FAHAMU TATIZO LA KUWA NA HOFU NA WASIWASI KUPITILIZA (ANXIETY DISORDERS) NA MATIBABU YAKE

FAHAMU TATIZO lA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,
Tunakuombea afya njema zaidi wewe pamoja na familia yako na wote unaowapenda
MWENYEZIMUNGU MTUKUFU AZIDI KUWAHIFADHI NA KUWAJAALIA REHMA ZAKE 
AMEEN!

Naam leo nimeona ni khery tukaongelea juu ya mada hapo juu kutokana na athari tunayoiona katika jamii zetu kwa watu wengi kuathirika kisaikolojia kwa kukosa uwezo wa kujiamini kwa kuathirika kwao kwa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza,mathalani ni kitu cha kawaida mtu kupata wasiwasi au hofu pale anapopatwa na changamoto za kimaisha kwa kushindwa kupata ajira, kushindwa kufaulu shuleni, kusalitiwa ama kukosana na mpenzi wake,kufiwa,kufilisika,kuhofia usalama wa maisha yake na kadhalika  lakini endapo wasiwasi na hofu vikakufanya ushindwe kumudu maisha yako ya kawaida kama unavyopenda, hapo ndipo tunasema mhusika Ana tatizo la wasiwasi na hofu kupitiliza ( anxiety disorder/ugonjwa wa hofu na wasiwasi)

Kuna aina nyingi za tatizo la kuwa na wasiwasi na hofu kupitiliza (anxiety disorders)  na njia nyingi za kutibu au kumfanya mtu ajisaidie. Ukishakuwa umelijua tatizo lako hili la wasiwasi na hofu kupitiliza (anxiety disorder) kuna hatua za kuchukua ili kupunguza dalili zake au kurudisha udhibiti wa maisha yako hivyo usijali sana iwapo unasumbuliwa na hill tatizo


JE, TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS) NI NINI?


Wasiwasi au hofu unaweza kuelezewa kuwa ni mwitiko wa mwili wako kwa vitu hatarishi kwa maisha yako vinavyokuja au unavyofikiria vinaweza kuja.
Wasiwasi unahusiana sana na hofu ambayo ni mwitiko wa mwili wako kukujulisha kuhusu hatari halisi (hatari iliyo mbele yako) au inayofahamika kuja siku za karibuni.
Hivyo Hofu na wasiwasi uliopitiliza ni hali ya ugonjwa wa kiakili ambao unamfanya muhusika kua na hofu muda wote na kukosa utulivu wa akili na hata kushindwa kutoa maamuzi.

Mfumo wa ubongo hudhibiti mwitiko huu wa mwili wa kupambana au kuyakimbia mazingira hatarishi, na mara nyingi huambatana na kupanuka kwa mboni za macho, kuongezeka kwa kasi ya mapigo ya moyo, na kuongezeka kwa jasho/uhemaji.

Mwitiko wa wasiwasi unaweza kuambatana na uangalifu zaidi wa mazingira na kukaza kwa misuli tayari kuikabili hatari.
Wasiwasi unaweza kuwa na manufaa, kama kuongeza ufanisi na kufanya vizuri zaidi kwenye michezo, au kuzungumza mbele ya kadamnasi. Pamoja na kuwa hii ni miitiko ya kawaida ya mwili na mara nyingi ni miitiko yenye manufaa wakati wa hatari, wasiwasi unaweza kuwa na athari endapo utazidi kiwango au ukiendelea kuwepo bila ya kuwepo kwa hatari
Wasiwasi mwingi uliokithiri(kupitiliza) unaweza kukukosesha raha, na kuharibu utendaji wako wa kazi, na huu ndio huitwa ugonjwa wa hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder)
Lakini pia tatizo hili lipo katika namna au aina nyingi.

Aina ZA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY disorders)

Tatizo la hofu na wasiwasi mwingi uliopitiliza (anxiety disorders)hutofautishwa kufuatana na aina ya kitu au mazingira yanayosababisha woga na wasiwasi, pamoja na namna ya fikra anazokuwa nazo mtu akishikwa na hofu au wasiwasi.
Lakini Kusudi mtu aitwe ana tatizo hili, hofu na wasiwasi lazima viwe vya muda mrefu, vilivyodumu miezi 6 au zaidi.
Matatizo ya kuwa na wasiwasi kwa kawaida huanza utotoni lakini hudumu ukubwani.

Aina ya tatizo la kuwa na hofu na wasiwasi kupitiliza (anxiety disorder ni ;

Specific PHOBIAS ANXIETY DISORDERS
 Hii ni hali ya kuwa na hofu na wasiwasi uliokithiri kwa kuhofia kitu au mazingira fulani, mfano;kama buibui kuwa juu ya nyumba yako,kupanda ndege, au kukaa sehemu zilizofungwa Katika mambo ya kijamii.

SociAL PHOBIA/PERFORMANCE ANXIETY DISORDERS

Hii ni hali ambayo mtu anakuwa na wasiwasi na hofu kubwa kwa kuogopa kushiriki shughuli za kijamii, au mazingira yanayomfanya watu wamwone au kumjadili.

GENERALIZED ANXIETY DISORDERS(GAD)

 ni aina ya tatizo linalojitambulisha kwa mtu kuwa na wasiwasi na hofu kubwa inayodumu kwa kipindi kirefu inayotokana na maeneo tofauti ambayo ni vigumu kuyadhibiti.
Woga unaoendana na aina ya tatizo la wasiwasi aina ya GAD huathiri uwezo wa mtu wa kufikiri, kupata usingizi, au kufanya shughuli fulani.
 Dalili zake hujionyesha kwenye hisia na tabia na namna ya kufikiri ambavyo ni matokeo ya hali ya mwili kufikiria kuwa kuna hatari.
Ukiwa na aina hii ya wasiwasi GAD, utapata wasiwasi kutokana na vitu vinavyowapa wasiwasi watu wote, lakini wewe utaupeleka wasiwasi huo kwenye ngazi nyingine, ya juu zaidi
Mfano;
Mfanya kazi mwenzako akitoa maoni yake kuhusu hali ya uchumi kwako shida utaanza kufikiri sana na kuwa na hofu
rafiki yako asipotoa majibu kwa simu yako haraka, unaanza kufikiri kuwa mahusiano yenu si mazuri.
Wakati mwingine hata wazo tu la kuwa utashinda kazini kwako ni mwanzo wa wasiwasi. Unaendesha shughuli zako ukiwa umejaa hofu isiyobainika, na hata kama hakuna kitu cha kuanzisha hofu hizo.

Waweza kuwa unatambua kuwa wasiwasi wako unazidi hali halisi, au unaamini kuwa wasiwasi wako unakulinda kwa namna fulani, mwisho wake ni ule ule. Huwezi kuyafuta mawazo yanayokuletea wasiwasi. Yanazidi kutembea kichwani mwako, yakijirudiarudia  bila kufika mwisho.

SEPARATION ANXIETY DISORDERS
Imezoeleka kuona watoto wadogo ndio wao  pekee ambao huhisi hofu au wasiwasi wakati mtu wanayempenda anaondoka,lakini kumbe Mtu yeyote anaweza kupata hofu na wasiwasi na kujitenga kwa kuwaza au kuhofia juu ya mtu wao wa karibu kua kuna tatizo linaweza kumtokea.

SELECTIVE MUTISM ANXIETY DISORDERS
Hii ni aina ya hofu na wasiwasi wa kijamii ambao watoto wadogo au watu wakubwa ambao huongea kawaida na familia zao lakini wanakua na hofu na wasiwasi yani hawawezi kuzungumza hadharani kama shuleni,kazini nk
Yani kushindwa kuzungumza kwenye baadhi ya mazingira ya watu wengi kama shuleni,kazini nk

AGORAPHOBIA ANXIETY DISORDERS
Hii ni aina ya hofu au wasiwasi uliopitiliza ambao humfanya mtu kuogopa sana kuwa katika mahali ambapo inaonekana kuwa ngumu kutoroka au kupata msaada ikiwa dharura itatokea.
Mfano:
Unaweza kuwa na hofu au kuhisi kuwa na wasiwasi unapokuwa kwenye ndege, usafirishaji wa majini nk

PANIC ANXIETY DISORDERS
Hii ni aina ya wasiwasi au hofu kubwa ambayo inaleta shambulio la hofu Sana kwa ghafla linapotokea jambo unaweza kutokwa kwa jasho kuwa na maumivu ya kifua na kuwa na maumivu ya pigo la moyo wakati mwingine unaweza kuhisi ni kama unavunja au kuwa na mshtuko wa moyo kutokana na hofu kupitiliza

MEDICATION INDUCED ANXIETY DISORDERS
Baadhi ya dawa huweza kusababisha dalili fulani za hofu na wasiwasi
uliopitiliza


CHANZO CHA TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)

Hadi sasa hakujaweza kupatikana chanzo cha moja kwa moja kinachosababisha tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza,ila kuna mambo kadhaa yanaweza kuelezwa kuwa ni chanzo kutokana na ufuatiliaji wa chanzo kwa muda mrefu imeonesha kuwa tatizo la hofu na wasiwasi inaweza kurithiwa kutoka  katika familia yako pia vyanzo vingine vyenye kufikiriwa ni 
Baadhi ya magonjwa: Utafit unaonyesha kuwa kuna magonjwa yanayohusishwa kuwa ni chanzo cha mtu kupata tatizo la hofu na wasiwasi kupitiliza baadhi ya magonjwa hayo ni
KISUKARI, MAGONJWA YA MOYO, MAGONJWA YA MAPAFU,PUMU, MAGONJWA SUGU YA TUMBO, MAGONJWA YA TEZI YA THYROID nk

Matatizo ya ubongo. Utafiti unaonyesha tatizo la hofu na wasiwasi zinaweza kuhusishwa na mzunguko mbaya katika ubongo unaodhibiti woga na hisia

Mazingira. Hii inahusu matukio yanayomusumbua mtu ambayo ameona au kuishi kupitia matukio ya maisha mara nyingi huweza kuhusishwa na tatizo la hofu na wasiwasi ni pamoja na unyanyasaji wa watoto na kutelekezwa, kifo cha mpendwa, au kushambuliwa au kuona vurugu na kushuhudia baadhi ya matukio ya ajali yenye kuogopesha

Matumizi ya dawa. Dawa zingine zinaweza kutumiwa kuficha au kupunguza dalili fulani za wasiwasi. Shida ya wasiwasi mara nyingi huambatana na ulevi na matumizi ya sigara

Ni muhimu kupata uchunguzi kamili wa mwili ili kudhibiti hali zingine za matibabu wakati wa kuzungumza na daktari wako juu  tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza


DALILI ZA TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)
Dalili za kawaida kwa mtu mwenye tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorders) ni pamoja na:

. Kutotulia yani kukukosa utulivu na kujaa wasiwasi
. Kuchoka kirahisi, kuwa mchovu;
. Hupata shida kutuliza mawazo kwenye kitu ambacho kinaweza kuonekana kuwa ni tatizo la kumbukumbu au la kawaida tu
. Kuwa na hisia dhaifu yan kuhisi kuwa ubongo unakuwa mtupu yani unashindwa kupata mawazo mazuri muda wote unajihisi kuhofu hatari 
. Kuwa na hasira za haraka
. Kukakamaa kwa misuli
. Kuumwa kichwa na kuwa na hofu kubwa
. Mapigo ya moyo kwenda mbio kupata shida kupumua
. Matatizo ya usingizi (kukosa usingizi)
. Kupata vidonda vya tumbo na kiungulia
. Kukosa ujasiri wa kupambana na changamoto
Wasiwasi unaohusiana na hofu ya kitu fulani (specific or simple phobia) au wasiwasi wa mambo ya kijamii (social phobia) unaweza kusababisha kuyakwepa mazingira fulani au kukuza dalili zinazoleta panic attack – hofu kubwa ya ghafla inayofikia kilele katika muda mfupi.

VIPIMO NA MATIBABU

Hatua ya kwanza ni kuonana na daktari wako ili kuhakikisha kuwa hakuna shida ya kiafya inayosababisha dalili za hofu na wasiwasi uliopitiliza.
Si kila mtu anayekuwa na wasiwasi sana ana tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder) Unaweza kuwa na wasiwasi kwa sababu ya kuwa na majukumu mengi,ratiba kali ya kazi, kukosa usingizi au mazoezi, msongo wa mawazo au majukumu ya ulezi wa familia  nyumbani, au kunywa kahawa kupita kiasi.
Lakini pia kama maisha yako si ya furaha na ni ya msongo wa mawazo na huzuni kila wakati, ni ishara tosha kuwa una tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza hivyo unahitajika kufika hospital kwa uchunguzi zaidi.
Kadhalika matibabu ya tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza hutegemea asili au chanzo cha tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza hivyo hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine
Mara nyingi matibabu ya tatizo hili huchanganywa kutegemeana na hali ya mgonjwa jinsi ilivyo ambapo kuna matibabu ya dawa na ushauri nasaha ambao mgonjwa akipatiwa anaweza kupona pasipo kuhitajika kutumia dawa
Walakini, ikiwa njia ya ushauri haipunguzi athari za dalili za wasiwasi, au ikawa ni chanzo cha kuongeza mashambulizi ya mshtuko na wasiwasi wa ghafla yani dalili kuwa kali daktari wako atawajibika kukupatia huduma ya matibabu mengine yatakayojumisha dawa na ushauri nasaha.
Kadhalika Kuna matibabu ya tabia ya utambuzi (CBT) ambayo ni aina ya tiba ya kuongea, inaweza kumsaidia mtu kujifunza njia tofauti za fikra na kusaidia kuondoa wasiwasi pia dawa zinazotumika sana ni dawa za kupunguza wasiwasi (kwa ujumla zinatumika kwa kipindi kifupi tu) ambazo ni Antidepressants,anxiolytics,beta-blockers ambazo hutumiwa kwa matatizo ya moyo, wakati mwingine hutumiwa kudhibiti dalili za mwili za wasiwasi na mfadhaiko.


HATUA ZA KUFATA KUPAMBANA NA TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)
Mpendwa msomaji nina imaani ya kwamba umejifunza mambo mengi kuhusu tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorders)
Napenda nihitimishe kwa kukupatia ufumbuzi wa kuweza kupambana na tatizo hili ukiwa una shaka au kuhofia kuwa unalo hili tatizo
Kwa kufanya yafuatayo unaweza kupunguza wasiwasi na kudhibiti dalili za hofu na wasiwasi uliopitiliza na kupunguza ukubwa wa tatizo


EPUKA KUKAA PEKE YAKO,JICHANGANYE NA WENGINE.
Upweke unaweza kukuletea au kukuongezea wasiwasi, jitahidi kuwa muwazi zungumzia matatizo yako kwa watu wako wa karibu na changamana nao ili uweze kujipunguzia hofu na kupata matumaini na kuwa ni mwenye kujiamini
Jitahidi kila wakati kukutana na marafiki zako, jiunge na vikundi vya kusaidiana, au mshirikishe mambo yanayokusumbua mtu umpendaye.
 Kama huna mtu wa namna hii, hujachelewa kuanza kujenga mahusiano mapya yenye kukujenga


DHIBITI MSONGO WA MAWAZO
Kama unasumbuliwa sana na msongo wa mawazo jitahidi kupata ushauri wa kuondokana na msongo wa mawazo au dawa zitakazokusaidia kuondokana na msongo wa mawazo kadhalika Unaweza pia kuona ni majukumu yapi ya kuyaacha, kuyapunguza au kuwaachia wengine ili yasiushughulishe ubongo wako kiasi cha kupata hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder)

JENGA TABIA YA KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU
Kufanya mazoezi ya mwili ni njia ya asili ya kupunguza msongo wa mawazo na kuondoa wasiwasi pamoja na mfadhaiko
Ili Kupata matokeo bora kabisa, lenga kufanya mazoezi ya kuongeza mapigo ya moyo na kutoa jasho (aerobic exercises) kwa muda wa dakika 30 kila siku.
Mazoezi au shughuli za kuifanya mikono na miguu kuwa katika mwendo kwa wakati mmoja (rhythmic activities) ni ya manufaa sana. Jaribu kutembea, kukimbia, kuogelea, kucheza,kurukaruka nk itasaidia Kupunguza hatari na dalili za hofu na wasiwasi uliopitiliza

PATA USINGIZI WA KUTOSHA
Kukosa usingizi wa kutosha kunaweza kukuza tatizo la kuwa na wasiwasi kwa hiyo jitahidi kupata wasaa wa kulala masaa 8 hadi 9
Kulala usingizi mzuri ni miongoni mwa mambo yanayouweka mwili katika hali nzuri ya afya


JIAMINI NA PINGA(UKATAE) WASIWASI
Unapopatwa na hali ya  kuhofu au kuwa na wasiwasi uliopitiliza ikatae hiyo hali kwa kuamua kutoogopa kitu chochote jipatie ujasiri jiamini na ishinde hofu uliyonayo tena jitengenezee mkakati wa kufanya mambo yote ambayo unayapatia hofu hii itakusaidia kupambana na tatizo hili ambalo ni hatari kwa afya ya akili na mwili

EPUKA POMBE, SIGARA, MADAWA NA KAHAWA
Ikiwa unapambana na tatizo la kushinda wasiwasi, unatakiwa kupunguza au kuepuka kabisa matumizi ya pombe, kahawa,sigara na madawa ya kulevya kwasababu vitu hivi hasa pombe inafanya hali ya wasiwasi kuongezeka tofauti na kule kudhania kuwa inapunguza wasiwasi. Kadhalika na sigara inaonekana kama ni kitulizo bila ya kujua kua kuna sumu ya nikotini ambayo ndio kichocheo kikubwa cha kusababisha ongezeko la wasiwasi.
Unashauriwa iwapo una nia ya kupona tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorders) epukana na matumizi ya vitu hivyo.


VIFAHAMU VYAKULA VYENYE KUSAIDIA KUONDOA WASIWASI
Ni vyema ukafaham kuwa kuna vyakula ambavyo ukila kwa wingi vinakusaidia kupunguza ukali wa dalili za tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza kutokana na uwezo wa vyakula hivyo kusaidia  ubongo kufanya kazi ipasavyo
Baadhi ya vyakula hivyo ni ÷
1)MAFUTA YA SAMAKI (FISH OIL)

Mafuta ya samaki yana faida nyingi sana katika mwili wa mwanadamu na yanasaidia kupunguza hofu na wasiwasi.
Hii ni kutokana na kua yana virutubishi ambavyo vinakuza afya ya ubongo, pamoja na vitamini D na asidi ya asidi ya omega-3 eicosapentaenoic acid (EPA) na asidi ya dosahexaenoic (DHA) 

EPA na DHA zinaweza kusaidia kudhibiti homoni na kemikali za neurotransmitters  na serotonin kuondoa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza.


2)BINZARI NYEMBAMBA (TUMERIC)
 Unaweza ukastaajabu kusikia kiungo hiki kina uwezo wa Kupunguza na kuondoa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza
Ukweli ni kwamba binzari nyembamba ina uwezo wa kupambana na Kupunguza dalili za hofu kwa Kusaidia ufanyaji kazi katika ubongo

3) CHOCOLATE NYEUSI
4)MAZIWA MGANDO
5)MBEGU ZA CHIA(CHIA SEEDS)
6)KOROSHO NA LOZI(CASHEWS NUTS&ALMONDS)
7) MATUNDA YENYE VITAMIN C NYINGI
8)MAYAI NA NYAMA



 TATIZO HILI LA ANXIETY DISORDERS NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder) na magonjwa mengine mbalimbali na mmejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia ushauri au dawa za kuondoa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder)na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako

NOTED;
Mpendwa msomaji iwapo wewe au ndugu yako ana tatizo hili fanya haraka ya kupata ufumbuzi wa Matibabu kwakua tatizo hili lina athari nyingi katika mfumo wa mwili 
Miongoni mwa madhara ya kuwa na tatizo hili la hofu na wasiwasi uliopitiliza ni kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa mengine makubwa kama
KUPATA SHINIKIZO LA DAMU, MFADHAIKO,MATATIZO KATIKA MFUMO WA UPUMUAJI,KINGA YA MWILI HUSHUKA,KUKOSA USINGIZI,KUPATA MATATIZO KATIKA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA NK

Tunamuomba ALLAH HIFADHI NA SALAMA TUWE WENYE KUNUSURIKA NA MARADHI MAKUBWA 
AMEEN


Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre