FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI ( ADULTS NOCTURNAL ENURESIS)

 chanzo na matibABU YA TATIZO LA mtu mzima kukojoA KITANDani (ADULTS NOCTURNAL ENURESIS)


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya week nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya tatizo la mtu  mzima kukojoa kitandani ambapo kwa lugha ya kingereza na kitaalamu tunasema (adults nocturnal bedwetting/enuresis)

Je,tatizo la mtu mzima kukojoa kitandani(adults nocturnal ENURESIS) NI Nini?

Hili ni tatizo linaowasumbua watu wengi walio katika umri ambao tayari wana uwezo wa kuzuia mkojo,tatizo hili hutokea kwa mtu huyo ambaye tayari yupo katika umri wa kuweza kujizuia mkojo ila anakua bado anaendelea kukojoa kitandani au kwenye nguo.
Hivyo tunaweza kusema hili ni  tatizo la kushindwa kuzuia mkojo wakati wa mchana au usiku na linalotokea katika umri wa miaka mitano au zaidi.

Imezoeleka watoto wengi wanaacha kukojoa kitandani usiku au mchana katika umri wa miaka mitatu_minne,
Kadhalika asilimia 10 hadi 15 ya watoto wa miaka mitano wanaoendelea kujikojolea kitandani wengi wao ni wavulana ambao ni asilimia 7 kuliko wasichana ambao wenyewe ni asilimia 3.
Pia katika umri wa miaka 15 wanaoendelea kujikojolea kitandani ni asilimia 2 Hadi 3 tu, na asilimia 3 katika umri wa miaka 18 na kuendelea
 Kwahiyo tatizo la kujikojolea ni ugonjwa wa akili unaotokana na utofauti katika ukuaji wa fiziologia ya kuzuia mkojo.

Mkojo unapo hifadhiwa katika kibofu cha mkojo, kibofu kinatanuka kama puto. Katika sehemu za neva za kutanua kuta za kibofu cha mkojo zinapeleka ishara ya kuzuia mkojo katika akili.
Hii hutokea katika sehemu ya ubongo inayohusika na matendo yasiyo ya hiari. Kama ubongo wa mtoto haujapata ishara hii, au ukishindwa kujua maana ya hiyo ishara, hatua ya makusudi ya kuzuia mkojo haitafanyika hivyo mtu hushindwa kupata uwezo wa kuxuik mkojo.
Hali hii mara nyingi husababishwa na kuchelewa kwa ukuaji wa kibiologia wa utendaji kazi wa kuzuia mkojo na Ukuaji wa kijinsia unaweza kusababishwa na;

1} Kushindwa kwa akili kutambua ishara kutoka kwenye kibofu cha mkojo,
2} Ujazo mdogo wa kibofu cha mkojo; au 3} Usingizi mzito.
Kwa sasa tafiti zinaonyesha kwamba watu wanaokojoa kitandani ni wagumu kuamka kutoka usingizini kuliko ambao hawana tatizo hilo.
Ni muhimu kutambua kwamba watu hawa hawajikojolei kwa makusudi na kawaida huona aibu kwa sababu hiyo hivyo ukiwa ndugu au mzazi au mpenzi wa mwenye tatizo hili haupaswi kumdhalilisha kwa kumwaibisha au kumtenga bali unatakiwa kumsaidia kupata ufumbuzi wa tatizo Hili.

Kadhalika tatizo Hili la kujikojolea limegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Yani
1)Primary enuresis
Aina hii ni pale mtu anaposhindwa kuwa na uwezo wa kuzuia mkojo tangia utotoni kwake,

2)Secondary enuresis
Aina hii ni pale mtu anaweza kujizuia kujikojolea kwa miezi sita au zaidi, halafu anaanza kujikojolea tena.
Mpendwa msomaji katika aina hiyo ya  kwanza yani PRIMARY ENURESIS hili ni tatizo la kurithi na huwapata watu wa familia moja. Tafiti kutoka somo la vinasaba inaonyesha kwamba ikiwa wazazi wote walikuwa wanakojoa kitandani, asilimia 77 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano na ikiwa mzazi mmoja alikuwa na tatizo hili, asilimia 44 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano. Na ikiwa wazazi wote hawakuwa na tatizo hili la kukojoa kitandani, asilimia 15 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano.

Kadhalika tatizo hili limegawanyika katika sehemu mbili.
1. Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku (NOCTURNAL ENURESIS) na lile la mtu kujikojolea wakati wa mchana (DIURNAL ENURESIS). Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku huonekana zaidi kwa watoto wa kiume na lile la kujikojolea mchana mara nyingi huwa kwa wasichana.


Chanzo Cha tatizo

Mpendwa msomaji utafiti umeonyesha kua kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili la kukojoa kitandani na miongoni mwa sababu hizo ni

1)OVERACTIVE BLADDER (OAB)
Hili ni tatizo la kibofu cha mkojo kuruhusu mkojo kutoka kwa ghafla bila ya muhusika kuwa na utayari na hivyo hukosa uwezo wa kujizuia kujikojolea,hali hii husababisha mtu kuonekana amejikojolea pasipo kujitambua.

2) STRESS (Msongo mkali wa mawazo )
Kwa upande mwingine tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa limesababiswa na matatizo ya hisia au ya kisaikolojia na msongo wa mawazo(stress).
Mara nyingi hii hutokea utotoni hasa pale mtoto anapozaliwa mtoto mwenzie yani mdogo wake, ugomvi wa wazazi, msongo anaoupata mtoto anapoanza shule au kutengana na wazazi. Matatizo kama haya na mengine yanayofanana yanaweza kumsababishia mtu kupata matatizo ya kihisia na kusababisha tatizo la kukojoa kitandani kuanza au kuzidi Hadi ukubwani.

3)MADAWA
Kuna baadhi ya dawa husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea dawa hizo ni za usingizi na dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya akili mfano wa dawa hizo ni
Clozapine,cariprazine, risperidone etc

4) TATIZO LA KUKOSA HAJA KUBWA (CONSTIPATION)

5) KISUKARI (DIABETES)

6) MATATIZO YA FIGO (KIDNEY DISEASES)

7)TEZI DUME (ENLARGED PROSTATE)
8)MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(URINARY TRACT INFECTION)
9)TATIZO LA KUFUNGWA KWA NJIA ZA HEWA WAKATI WA USINGIZI (OBSTRUCTIVE SLEEP APNEA)
10) KIBOFU CHA MKOJO KUWA KIDOGO(SMALL BLADDER)

VIPIMO NA uchuNGUZI




Mpendwa msomaji wetu iwapo una tatizo hili usiwe na dhana mbaya za kuhisi una mashetani  au majini fahamu hili ni tatizo lenye kutibika hospitalini hivyo achana na fikra hasi haraka fika hospitali,daktari wako atakufanyia uchunguzi na kukuliza maswali juu ya dalili zako na historia ya afya yako.
Unashauriwa kuwa na diary utakayoandika majibu ya maswali utakayoulizwa na daktari wako ili kusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo
Maswali utakayoulizwa ni ÷

Ni mara ngapi na kwa wakati gani huwa unajikojolea (je,ni usiku au mchana)?

Kiasi gani mkojo hukutoka (mwingi au kidogo)?

Ni kiasi gani cha vinywaji ulikunywa kabla ya kupanda kitandani?

Dalili zingine zozote ambazo umekuwa nazo(unahisi maumivu baada ya kutokwa na mkojo)?

Iwapo daktari wako atahitaji zaidi Kukufanyia uchunguzi ataagiza vipimo vifuatavyo÷

Urine culture and urine analysis: Vipimo hivi hutumika kuangalia maambukizi, damu isiyohitajika na vitu vingine kwenye mkojo.

Blood tests : kipimo hiki cha damu hutumika kuangalia figo na tezi, kiwango cha cholesterol iliyopo katika damu na iwapo kama Kuna shida ya upungufu wa damu au ugonjwa wa kisukari na homoni.

Bladder scans: hiki ni kipimo cha ultrasound ambacho mgonjwa atatakiwa kupima ili tujue ni kiwango  gani cha mkojo hubakia katika kibofu mara baada ya kukojoa.

Urodynamic tests: kipimo hiki kitahitajika kupimwa ili kuangalia au kuona jinsi sehemu ya chini ya mkojo huhifadhi na kutoa mkojo kiwango gani

Cystoscopy: kipimo hiki pia kitahitajika kuhitimisha uchunguzi ambapo daktari ataingiza bomba nyembamba na lens ndogo ndani ya kibofu cha mkojo ili kuangalia iwapo kuna dalili ya uvimbe,kansa na matatizo mengine.

MATIBABU 


Mpendwa msomaji napenda kuhitimisha somo langu hili kwa kukusihi iwapo una hili tatizo au ndugu yako analo tafadhal fahamu kuwa tatizo hili lina matibabu mengi ambayo matibabu haya hutofautiana kwani mengine hufanya kazi vizuri zaidi ya matibabu mengine.
Kadhalika matibabu ya kukojoa kitandani kwa watu wazima yamegawanyika  katika aina kuu tatu:

1) MATIBABU YANAYOHUSU MFUMO WA MAISHA(LIFESTYLE TREATMENT)


Aina hii ya matibabu inajumuisha kubadilisha ama kudhibiti baadhi ya mambo yaliyopo katika maisha ya muhusika ili kuweza kupona  tatizo hili,miongoni mwa hayo mambo ni

°Kudhibiti utumiaji wa vinywaji:Unashauriwa kupunguza unywaji wa vinywaji vyako wakati wa mchana na jioni.
Lakini pia unaruhusiwa kunywa vinywaji vingi zaidi wakati wa asubuhi ya mapema wakati unaweza kwenda chooni kwa urahisi, unatakiwa kuepuka matumizi ya vinywaji wakati wa jioni.

°Kuwa na ratiba ya kuamka usiku: unashauriwa kuweka kengele katikati ya usiku itakayoweza kukusaidia Kuamka mara moja au mara mbili kwa usiku ili kwenda kukojoa chooni hata kama Hauna mkojo hii itasaidia kujenga mazoea ya kuweza kushtuka unapohisi mkojo

°Kuwa na ratiba ya kwenda chooni mara kwa mara wakati wa mchana; hii itasaidia kuwa sehemu ya utaratibu wako. Hata ukilala wakati wa mchana weka kengele itakayokuamsha ili kuweza kuamka na kwenda kukojoa  lakini pia hakikisha unakojoa kabla ya kulala.

°Epuka vitu vinavyofanya kibofu cha mkojo kujaa kwa haraka; unapaswa kuacha matumizi ya kahawa,pombe,vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi kwani husababisha kibofu chako cha mkojo kujaa na kusababisha mkojo wa mara kwa mara.

2) MATIBABU YANAYOHUSISHA DAWA (MEDICINE)

Aina hii ya matibabu imegawanyika katika sehemu nne kulingana na sababu au chanzo cha tatizo kilichogunduliwa ambapo ni
°dawa za antibiotics hizi hutolewa kutibu maambukizo ya njia ya mkojo(urinary tract infection)

°dawa za anticholinergic hizi hutolewa kwa ajili ya kutibu na kutuliza tatizo la misuli ya kibofu cha kibofu

°dawa za desmopressin acetate hizi hutolewa kwa ajili ya kuongeza viwango vya ADH ili figo zako ziache kutoa mkojo mwingi usiku

°dawa za 5-alpha reductase inhibitor hizi hutolewa kwa ajili ya tatizo la tezi dume na hutumika pia kutibu tatizo hili la kukojoa kitandani pia
Mfano wa dawa hizo ni finasteride


3) MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI (SURGERY)

Aina hii ya matibabu huamuliwa kufanyika kutokana na ukubwa wa tatizo na chanzo au kisababishi cha tatizo hili kuwa kubwa

1)SACRAL NEUROMODULATION THERAPY


Hii ni moja wapo ya chaguzi kadhaa za matibabu ya oparesheni  kwa ajili ya kutibu tatizo la kukojoa kitandani kwa mtu mzima ambapo tatizo hilo limetokana na kuwepo kwa matatizo katika kibofu cha mkojo kushindwa kudhibiti au kuzuia mkojo kutoka (overactive bladder)

2) AUGMENTATION CYSTOPLASTY


Haya ni matibabu ya upasuaji katika kibofu cha mkojo ambapo upasuaji hufanyika kwa ajili ya Kuongeza ukubwa wa kibofu cha mkojo kutokana na tatizo la kibofu kuwa kidogo (Small bladder)
Lengo la utaratibu huu ni kuongeza ukubwa na uwezo wa kibofu cha mkojo

3) PELVIC ORGANS PROLAPSE FIX

Haya ni matibabu yanayoweza kuhitajika ikiwa kuna viungo vya uzazi vya kike ambavyo havipo kwenye nafasi iliyokusudiwa nikimaanisha viungo hivyo kutoka mahali na kushinikiza  uzito wote katika kibofu cha mkojo.

4) DETRUSOR MYECTOMY


Huu ni upasuaji ambao unajumuisha kuondoa sehemu au safu zote za nje za misuli ambazo huzunguka kibofu cha mkojo. Hii inalenga kupunguza kiwango na nguvu ya msukumo/shinikizo katika kibofu cha mkojo ambayo husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea pasipo ridhaa yake

NOTED
Mpendwa msomaji wetu ni muhimu kukumbuka kuwa waathirika wenye tatizo hili wataacha kukojoa kadiri wanavyopata matibabu  na ikiwa utamsaidia inavyotakiwa, utamsaidia kuacha mapema zaidi kujikojolea kitandani.
Dharau,kejeli,masimango,kumpiga, au kumchapa mtu mwenye tatizo hili awe mkubwa au mdogo unamuongezea tatizo na kufanya tatizo lizidi au kuchelewa kuisha.
 Ni muhimu sana kumstiri,kutomtisha au kumsema vibaya mwenye tatizo hili. Kufanya hivyo sio tu kama kutazidisha tatizo bali pia humfanya kuwa katika hatari ya kupata matatizo mengine ya kisaikolojia kwa wakati huo na hata baadae katika maisha yake.
Ili kumsaidia mtu mwenye tatizo hili ni muhimu na inashauriwa kumhakikishia na kumfariji  kwa kumuonesha kua anapitia hatua ya kawaida ya maradhi na kuwa kadiri siku zinapita tatizo hilo litaisha. Hii itamsaidia mgonjwa kutopata msongo(stress) na kuusaidia mwili kufanya kazi yake vizuri ambayo hatimaye humsaidia kuondokana na tatizo hili mapema zaidi.


MATIBABU YA TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI (ADULTS NOCTURNAL BEDWETTING/ENURESIS )NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER



Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la kukojoa kitandani ( adults nocturnal bedwetting/enuresis) na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia huduma na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako


Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud ) 

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre