotakiwa ni kupaka rangi kwenye chunjua mara tatu hadi nne kwa siku.
usiku unashauriwa kulala nayo na ubandue asubuhi.Ukifanya hivi kila siku mfululizo kwa muda wa wikimoja tuu utapata matokeo mazuri y a kukufurahisha

5.GANDA LA NDIZI MBIVU

Unaweza ukajiuliza "GANDA LA NDIZI LINAWEZAJE KUONDOA CHUNJUA"
Jibu ni rahisi chukua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na usugue kwenye chunjua Mara nyingi uwezavyo kwa siku .ili upate matokeo mazuri bandika plasta  na uiache kwa muda mrefu.

NOTED
Matibabu ya nyumbani huweza kuchukua muda mrefu kuleta matokeo,hivyo inashauriwa kuwasiliana na daktari wako kwa msaada zaidi wa matibabu.
Pia
Inashauriwa wote ambao ni waathirika wa tatizo hili kudhibiti maambukizi  katika sehemu zingine za mwili na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi haya ya virusi vya HPV kwa kufanya yafuatayo
1)kutochangia mataulo,viatu na soksi
2) kutochangia viwembe
3)kutogusa vichunjua kwa mkono ili kuzuia kuhamisha virusi kutoka sehemu moja ya mwili kwenda sehem nyingine
4) kuosha mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara

MATIBABU YA TATIZO LA CHUNJUA VIGWARU/MASUNDOSUNDO/VIJINYAMA VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI(PLANTAR WARTS/FOOT WARTS)CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kutokewa na chunjua/vinyama vidogovidogo vinavyotokea katika ngozi sehemu mbalimbali za mwili na hata miguuni (genitals warts and plantar warts) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam 
Tutakufanyia uchunguzi wa kujua ni aina gani ya chunjua ulizonazo pia tutakupatia dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya pasipo kukuunguza
Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la vinyama sehemu mbalimbali katika mwili,tatizo la hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre