Ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya ugonjwa wa mkanda wa jeshi/moto wa mungu (shingles/herpes zoster).

Kwa miaka mingi sasa  ugonjwa huu umekua mkubwa na endelevu katika jamii kwa sasa ambapo pia imekua ikichukuliwa kwa dhana au fikra mbovu kua ugonjwa huu ni kipimo cha dalili/ishara ya kuwepo kwa virusi vya ukimwi katika mwili wa mgonjwa huyo kitu ambacho sio cha kweli kua na ugonjwa wa mkanda wa jeshi/moto wa mungu(shingles/herpes zoster) haimaanishi kua una ugonjwa wa ukimwi.

Mkanda wa jeshi/moto wa mungu kwa lugha ya kitabibu  shingles au zoster ni ugonjwa unaosababishwa na virus wabaya aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa maarufu  unaotokea hasa kwa watoto unaoitwa tetekuwanga(chickenpox).

ugonjwa huu umekua ukiwapata watu ambao waliwahi kuugua tetekuwanga huko kipindi cha nyuma,kwani mtu anapougua tete kuwanga na baadae akapona virusi hawa hujificha kwenye mishipa ya damu kwa miaka mingi hadi pale kinga ya mwili inapokua ndogo sana mwilini ndipo virusi hawa hujitokeza kwa mara nyingine na kusababisha ugonjwa mwingine mpya ambao ndio huu ugonjwa wa Mkanda wa jeshi/moto wa mungu (shingles).

Ugonjwa huu hatari ambao huathiri ngozi  huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali kulinganisha na ugonjwa wa tete kuwanga ambapo huathiri sana neva za kwenye ngozi.

Kwa kawaida shambulio la mkanda wa jeshi hutokea mara moja maishani ingawa laweza kujirudia kulingana na kinga ya mwili kua katika kiwango cha chini.

Kadhalika ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi unaweza kumpata mtu wa umri wowote ule ingawa watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi:

• Wenye umri wa zaidi ya miaka 60

• Mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya umri wa mwaka mmoja

• Watu ambao kinga yao ya mwili imepungua kwa sababu mbalimbali kama vile matumizi ya aina fulan za dawa, magonjwa kama vile maambukizi ya VVU (HIV/AIDS), saratani na utapiamlo(unyogofu)

Pia ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine! Lakini iwapo itatokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga maishani mwake na ambaye pia hajawahi kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo akakutana na mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto au mtu huyo atapatwa na ugonjwa wa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.


CHANZO/VISABABISHI

Mpendwa msomaji kama nilivyokwisha tangulia kueleza hapo juu kuwa ugonjwa huu husababishwa na virus aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga hivyo baada ya mtu kupatwa na tetekuwanga, virus hawa hubaki katika hali ya kupooza/kutokuwa na madhara (dormant) katika neva fulani za mwili lakini baada ya miaka kadhaa, iwapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu yoyote ile, virus hawa hupata tena nguvu/kuwa na madhara (active), kuibuka na kusababisha ugonjwa mpya ambao ndio huu ugonjwa wa mkanda wa jeshi.


DALILI


Dalili kuu kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yakiambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi. Maumivu pamoja na hisia za kuungua huwa makali sana na hutokea kabla ya vipele/michubuko kutokea kwenye ngozi. 

Kadhalika vipele au michubuko hiyo hutokea eneo fulani la mwili kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, mdomo au masikio.

Pia dalili nyingine ni pamoja na

• Maumivu ya tumbo 

• Homa 

• Maumivu ya mwili mzima 

• Vidonda sehemu za siri 

• Maumivu ya kichwa 

• Maumivu ya viungo 

• Kuvimba kwa mitoki/ matezi 

Pia iwapo  neva za maeneo ya uso zitaathiriwa, mgonjwa anaweza kupatwa na matatizo ya kutoona, kutohisi ladha na au kutosikia.


Vipimo na UCHUNGUZI


Hakuna vipimo maalum kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea pekee kadhalika daktari mzoefu anaweza kuutambua ugonjwa huu bila vipimo kabisa kwa kuchukua historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa. 

Pia huweza kutumika vipimo vya damu yaani FBP Kwa ajili ya kuonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu na antibodies dhidi ya virus wa tetekuwanga.


Matibabu

Mpendwa msomaji kwa bahati mbaya ugonjwa huu hauna dawa maalumu hospitalini hivyo matibabu ya mkanda wa jeshi  hujumuisha matumizi ya dawa tofauti kama vile Acyclovir, Famciclovir na Valacyclovir kwa ajili ya kuua virus wanaosababisha ugonjwa huu na kusaidia kupunguza maumivu, kuzuia madhara zaidi ya ugonjwa huu.

Dawa hizi hutolewa angalau saa 72 baada ya mgonjwa kuanza kuhisi maumivu na hali ya kuungua. Ni vema dawa zianze kutumika kabla ya vipele/michubuko kujitokeza.

Pia jamii ya dawa za corticosteroids kama vile prednisolone husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwa badhi ya wagonjwa. 

Kadhalika dawa nyingine zinazofaa kutumika ni pamoja na jamii ya antihistamines kwa ajili ya kupunguza muwasho hasa calamine lotion ambayo mara nyingi hutumika  kwa ajili ya kupunguza muwasho,pia mgongwa hushauriwa kupata mapumziko ya kutosha kwa kutulia nyumbani kwa muda kadhaa hata hivyo pia mkanda wa jeshi kwa kawaida huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu kupona.


MADHARA

Mpendwa msomaji napenda kukufahamisha licha ya kuwepo madhara mengi ya ugonjwa huu ila ni nadra sana kwa ugonjwa huu kujirudia tena iwapo ukatumia dawa ukapona hivyo ondoa hofu.

Lakini Iwapo neva zinazothibiti mwendo katika mwili zitakuwa zimeathirika, mgonjwa anaweza kupatwa na kupooza kwa muda au kwa kudumu kwa sehemu ya mwili iliyoathiriwa. Wakati mwingine, maumivu yanayosababishwa na mkanda wa jeshi yanaweza kudumu kwa miezi mpaka mwaka hata baada ya mgonjwa kupona kabisa. Maumivu haya yanayojulikana kama postherpetic neuralgia kwa kawaida huwakumba wagonjwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na husababishwa na uharibifu katika neva za mwili,

Kadhalika madhara mengine ya mkanda wa jeshi ni pamoja na kupatwa na shambulio jingine la ugonjwa huu, maambukizi ya bakteria, upofu iwapo eneo la jicho litahusika, ukiziwi, maambukizi katika utando wa ubongo (encephalitis), uwepo wa vimelea kwenye damu (sepsis) au ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt Syndrome iwapo utahusisha neva za uso, kadhalika kupatwa na homa ya uti wa mgongo na kubakia na makovu kama vile umeungua na moto.


NAMNA UNAVYOWEZA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA MAUMIVU UKIWA NYUMBANI

Mpendwa msomaji wetu kuna njia tatu ninazoziamini anazoweza kuzitumia mgonjwa kujitibia kwa kupunguza maumivu na kupona haraka tatizo hili akiwa nyumbani lakini pia ni muhimu na ni lazima kufika hospital na kutumia dawa ili kupata matokeo ya kupona kwa haraka.


PATA MLO WENYE VIRUTUBISHO VYOTE



Mpendwa msomaji napenda kukusisitiza kuwa lishe kamili ni muhimu kwa kutibu,kuzuia na kupigana na magonjwa ndani ya miili yetu.

Miongozo ya Lishe kwa Wamarekani inapendekeza kula lishe kamili inayojumuisha mboga nyingi, matunda, na nafaka nzima pamoja na kunde, karanga,nyama na samaki.

Kadhalika watu wenye kusumbuliwa na ugonjwa  wa mkanda wa jeshi(shingles/herpes zoster) wanashauriwa sana kula machungwa,nyama nyekundu, na mboga za kijani kibichi na matunda mekundu ambayo yamesheheni viambata vya  lycopene,carotenoids, lutein, zeaxanthin, na proitamin A.

Kiambata cha Carotenoids ni muhimu sana kwenye miili yetu  kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya kinga zetu.

kadhalika vyakula vifuatavyo vimeonekana kuwa na kiambata cha Carotenoids kwa wingi zaidi ni

vyakula vya rangi ya machungwa(orange foods): Vyakula hivyo ni karoti, maboga, na apricot.

vyakula vya rangi nyekundu(red foods): Vyakula hivyo ni tikiti, pilipili nyekundu, zabibu, na cherry

vyakula vya  rangi ya kijani(green foods): Vyakula hivyo ni parsley, mchicha, limao, lettuce, na broccoli.

Wakati unakula mlo kamili unashauriwa kuacha kutumia sukari tumia chumvi pekee katika milo yako pia epuka kahawa na vilevi hii itakusaidia kuboresha kinga yako ya mwili na kupunguza maumivu na kupona kwa haraka sana.


KUOGA MAJI BARIDI/VUGUVUGU MARA KWA MARA

Inashauriwa kuoga maji ya baridi au vuguvugu  walau mara 3_4 kwa siku hii itasaidia kupunguza maumivu na kuondoa umoto na homa zinazotokana na ugonjwa huo na kuzuia maambukizi mapya.


ACHA KUVUTA SIGARA/ACHA KUNYWA POMBE

Uvutaji sigara hautoi faida za kiafya na huwa hatari kila wakati. Ni muhimu kuacha sigara kwani inaongeza hatari ya saratani ya ngozi na magonjwa mengine.

Kadhalika uvutaji wa sigara na kunywa pombe hupunguza kinga kwa ajili ya kupambana dhidi ya maambukizi haswa kwa watu wazee, na kinga ikiwa ndogo ni sababu ya kutokupona haraka.


MATIBABU YA UGONJWA WA MKANDA WA JESHI (SHINGLES/HERPES ZOSTER) CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama unasumbuliwa na ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi(shingles/herpes zoster) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha kabla hujapata madhara makubwa tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam tuweze kushughulikia tatizo lako.
Tutakufanyia uchunguzi  kwa kina pia tutakupatia ushauri na dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya kabisa.

Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tunatoa huduma ya matibabu ya ushauri na dawa za kuondoa magonjwa mbalimbali katika mwili kama vile matatizo ya figo,mapafu,Moyo,macho, hedhi mbovu,uzazi, magonjwa ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa  na kadhalika karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )


Ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya siku nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya ugonjwa au tatizo la kutapika damu (hematemesis/vomiting blood).

Tatizo la kutapika damu limekua kubwa na endelevu katika jamii kwa sasa ambapo pia imekua ni dalili/ishara ya kuwepo moja ya matatizo kadhaa katika mwili wa binadamu.

Mpendwa msomaji tatizo hili kwa lugha zingine hujulikana pia kwa jina la HEMATEMESIS au VOMITING BLOOD ambapo huashiria kuwepo kwa ugonjwa ndani ya mwili wa binadamu ambapo pia ishara hii ya kutapika damu haitakiwi kuchukuliwa kimasihara au kupuuza kwani ni ishara kwamba kuna tatizo lenye kuhitajika msaada katika mfumo wa njia ya chakula au ndani katika viungo vingine hivyo uchunguzi wa kina na haraka unahitajika,

Kadhalika tatizo linaweza kuwa dogo, hivyo mgonjwa kutapika damu kidogo, au iliyo ganda kidogo pia tatizo linaweza kuwa kubwa kiasi cha mgonjwa akatapika damu nyingi, tena mbichi mfulululizo na kutishia uhai ikiwa hatapelekwa hospitali kwa matibabu rasmi pia kutapika damu huku kunaweza kuambatana na maumivu ya tumbo kwa juu au kutanguliwa na maumivu ya mara kwa mara ya tumbo upande wa juu, katika hali hii ya awali mgonjwa akifanyiwa uchunguzi ni rahisi kujua chanzo cha tatizo na kupatiwa matibabu haraka.

Lakini pia iwapo mgonjwa atatapika damu mbichi na wakati huo huo anatoka damu mbichi katika njia ya haja kubwa humaanisha hali ni hatarishi na inatakiwa apelekwe hospitali mara moja kwani damu inayovuja inachuruzika kupitia kwenye utumbo na kutokea katika njia ya haja kubwa.

Kadhalika pia rangi ya damu iliyotapikwa mara nyingine huweza kutuonyeshea chanzo cha tatizo,

Kwa mfano, mtu akitapika damu nyekundu sana mithili ya kutaka kua nyeusi kwa ujumla inaonyesha kuwa kutapika kwake damu kunatokana na kuwepo kwa hitilafu au tatizo katika sehemu za juu za tumbo (upper gastrointestinal source) kama vile tumboni.


Pia damu nyekundu mpauko mara nyingi huonyesha kuwepo kwa hitilafu au tatizo ndani ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa katika utumbo.


Mpendwa msomaji wakati mwingine rangi ya damu inayotapikwa huweza isionyeshe usahihi wa tatizo linalokusumbua hivyo daktari wako atalazimika Kukufanyia vipimo kwa ajili ya kuchunguza/kubaini tatizo.


CHANZO/VISABABISHI


Kuna vyanzo na sababu nyingi zinazofanya mtu kutapika damu. 

Sababu hizi zinapatikana kutokana na ukubwa na udogo wa tatizo,sababu hizo za kutapika damu ni

°michubuko katika koo la chakula

°kutokwa na damu puani

°vidonda vya tumbo

°maambukizi katika umio la chakula

°saratani ya kongosho

°madhara ya matumizi ya dawa ya vidonge ya aspirin

°uvimbe katika tumbo na koo la chakula

°saratani ya utumbo

°michubuko katika umio na koo kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kifua au kutapika kwa muda mrefu

°saratani ya koo

°magonjwa sugu ya ini (cirrhosis)


DALILI

Dalili kuu ya tatizo hili ni KUTAPIKA DAMU japo pia kuna dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza pamoja na kutapika damu. Dalili hizi ni 

°kuhisi kichefuchefu

°maumivu ya tumbo au kukosa utulivu tumboni

°kutapika yaliyomo katika tumbo hasa vipande vya damu.


VIPIMO NA UCHUNGUZI

Mpendwa msomaji daktari wako ili aweze kujua tatizo hili limesababishwa na nini!

Vipimo kadhaa huweza kufanyika kujua chanzo cha kutapika damu, vipimo vya awali ni muhimu pia kufanyika kama vile, kufahamu wingi wa damu (hemoglobin), kuangalia chembechembe zinazosaidia damu kuganda (platelets).

Kadhalika daktar wako atakuhoji juu ya dalili unazopata. 

Atauliza tatizo la  kutapika damu limekuanza lini hivyo utawajibika kufafanua kiasi cha damu uliyotapika, na ikiwa ilikuwa nyekundu mpauko au ilionekana kama rangi nyekundu sana mithili ya rangi nyeusi,pia utapaswa kumueleza iwapo kuna ugonjwa wowote wa hivi karibuni unaokusumbua, au ikiwa una magonjwa ya muda mrefu yanayokusumbua kama vile vidonda vya tumbo,nk.

Pia utapaswa kumwambia iwapo umemeza dawa aina ya aspirin na ni kiasi gani umemeza.

Kadhalika daktari wako anaweza pia kukuuliza iwapo wewe ni mnywaji wa pombe mara kwa mara.

Maswali yote haya husaidia kujua chanzo cha tatizo,pia vipimo vifuatavyo huweza kutumika ili kubaini chanzo cha tatizo kwa usahihi.

°Endoscopy kipimo ambacho kitatumika kuchunguza sehemu ya juu ndani ya tumbo (GI).

°ultrasound

°MRI

°CT Scan au  x-ray vipimo hivi vinaweza kuonyesha chanzo cha kutapika damu. Picha za vipimo hivi zinaweza kuonyesha michubuko,vidonda na uvimbe ambao ndio sababu ya watu wengi kutapika damu.


MATIBABU

Mpendwa msomaji matibabu ya ugonjwa au tatizo la kutapika damu yanategemea zaidi chanzo chake, kila ugonjwa au tatizo linalosababisha kutapika damu lina matibabu yake tofauti hivyo ni muhimu kwa mgonjwa kwenda hospitali bila kuchelewa. 

Iwapo mgonjwa ametapika damu nyingi kiasi cha kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu basi huhitajika kuwekwa katika chumba maalumu, kuongezewa damu na maji mwilini ili kuokoa maisha yake.

Pia kuna aina kadhaa za matibabu ambazo daktari wako anaweza kukupatia ili kutibu tatizo hili kama vile ÷

MATIBABU YA DAWA 

Dawa zinaweza kutolewa ili kupunguza kiasi cha asidi ambayo huzalishwa tumboni mwako,dawa hizi husaidia iwapo tatizo lako la kutapika damu(hematemesis) husababishwa na kuwepo kwa vidonda tumboni.

OPARESHENI

Kufanyiwa oparesheni kunaweza kuhitajika ikiwa unaendelea kutapika damu nyingi na matibabu mengine uliyopatiwa hayajafanya kazi hivyo oparesheni huweza kutumika kurekebisha michubuko kwenye maeneo ya ndani ya tumbo lako au utumbo.kadhalika hufanyika oparesheni ili kuondoa viuvimbe tumboni.


MATIBABU YA UGONJWA/TATIZO LA KUTAPIKA DAMU (HEMATEMESIS/VOMITING BLOOD) CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kutapika damu (hematemesis/vomiting blood) kwa muda mrefu na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam 
Tutakufanyia uchunguzi  kwa kina pia tutakupatia dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya kabisa.

Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tunatoa huduma ya matibabu ya ushauri na dawa za kuondoa magonjwa mbalimbali katika mwili kama vile matatizo ya figo,mapafu,Moyo,macho, hedhi mbovu,uzazi, magonjwa ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa  na kadhalika karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya wiki nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya matibabu ya tatizo au ugonjwa wa maumivu ya nyayo na kisigino ambapo tatizo hili hujulikana kwa lugha ya kitaalam kama PLANTAR FASCIITIS/POLICEMAN HEELS.

Tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino(Plantar fasciitis /policeman heels)ni moja ya sababu/chanzo kilichozoeleka juu ya tatizo la maumivu ya kisigino hivyo tatizo hili au ugonjwa huu tunaweza kusema kwa maana moja ni maambukizi yanayojumuisha kuvimba kwa bendi nene ya tishu ambayo hupatikana katika nyayo zetu miguuni ambayo inaunganisha mfupa wa kisigino na vidole vya miguu (Plantar fascias).

Kadhalika tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino(Plantar fasciitis) husababisha maumivu makali ambayo mara nyingi hutokea asubuhi pale muhusika anapoamka na anapoweka miguu yake chini na kuanza kupiga hatua zake za kwanza asubuhi maumivu huwa makali sana ambayo hupungua kadri anavyopiga hatua lakini pia hali ya maumivu huweza kurudi baada ya muda mrefu wa kusimama au unaposimama baada ya kukaa.

Tatizo hili  la maumivu makali ya nyayo na kisigino (Plantar fasciitis)huweza kuwapata watu wa rika zote ingawa hutokea zaidi kwa watu wanaofanya mazoezi ya kukimbia sana kadhalika watu ambao ni wenye uzito mkubwa sana na wale ambao huvaa viatu visivyo na visigino na wale wanaovaa viatu vyenye visigino virefu mara kwa mara.


CHANZO/VISABABISHI


Inakadiriwa kuwa wanawake na wanaume walio katika umri wa miaka 40_70 wapo katika hatari kubwa ya kupata tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis), kadhalika wanawake wameonekana ndio wahanga wa kubwa wa tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino ( plantar fasciitis)kuliko wanaume pia wanawake wajawazito nao wamekua wakisumbuliwa na tatizo hili vipindi vya mwisho vya ujauzito.

Lakini pia Mpendwa msomaji ili uweze kuelewa chanzo cha tatizo hili napenda kukujuza kua katika miguu yetu kuna tishu nyembamba ndefu  inayopatikana katika maunganio ya nyayo na kisigino ambayo iko moja kwa moja chini ya miguu yetu,tishu hii inasaidia upinde wa mguu wako na kutusaidia hasa wakati tunapotembea au kusimama.

Lakini Iwapo kutatokea mvutano na msukumo mkubwa juu ya mishipa, mvutano au msukumo huo mkubwa huharibu tishu hiyo na kupelekea kupatikana maambukizi ambayo ndio chanzo cha kupata maumivu makali ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis).

DALILI


Mpendwa msomaji dalili zinazoweza kukujulisha kua una ugonjwa huu wa plantar fasciitis ni kupata maumivu makali chini ya miguu yako hasa eneo la kisigino.

Mgonjwa anapoamka na anapoweka miguu yake chini na kuanza kupiga hatua zake za kwanza asubuhi hupata maumivu makali sana ambayo hupungua kadri anavyopiga hatua lakini pia hali ya maumivu huweza kurudi baada ya muda mrefu wa kusimama au unaposimama baada ya kukaa.

VIPIMO NA UCHUNGUZI

Mpendwa msomaji uchunguzi wa tatizo hili kawaida  hufanywa na daktari ama mtaalamu aliyebobea katika magonjwa ya mifupa hivyo baada ya kumuelezea daktari dalili zinazokusumbua daktari wako atachunguza mguu wako kwa umakini ambapo atalenga kutafuta ishara hizi:

Upinde wa juu au muelekeo wa juu ya kisigino chako

Eneo unalohisi maumivu chini ya mguu wako, iwapo ni mbele tu ya mfupa wa kisigino au la

Kuchunguza kujua maumivu makali unayapata wakati gani hasa hivyo daktari atajaribu kukupa mazoezi ili kuweza kubaini tatizo

Kadhalika daktari wako anaweza kukuagiza vipimo vifuatavyo 

X_Ray na MRI_SCAN 

Ili kujiridhisha kua hakuna chochote kingine kinachosababisha maumivu ya kisigino, kama vile kupasuka kwa mfupa(bone fractured)

MATIBABU

Mpendwa msomaji kuna aina kadhaa za matibabu ambazo daktari wako anaweza kukupatia ili kupunguza maumivu na kupunguza ukubwa wa tatizo. 

Kadhalika Daktari Anaweza kupendekeza kutumia matibabu kadhaa kwa wakati mmoja kama ifuatavyo;

MATIBABU YA DAWA 

Daktari huamua kukupatia dawa za kumeza aina ya Nonsteroidal  anti inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen,naproxen sodium nk kwaajili ya kupambana na maambukizi pamoja na kusaidia kupunguza maumivu katika kisigino.

MATIBABU YA SINDANO

Daktari huamua kukupatia matibabu ya sindano zenye steroids iwapo maumivu ni makali na matibabu ya  dawa nilizoelezea hapo juu kushindwa kupunguza maumivu,

Hivyo daktari wako atakuchoma sindano ya steroid sehemu ambayo unahisi maumivu makali zaidi katika kisigino chako hii itakusaidia kupunguza maumivu kwenye kisigino kwa muda angalau wa mwezi mmoja au zaidi.

MATIBABU YA TIBA MWILI(PHYSICAL THERAPY)

 Ndugu mpendwa msomaji iwapo matibabu ya dawa,sindano na hata mazoezi kushindwa kusaidia kuondoa tatizo hili daktari atakupendekezea uende kwa mtaalamu wa viungo (physical therapist),Ambapo Utajifunza mazoezi ya kunyoosha na kuimarisha tishu zilizopo miguuni na misuli ya miguu ya chini. Kadhalika Mtaalam wako wa mwili anaweza pia kukupatia huduma zingine kama kukufanyia massage,kukushauri kutumia night splint,foot pads, na hata ultrasonography kusaidia kupona kwa muda mrefu.

Lakini pia Iwapo hauonyeshi maendeleo baada ya miezi kadhaa, daktari wako anaweza kupendekeza utaratibu mwingine kama vile Shockwave therapy, tenex na hata kushauri ufanyiwe upasuaji.

OPARESHENI

Daktari hufikia maamuzi ya kukufanyia upasuaji mara baada ya njia zote zilizotumika kushindwa kukusaidia yani kufanyiwa upasuaji kwa tatizo hili kawaida ni njia ya mwisho ikiwa una maumivu makali au jeraha la muda mrefu ambalo matibabu mengine hayakusaidia.

NAMNA UNAVYOWEZA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA UKUBWA WA TATIZO LA MAUMIVU katika nyayo na visigino UKIWA NYUMBANI

Mpendwa msomaji wetu kuna njia nyingi anazoweza kuzitumia mgonjwa kujitibia au kupunguza ukubwa wa tatizo hili akiwa nyumbani lakini pia licha ya kuwa baadhi ya njia nimeziorodhesha hapa chini zimewasaidia wengi ila unahitajika kupata ushauri na vipimo kutoka kwa mtaalamu wa afya ili kujiridhisha juu ya tatizo hili kabla hujatumia njia yoyote ili akupatie ushauri ni njia gani inaweza ikakufaa bila ya kukuathiri iwapo utakua una matatizo mengine tofauti na tatizo hili.
Baadhi ya njia zinazotumika kupambana na tatizo hili ni;

1.PUNGUZA UZITO

Mpendwa msomaji napenda ufahamu kwamba Mtu kua na uzito mkubwa ni miongoni mwa vyanzo vya kupata tatizo hili kwani kua na uzito mkubwa huweka shinikizo au uzito zaidi kwenye tishu zilizopo miguuni. Hivyo Ikiwa una uzito mkubwa jitahidi upunguze japo kidogo ili kusaidia kupunguza shinikizo la uzito mguuni.
 Unaweza kuwasiliana na daktari wako ili akupatie mpango au ratiba ya milo inayozingatia lishe bora na mazoezi ya kawaida yatakayokusaidia kupambana na tatizo hili.

2.PUMZIKA

Mpendwa msomaji wakati mwingine maumivu ya nyayo na visigino ni ishara kwamba miguu yako inahitaji kupumzika tu, haswa ikiwa unafanya shughuli ngumu mara kwa mara kama vile kusimama kwa muda mrefu, kukimbia,kuvaa viatu virefu mara kwa mara hivyo basi unashauriwa kujitahidi Kujipatia mapumziko ya miguu yako kwa siku chache ili kusaidia kupunguza uvimbe na kuiruhusu tishu na misuli ya miguu kupumzika.

3.VAA VIATU VYENYE KISIGINO KIFUPI

Imeonekana kua Watu wanaovaa Viatu visivyo na visigino na viatu vyenye visigino virefu husumbuliwa sana na hili tatizo hivyo tunashauriwa kuvaa viatu vyenye visigino vifupi ambavyo vinatoa msaada mzuri kwa misuli ya miguu wakati tunapotembea au kusimama.

4.VAA PEDI ZA MIGUU

Mpendwa msomaji unaweza kununua/kuvaa pedi za miguu ambazo husaidia kupunguza maumivu na maambukizi  miguuni.
Pedi hizi zinapatikana katika baadhi ya maduka ya dawa
Hata ofisini kwangu unaweza kuzipata tuwasiliane kwa namba zifuatazo ujipatie pedi hizo iwapo utahitaji
+255746465095/+255657041420

5.INYOOSHE/KUKANDA NYAYO

Mpendwa msomaji wakati mwingine ili kutuliza au kupunguza maumivu yanayosababishwa na kuvimba kwa tishu, tunatakiwa kunyoosha au kujikanda na mafuta ya mzaituni kwa upole au taratibu.
Mara baada ya kumaliza shughuli zako usiku kabla hujalala paka mafuta katika nyayo zako na umuombe mkeo/rafiki/mumeo/ndugu akukande kwa muda wa dakika 15 kuanzia kwenye vidole,nyayoni akimalizia taratibu katika visigino hii husaidia hasa kuondoa maumivu na kuponya maradhi mengi na hata kuondoa uchovu wa mwili.

MATIBABU YA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI YA NYAYO NA KISIGINO (PLANTAR FASCIITIS/POLICEMAN HEELS)  CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kupata maumivu makali chini ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis/policeman heels) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam 
Tutakufanyia uchunguzi  kwa kina pia tutakupatia dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya kabisa.

Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tunatoa huduma ya matibabu ya ushauri na dawa za kuondoa magonjwa mbalimbali katika mwili kama vile matatizo ya hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na kadhalika karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )


CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA CHUNJUA/vijiuvimbe/VIGWARU/VIOTEO VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI(PLANTAR WARTS/FOOT WARTS)


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya siku nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya matibabu ya tatizo la chunjua/vijiuvimbe/vigwaru/vioteo vinavyoota kwenye visigino/nyayo na sehemu za miguuni.

JE, TATIZO LA CHUNJUA/VIGWARU/VIOTEO VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI (PLANTAR WARTS/FOOT WARTS) ni Nini?

Ni viuvimbe/vigwaru/warts/vioteo vidogovidogo vinavyotokea kwenye kisigino au sehemu ambazo zinabeba uzito za kwenye miguu. Mgandamizo kwenye maeneo hayo huweza kusababisha vichunjua hivyo vya miguuni(plantar warts) kuota kuelekea ndani, chini ya tabaka nene la ngozi (callus).
Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya HPV(Human papilloma Viruses),Kirusi huyu huingia mwilini kupitia sehemu ndogo ulizojikata, au sehemu nyingine dhaifu za maeneo ya chini ya mguu.
Kwa maana hiyo ugonjwa huu unasababishwa na virusi hivyo anapoingia kwenye tabaka la juu la ngozi ya kwenye unyayo kupitia vijijeraha vidogo au maeneo mengine yaliyo dhaifu yaliyo maeneo ya chini ya mguu.

Kadhalika virusi hivi hupatikana kwa wingi, na kuna aina tofauti zaidi ya 100 ya virusi hawa Lakini ni aina chache tu ambazo zinaweza kuleta chunjua kwenye mguu. Aina nyingine zinaweza kuleta chunjua kwenye maeneo mengine ya ngozi au kwenye utando telezi.

Pia ifahamke kutokana na kua kila mtu ana kinga zake za mwili zenye uwezo tofauti wa kupambana na Virusi basi  Si kila mtu atakayegusana na kirusi huyu atapata chunjua. Hata watu wa familia moja wana uwezo wa kustahimili kirusi huyu kwa viwango tofauti.

Kadhalika virusi  wanaoeneza chunjua za miguuni (plantar warts) ni wenye kuambukiza japo kua hawaambukizi kirahisi. Kwa hiyo chunjua hizi haziambukizi kwa kugusana.
 Lakini wanapenda kuishi kwenye mazingira ya vuguvugu, yenye unyevu. Kwa hiyo unaweza kumpata kirusi huyu kwa kutembea peku kwenye mabwawa ya kuogelea,kuvaliana soksi au viatu na kuchangia taulo na muathirika wa tatizo hili,kirusi akipenya sehemu moja, anaweza kuenea hadi maeneo mengine na kusababisha chunjua.

CHANZO/VISABABISHI

Mpendwa msomaji hapo juu nimeelezea kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi vinavyoitwa HUMAN PAPILOMA VIRUSES (HPV)
Kadhalika kuna aina 120 za virusi hivi vya human papiloma viruses Ila kuna aina chache ambazo husababisha chunjua za miguuni,aina nyingine husababisha chunjua sehem nyingine tofauti za mwili.
Aina za HPV 57, 27 na 1a zimeonekana zaidi kusababisha chunjua za miguuni.
Mtu hupata maambukizi ya virusi hawa kwa njia ya ngozi kwa kupitia magusano ya moja kwa moja.
 Kadhalika imeonekana kuwa maambukizi huingia katika ngozi kutoka maeneo yanayoweza kuenezwa kwa virusi hivi kama katika mabwawa ya kuogelea ya jamii.
Mara baada ya mtu kuambukizwa virusi vya HPV, maazimio ya kusambaza maambukizi mwilini hutegemea maendeleo ya lymphocyte za kinga ambazo huharibu seli zilizoambukizwa na virusi. 
Lakini pia kuna chanjo zinazopatikana kwa ajili ya  kujilinda dhidi ya maambukizo ya virusi hawa wa HPV wanaosababisha vinyama sehemu za siri lakini hakuna chanjo dhidi ya HPV zinazosababisha vichunjua miguuni.
Hivyo ni wajibu wetu kujiepusha kupata maambukizi na hata kuepusha wengine kuambukizwa kwakua ugonjwa huu huonekana katika makundi yote ya umri ingawa huathiri sana vijana kuliko wazee

DALILI


Mpendwa msomaji wetu dalili zinazoweza kukujulisha kua unasumbuliwa na tatizo hili ni kupata maumivu makali ya miguu kutokana na shinikizo kwenye miguu yako wakati unatembea au kusimama.
Kadhalika utaona sehemu ya mviringo au duara kwenye ngozi ama kioteo chenye gamba gumu.
Kinyama au kioteo kinaweza kuonekana kuwa na rangi ya manjano au kutu, au hata kuwa na madoa madogo meusi katikati.
Kukosa utulivu kwa kuhisi kutekenywatekenywa ndani ya kichunjua  pale unapokanyaga chini au kutembea.


VIpimo na uchunguzi


Mpendwa msomaji uchunguzi wa tatizo hili kawaida  hufanywa na daktari ama mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa kutizama na kuchunguza kwa umakini kugungua kama kweli  ni chunjua(warts)au  ni tatizo lingine. Iwapo kutakua na mashaka daktari anaweza kutuma sampuli ya tishu ya chunjua(warts)kwa mtaalam wa uchunguzi ili kuweza kujiridhisha.
Mathalani Daktari anaweza kuhisi ni matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha kuonekana sawa na tatizo la chunjua miguuni , kama vile calluses, corn's au black heels(ruptured capillaries).

MATIBAbu

Mpendwa msomaji wetu licha ya kuwepo kwa matibabu ya chunjua za miguuni (plantar warts),tatizo hili mara nyingine huondoka lenyewe bila matibabu. Karibu asilimia 65-78% ya watu wenye tatizo hili hupona bila ya kutumia dawa ndani ya miaka 2.
Kadhalika  baada ya vipimo na uchunguzi kugundulika ugonjwa huu,daktari wako anaweza kukuchagulia matibabu kulingana na hali uliyonayo.
Matibabu haya yapo ya aina tofauti kama ifuatavyo

prescription creams

Daktari anaweza kukuagiza kutumia dawa ya kupaka yenye asidi ya salicylic kutibu chunjua za miguuni, Kemikali hii ni chaguo la kwanza la matibabu kwa kuondoa chunjua za miguuni (plantar warts)

Waathirika wa tatizo hili wameonesha kupona kwa kutumia dawa ya asidi ya salicylic kwa muda mchache.

 Cryotherapy


Daktari huweza pia kushauri njia hii ya matibabu ambayo hugandisha chunjua kwa kutumia naitrojeni ya maji (liquid nitrogen). Ni njia bora sana kwa sababu imetoa matokea mengi mazuri ikiwa na madhara machache sana tofauti na matibabu mengine licha ya kuwa na maumivu makali lakini pia matibabu haya hayafai kutumika kwa watoto.

Laser treatment

Daktari huamua kutumia njia hii ya matibabu ambayo hutumika kuondoa chunjua  zilizoenea au zinazojirudirudia. Mionzi ya laser huharibu kabisa uvimbe  uliotokana na HPV hivyo kuondoa uwezekano wa viruses hivi kuendelea kuwepo
Matibabu haya ni yenye ufanisi kwa asilimia kubwa ingawaje gharama yake ni bei kubwa, muda mrefu wa matibabu, na kuacha makovu.

Immunotherapy

Njia hii ya matibabu hutumika Mara ambapo njia nyingine za matibabu zimeshindwa kufanya kazi ipaswavyo.
Tiba hii (immunotherapy)hufanya kazi ya kuchochea mfumo wa kinga ya mwili kupigana na virusi vya HPV ambavyo vinaendelea kusambaza ugonjwa ndani ya mwili

Fluorouracil (5-FU) ni dawa ya Kemikali yenye matumizi mengi ambayo pia kinyume na matumizi yaliyowekwa na mamlaka ya dawa na chakula  watu wanaweza  kutumia kupaka kama cream kwa chunjua za miguuni.
Kadhalika  Jumuiya ya matibabu haipendekezi  matumizi ya dawa hii kwa wanawake ambao ni wajawazito au wanaopanga kuwa wajawazito siku za karibuni.
Watu wanaweza pia kuchukua dawa ya kumeza kama vile cimetidine, kinyume na matumizi(off labels)kuongeza mwitikio wa kinga mwilini, ingawa kuna ukosefu wa ushahidi wa kutosha.
Watafiti wengine wamependekeza kwamba matumizi ya vidonge vya zinc husaidia sana kuongezeka kwa kinga mwilini na hivyo husaidia waathirika wa vichunjua(warts) kupona haraka.

NAMNA UNAVYOWEZA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA CHUNJUA UKIWA NYUMBANI

Mpendwa msomaji wetu kuna njia nyingi anazoweza kuzitumia mgonjwa kujitibia tatizo hili akiwa nyumbani lakini pia licha ya kuwa baadhi ya njia ninameziorodhesha hapa chini zimewasaidia wengi ila unahitajika kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya kabla hujatumia njia yoyote ili akupatie ushauri ni njia gani inaweza ikakufaa bila ya kukuathiri iwapo utakua una maradhi mengine kama vile kisukari,matatizo ya mzio nk.

1.KITUNGUU SAUMU, BAKINGS SODAS NA LIMAO

Kitunguu saumu kimekua kikitumika katika matibabu kwa muda mrefu sana,kutokana na uwezo wake wa kupambana na aina tofauti za magonjwa.
Ili kuweza kutibu vichunjua  menya vitunguu saumu punje 10,kisage kiwe laini changanya na  baking soda kijiko kimoja kisha changanya na limao.Paka mchanganyiko huu kwenye chunjua pia ukiweza funga na  plasta,kaa kwa masaa mawili hadi matatu osha. Paka mara 3 kwa siku. Ni vizuri usiku ukilala nayo. Baada ya muda mfupi utapata matokeo mazuri.

2.SIKI YA TUFAHA NA VITUNGUU MAJI (APPLE CIDER VINEGAR AND ONIONS)
Siki ya tufaha (Apple cider vinegar) imejizoelea umaarufu kutokana na uwezo wake wa kutibu magonjwa mengi tofauti.
Hapa unatakiwa kuchukua vitunguu maji viwili kata vipande weka kwenye bakuli ,changanya na apple cider kisha viache vilowane usiku kucha,asubuhi chukua vitunguu bandika kwenye visunzua kisha funga vizuri na plasta visitoke acha kwa masaa 4 hadi matano.Fanya hivi kila siku kwa muda wa wiki moja utajionea utofauti.

3.ASPIRIN
Vidonge aina ya aspirin ambayo ni dawa maarufu humezwa Kwa ajili ya kutuliza maumivu, hapa hutumika kinyume na matumizi (off labels)huimezi bali unaiponda upate  unga kisha changanya na matone ya mafuta ya  maji ilainike.paka kwenye chunjua Mara tatu hadi nne kwa siku. Baada ya wiki utajifurahia na kuona matokeo mazuri

4.RANGI YA KUCHA

Unaweza kushangaa juu ya jambo hili kwakua imezoeleka rangi ya kucha ni kwa ajili ya urembo pekee wa
kucha,jambo ambalo si la kweli kwani hapa rangi inafanya kazi nyingine ya kuondoa chunjua miguuni.
Unachotakiwa ni kupaka rangi kwenye chunjua mara tatu hadi nne kwa siku.
usiku unashauriwa kulala nayo na ubandue asubuhi.Ukifanya hivi kila siku mfululizo kwa muda wa wikimoja tuu utapata matokeo mazuri y a kukufurahisha

5.GANDA LA NDIZI MBIVU

Unaweza ukajiuliza "GANDA LA NDIZI LINAWEZAJE KUONDOA CHUNJUA"
Jibu ni rahisi chukua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na usugue kwenye chunjua Mara nyingi uwezavyo kwa siku .ili upate matokeo mazuri bandika plasta  na uiache kwa muda mrefu.

NOTED
Matibabu ya nyumbani huweza kuchukua muda mrefu kuleta matokeo,hivyo inashauriwa kuwasiliana na daktari wako kwa msaada zaidi wa matibabu.
Pia
Inashauriwa wote ambao ni waathirika wa tatizo hili kudhibiti maambukizi  katika sehemu zingine za mwili na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi haya ya virusi vya HPV kwa kufanya yafuatayo
1)kutochangia mataulo,viatu na soksi
2) kutochangia viwembe
3)kutogusa vichunjua kwa mkono ili kuzuia kuhamisha virusi kutoka sehemu moja ya mwili kwenda sehem nyingine
4) kuosha mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara

MATIBABU YA TATIZO LA CHUNJUA VIGWARU/MASUNDOSUNDO/VIJINYAMA VIDOGOVIDOGO VINAVYOOTA KWENYE VISIGINO/NYAYO NA SEHEMU ZA MIGUUNI(PLANTAR WARTS/FOOT WARTS)CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili la kutokewa na chunjua/vinyama vidogovidogo vinavyotokea katika ngozi sehemu mbalimbali za mwili na hata miguuni (genitals warts and plantar warts) na umeshafanya matibabu kadhaa ila bado hujapata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam 
Tutakufanyia uchunguzi wa kujua ni aina gani ya chunjua ulizonazo pia tutakupatia dawa stahiki zenye uwezo wa kukuponya pasipo kukuunguza
Pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la vinyama sehemu mbalimbali katika mwili,tatizo la hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
 chanzo na matibABU YA TATIZO LA mtu mzima kukojoA KITANDani (ADULTS NOCTURNAL ENURESIS)


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya week nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya tatizo la mtu  mzima kukojoa kitandani ambapo kwa lugha ya kingereza na kitaalamu tunasema (adults nocturnal bedwetting/enuresis)

Je,tatizo la mtu mzima kukojoa kitandani(adults nocturnal ENURESIS) NI Nini?

Hili ni tatizo linaowasumbua watu wengi walio katika umri ambao tayari wana uwezo wa kuzuia mkojo,tatizo hili hutokea kwa mtu huyo ambaye tayari yupo katika umri wa kuweza kujizuia mkojo ila anakua bado anaendelea kukojoa kitandani au kwenye nguo.
Hivyo tunaweza kusema hili ni  tatizo la kushindwa kuzuia mkojo wakati wa mchana au usiku na linalotokea katika umri wa miaka mitano au zaidi.

Imezoeleka watoto wengi wanaacha kukojoa kitandani usiku au mchana katika umri wa miaka mitatu_minne,
Kadhalika asilimia 10 hadi 15 ya watoto wa miaka mitano wanaoendelea kujikojolea kitandani wengi wao ni wavulana ambao ni asilimia 7 kuliko wasichana ambao wenyewe ni asilimia 3.
Pia katika umri wa miaka 15 wanaoendelea kujikojolea kitandani ni asilimia 2 Hadi 3 tu, na asilimia 3 katika umri wa miaka 18 na kuendelea
 Kwahiyo tatizo la kujikojolea ni ugonjwa wa akili unaotokana na utofauti katika ukuaji wa fiziologia ya kuzuia mkojo.

Mkojo unapo hifadhiwa katika kibofu cha mkojo, kibofu kinatanuka kama puto. Katika sehemu za neva za kutanua kuta za kibofu cha mkojo zinapeleka ishara ya kuzuia mkojo katika akili.
Hii hutokea katika sehemu ya ubongo inayohusika na matendo yasiyo ya hiari. Kama ubongo wa mtoto haujapata ishara hii, au ukishindwa kujua maana ya hiyo ishara, hatua ya makusudi ya kuzuia mkojo haitafanyika hivyo mtu hushindwa kupata uwezo wa kuxuik mkojo.
Hali hii mara nyingi husababishwa na kuchelewa kwa ukuaji wa kibiologia wa utendaji kazi wa kuzuia mkojo na Ukuaji wa kijinsia unaweza kusababishwa na;

1} Kushindwa kwa akili kutambua ishara kutoka kwenye kibofu cha mkojo,
2} Ujazo mdogo wa kibofu cha mkojo; au 3} Usingizi mzito.
Kwa sasa tafiti zinaonyesha kwamba watu wanaokojoa kitandani ni wagumu kuamka kutoka usingizini kuliko ambao hawana tatizo hilo.
Ni muhimu kutambua kwamba watu hawa hawajikojolei kwa makusudi na kawaida huona aibu kwa sababu hiyo hivyo ukiwa ndugu au mzazi au mpenzi wa mwenye tatizo hili haupaswi kumdhalilisha kwa kumwaibisha au kumtenga bali unatakiwa kumsaidia kupata ufumbuzi wa tatizo Hili.

Kadhalika tatizo Hili la kujikojolea limegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Yani
1)Primary enuresis
Aina hii ni pale mtu anaposhindwa kuwa na uwezo wa kuzuia mkojo tangia utotoni kwake,

2)Secondary enuresis
Aina hii ni pale mtu anaweza kujizuia kujikojolea kwa miezi sita au zaidi, halafu anaanza kujikojolea tena.
Mpendwa msomaji katika aina hiyo ya  kwanza yani PRIMARY ENURESIS hili ni tatizo la kurithi na huwapata watu wa familia moja. Tafiti kutoka somo la vinasaba inaonyesha kwamba ikiwa wazazi wote walikuwa wanakojoa kitandani, asilimia 77 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano na ikiwa mzazi mmoja alikuwa na tatizo hili, asilimia 44 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano. Na ikiwa wazazi wote hawakuwa na tatizo hili la kukojoa kitandani, asilimia 15 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano.

Kadhalika tatizo hili limegawanyika katika sehemu mbili.
1. Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku (NOCTURNAL ENURESIS) na lile la mtu kujikojolea wakati wa mchana (DIURNAL ENURESIS). Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku huonekana zaidi kwa watoto wa kiume na lile la kujikojolea mchana mara nyingi huwa kwa wasichana.


Chanzo Cha tatizo

Mpendwa msomaji utafiti umeonyesha kua kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili la kukojoa kitandani na miongoni mwa sababu hizo ni

1)OVERACTIVE BLADDER (OAB)
Hili ni tatizo la kibofu cha mkojo kuruhusu mkojo kutoka kwa ghafla bila ya muhusika kuwa na utayari na hivyo hukosa uwezo wa kujizuia kujikojolea,hali hii husababisha mtu kuonekana amejikojolea pasipo kujitambua.

2) STRESS (Msongo mkali wa mawazo )
Kwa upande mwingine tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa limesababiswa na matatizo ya hisia au ya kisaikolojia na msongo wa mawazo(stress).
Mara nyingi hii hutokea utotoni hasa pale mtoto anapozaliwa mtoto mwenzie yani mdogo wake, ugomvi wa wazazi, msongo anaoupata mtoto anapoanza shule au kutengana na wazazi. Matatizo kama haya na mengine yanayofanana yanaweza kumsababishia mtu kupata matatizo ya kihisia na kusababisha tatizo la kukojoa kitandani kuanza au kuzidi Hadi ukubwani.

3)MADAWA
Kuna baadhi ya dawa husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea dawa hizo ni za usingizi na dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya akili mfano wa dawa hizo ni
Clozapine,cariprazine, risperidone etc

4) TATIZO LA KUKOSA HAJA KUBWA (CONSTIPATION)

5) KISUKARI (DIABETES)

6) MATATIZO YA FIGO (KIDNEY DISEASES)

7)TEZI DUME (ENLARGED PROSTATE)
8)MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(URINARY TRACT INFECTION)
9)TATIZO LA KUFUNGWA KWA NJIA ZA HEWA WAKATI WA USINGIZI (OBSTRUCTIVE SLEEP APNEA)
10) KIBOFU CHA MKOJO KUWA KIDOGO(SMALL BLADDER)

VIPIMO NA uchuNGUZI




Mpendwa msomaji wetu iwapo una tatizo hili usiwe na dhana mbaya za kuhisi una mashetani  au majini fahamu hili ni tatizo lenye kutibika hospitalini hivyo achana na fikra hasi haraka fika hospitali,daktari wako atakufanyia uchunguzi na kukuliza maswali juu ya dalili zako na historia ya afya yako.
Unashauriwa kuwa na diary utakayoandika majibu ya maswali utakayoulizwa na daktari wako ili kusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo
Maswali utakayoulizwa ni ÷

Ni mara ngapi na kwa wakati gani huwa unajikojolea (je,ni usiku au mchana)?

Kiasi gani mkojo hukutoka (mwingi au kidogo)?

Ni kiasi gani cha vinywaji ulikunywa kabla ya kupanda kitandani?

Dalili zingine zozote ambazo umekuwa nazo(unahisi maumivu baada ya kutokwa na mkojo)?

Iwapo daktari wako atahitaji zaidi Kukufanyia uchunguzi ataagiza vipimo vifuatavyo÷

Urine culture and urine analysis: Vipimo hivi hutumika kuangalia maambukizi, damu isiyohitajika na vitu vingine kwenye mkojo.

Blood tests : kipimo hiki cha damu hutumika kuangalia figo na tezi, kiwango cha cholesterol iliyopo katika damu na iwapo kama Kuna shida ya upungufu wa damu au ugonjwa wa kisukari na homoni.

Bladder scans: hiki ni kipimo cha ultrasound ambacho mgonjwa atatakiwa kupima ili tujue ni kiwango  gani cha mkojo hubakia katika kibofu mara baada ya kukojoa.

Urodynamic tests: kipimo hiki kitahitajika kupimwa ili kuangalia au kuona jinsi sehemu ya chini ya mkojo huhifadhi na kutoa mkojo kiwango gani

Cystoscopy: kipimo hiki pia kitahitajika kuhitimisha uchunguzi ambapo daktari ataingiza bomba nyembamba na lens ndogo ndani ya kibofu cha mkojo ili kuangalia iwapo kuna dalili ya uvimbe,kansa na matatizo mengine.

MATIBABU 


Mpendwa msomaji napenda kuhitimisha somo langu hili kwa kukusihi iwapo una hili tatizo au ndugu yako analo tafadhal fahamu kuwa tatizo hili lina matibabu mengi ambayo matibabu haya hutofautiana kwani mengine hufanya kazi vizuri zaidi ya matibabu mengine.
Kadhalika matibabu ya kukojoa kitandani kwa watu wazima yamegawanyika  katika aina kuu tatu:

1) MATIBABU YANAYOHUSU MFUMO WA MAISHA(LIFESTYLE TREATMENT)


Aina hii ya matibabu inajumuisha kubadilisha ama kudhibiti baadhi ya mambo yaliyopo katika maisha ya muhusika ili kuweza kupona  tatizo hili,miongoni mwa hayo mambo ni

°Kudhibiti utumiaji wa vinywaji:Unashauriwa kupunguza unywaji wa vinywaji vyako wakati wa mchana na jioni.
Lakini pia unaruhusiwa kunywa vinywaji vingi zaidi wakati wa asubuhi ya mapema wakati unaweza kwenda chooni kwa urahisi, unatakiwa kuepuka matumizi ya vinywaji wakati wa jioni.

°Kuwa na ratiba ya kuamka usiku: unashauriwa kuweka kengele katikati ya usiku itakayoweza kukusaidia Kuamka mara moja au mara mbili kwa usiku ili kwenda kukojoa chooni hata kama Hauna mkojo hii itasaidia kujenga mazoea ya kuweza kushtuka unapohisi mkojo

°Kuwa na ratiba ya kwenda chooni mara kwa mara wakati wa mchana; hii itasaidia kuwa sehemu ya utaratibu wako. Hata ukilala wakati wa mchana weka kengele itakayokuamsha ili kuweza kuamka na kwenda kukojoa  lakini pia hakikisha unakojoa kabla ya kulala.

°Epuka vitu vinavyofanya kibofu cha mkojo kujaa kwa haraka; unapaswa kuacha matumizi ya kahawa,pombe,vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi kwani husababisha kibofu chako cha mkojo kujaa na kusababisha mkojo wa mara kwa mara.

2) MATIBABU YANAYOHUSISHA DAWA (MEDICINE)

Aina hii ya matibabu imegawanyika katika sehemu nne kulingana na sababu au chanzo cha tatizo kilichogunduliwa ambapo ni
°dawa za antibiotics hizi hutolewa kutibu maambukizo ya njia ya mkojo(urinary tract infection)

°dawa za anticholinergic hizi hutolewa kwa ajili ya kutibu na kutuliza tatizo la misuli ya kibofu cha kibofu

°dawa za desmopressin acetate hizi hutolewa kwa ajili ya kuongeza viwango vya ADH ili figo zako ziache kutoa mkojo mwingi usiku

°dawa za 5-alpha reductase inhibitor hizi hutolewa kwa ajili ya tatizo la tezi dume na hutumika pia kutibu tatizo hili la kukojoa kitandani pia
Mfano wa dawa hizo ni finasteride


3) MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI (SURGERY)

Aina hii ya matibabu huamuliwa kufanyika kutokana na ukubwa wa tatizo na chanzo au kisababishi cha tatizo hili kuwa kubwa

1)SACRAL NEUROMODULATION THERAPY


Hii ni moja wapo ya chaguzi kadhaa za matibabu ya oparesheni  kwa ajili ya kutibu tatizo la kukojoa kitandani kwa mtu mzima ambapo tatizo hilo limetokana na kuwepo kwa matatizo katika kibofu cha mkojo kushindwa kudhibiti au kuzuia mkojo kutoka (overactive bladder)

2) AUGMENTATION CYSTOPLASTY


Haya ni matibabu ya upasuaji katika kibofu cha mkojo ambapo upasuaji hufanyika kwa ajili ya Kuongeza ukubwa wa kibofu cha mkojo kutokana na tatizo la kibofu kuwa kidogo (Small bladder)
Lengo la utaratibu huu ni kuongeza ukubwa na uwezo wa kibofu cha mkojo

3) PELVIC ORGANS PROLAPSE FIX

Haya ni matibabu yanayoweza kuhitajika ikiwa kuna viungo vya uzazi vya kike ambavyo havipo kwenye nafasi iliyokusudiwa nikimaanisha viungo hivyo kutoka mahali na kushinikiza  uzito wote katika kibofu cha mkojo.

4) DETRUSOR MYECTOMY


Huu ni upasuaji ambao unajumuisha kuondoa sehemu au safu zote za nje za misuli ambazo huzunguka kibofu cha mkojo. Hii inalenga kupunguza kiwango na nguvu ya msukumo/shinikizo katika kibofu cha mkojo ambayo husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea pasipo ridhaa yake

NOTED
Mpendwa msomaji wetu ni muhimu kukumbuka kuwa waathirika wenye tatizo hili wataacha kukojoa kadiri wanavyopata matibabu  na ikiwa utamsaidia inavyotakiwa, utamsaidia kuacha mapema zaidi kujikojolea kitandani.
Dharau,kejeli,masimango,kumpiga, au kumchapa mtu mwenye tatizo hili awe mkubwa au mdogo unamuongezea tatizo na kufanya tatizo lizidi au kuchelewa kuisha.
 Ni muhimu sana kumstiri,kutomtisha au kumsema vibaya mwenye tatizo hili. Kufanya hivyo sio tu kama kutazidisha tatizo bali pia humfanya kuwa katika hatari ya kupata matatizo mengine ya kisaikolojia kwa wakati huo na hata baadae katika maisha yake.
Ili kumsaidia mtu mwenye tatizo hili ni muhimu na inashauriwa kumhakikishia na kumfariji  kwa kumuonesha kua anapitia hatua ya kawaida ya maradhi na kuwa kadiri siku zinapita tatizo hilo litaisha. Hii itamsaidia mgonjwa kutopata msongo(stress) na kuusaidia mwili kufanya kazi yake vizuri ambayo hatimaye humsaidia kuondokana na tatizo hili mapema zaidi.


MATIBABU YA TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI (ADULTS NOCTURNAL BEDWETTING/ENURESIS )NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER



Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la kukojoa kitandani ( adults nocturnal bedwetting/enuresis) na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia huduma na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako


Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud ) 

Copyright © 2017 Green health consultation centre