FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI ( ADULTS NOCTURNAL ENURESIS)

 chanzo na matibABU YA TATIZO LA mtu mzima kukojoA KITANDani (ADULTS NOCTURNAL ENURESIS)


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,pole kwa majukumu ya week nzima napenda kukukaribisha kwa mara nyingine tena katika ukurasa wangu huu upate kujifunza juu ya tatizo la mtu  mzima kukojoa kitandani ambapo kwa lugha ya kingereza na kitaalamu tunasema (adults nocturnal bedwetting/enuresis)

Je,tatizo la mtu mzima kukojoa kitandani(adults nocturnal ENURESIS) NI Nini?

Hili ni tatizo linaowasumbua watu wengi walio katika umri ambao tayari wana uwezo wa kuzuia mkojo,tatizo hili hutokea kwa mtu huyo ambaye tayari yupo katika umri wa kuweza kujizuia mkojo ila anakua bado anaendelea kukojoa kitandani au kwenye nguo.
Hivyo tunaweza kusema hili ni  tatizo la kushindwa kuzuia mkojo wakati wa mchana au usiku na linalotokea katika umri wa miaka mitano au zaidi.

Imezoeleka watoto wengi wanaacha kukojoa kitandani usiku au mchana katika umri wa miaka mitatu_minne,
Kadhalika asilimia 10 hadi 15 ya watoto wa miaka mitano wanaoendelea kujikojolea kitandani wengi wao ni wavulana ambao ni asilimia 7 kuliko wasichana ambao wenyewe ni asilimia 3.
Pia katika umri wa miaka 15 wanaoendelea kujikojolea kitandani ni asilimia 2 Hadi 3 tu, na asilimia 3 katika umri wa miaka 18 na kuendelea
 Kwahiyo tatizo la kujikojolea ni ugonjwa wa akili unaotokana na utofauti katika ukuaji wa fiziologia ya kuzuia mkojo.

Mkojo unapo hifadhiwa katika kibofu cha mkojo, kibofu kinatanuka kama puto. Katika sehemu za neva za kutanua kuta za kibofu cha mkojo zinapeleka ishara ya kuzuia mkojo katika akili.
Hii hutokea katika sehemu ya ubongo inayohusika na matendo yasiyo ya hiari. Kama ubongo wa mtoto haujapata ishara hii, au ukishindwa kujua maana ya hiyo ishara, hatua ya makusudi ya kuzuia mkojo haitafanyika hivyo mtu hushindwa kupata uwezo wa kuxuik mkojo.
Hali hii mara nyingi husababishwa na kuchelewa kwa ukuaji wa kibiologia wa utendaji kazi wa kuzuia mkojo na Ukuaji wa kijinsia unaweza kusababishwa na;

1} Kushindwa kwa akili kutambua ishara kutoka kwenye kibofu cha mkojo,
2} Ujazo mdogo wa kibofu cha mkojo; au 3} Usingizi mzito.
Kwa sasa tafiti zinaonyesha kwamba watu wanaokojoa kitandani ni wagumu kuamka kutoka usingizini kuliko ambao hawana tatizo hilo.
Ni muhimu kutambua kwamba watu hawa hawajikojolei kwa makusudi na kawaida huona aibu kwa sababu hiyo hivyo ukiwa ndugu au mzazi au mpenzi wa mwenye tatizo hili haupaswi kumdhalilisha kwa kumwaibisha au kumtenga bali unatakiwa kumsaidia kupata ufumbuzi wa tatizo Hili.

Kadhalika tatizo Hili la kujikojolea limegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Yani
1)Primary enuresis
Aina hii ni pale mtu anaposhindwa kuwa na uwezo wa kuzuia mkojo tangia utotoni kwake,

2)Secondary enuresis
Aina hii ni pale mtu anaweza kujizuia kujikojolea kwa miezi sita au zaidi, halafu anaanza kujikojolea tena.
Mpendwa msomaji katika aina hiyo ya  kwanza yani PRIMARY ENURESIS hili ni tatizo la kurithi na huwapata watu wa familia moja. Tafiti kutoka somo la vinasaba inaonyesha kwamba ikiwa wazazi wote walikuwa wanakojoa kitandani, asilimia 77 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano na ikiwa mzazi mmoja alikuwa na tatizo hili, asilimia 44 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano. Na ikiwa wazazi wote hawakuwa na tatizo hili la kukojoa kitandani, asilimia 15 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano.

Kadhalika tatizo hili limegawanyika katika sehemu mbili.
1. Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku (NOCTURNAL ENURESIS) na lile la mtu kujikojolea wakati wa mchana (DIURNAL ENURESIS). Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku huonekana zaidi kwa watoto wa kiume na lile la kujikojolea mchana mara nyingi huwa kwa wasichana.


Chanzo Cha tatizo

Mpendwa msomaji utafiti umeonyesha kua kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili la kukojoa kitandani na miongoni mwa sababu hizo ni

1)OVERACTIVE BLADDER (OAB)
Hili ni tatizo la kibofu cha mkojo kuruhusu mkojo kutoka kwa ghafla bila ya muhusika kuwa na utayari na hivyo hukosa uwezo wa kujizuia kujikojolea,hali hii husababisha mtu kuonekana amejikojolea pasipo kujitambua.

2) STRESS (Msongo mkali wa mawazo )
Kwa upande mwingine tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa limesababiswa na matatizo ya hisia au ya kisaikolojia na msongo wa mawazo(stress).
Mara nyingi hii hutokea utotoni hasa pale mtoto anapozaliwa mtoto mwenzie yani mdogo wake, ugomvi wa wazazi, msongo anaoupata mtoto anapoanza shule au kutengana na wazazi. Matatizo kama haya na mengine yanayofanana yanaweza kumsababishia mtu kupata matatizo ya kihisia na kusababisha tatizo la kukojoa kitandani kuanza au kuzidi Hadi ukubwani.

3)MADAWA
Kuna baadhi ya dawa husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea dawa hizo ni za usingizi na dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya akili mfano wa dawa hizo ni
Clozapine,cariprazine, risperidone etc

4) TATIZO LA KUKOSA HAJA KUBWA (CONSTIPATION)

5) KISUKARI (DIABETES)

6) MATATIZO YA FIGO (KIDNEY DISEASES)

7)TEZI DUME (ENLARGED PROSTATE)
8)MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(URINARY TRACT INFECTION)
9)TATIZO LA KUFUNGWA KWA NJIA ZA HEWA WAKATI WA USINGIZI (OBSTRUCTIVE SLEEP APNEA)
10) KIBOFU CHA MKOJO KUWA KIDOGO(SMALL BLADDER)

VIPIMO NA uchuNGUZI




Mpendwa msomaji wetu iwapo una tatizo hili usiwe na dhana mbaya za kuhisi una mashetani  au majini fahamu hili ni tatizo lenye kutibika hospitalini hivyo achana na fikra hasi haraka fika hospitali,daktari wako atakufanyia uchunguzi na kukuliza maswali juu ya dalili zako na historia ya afya yako.
Unashauriwa kuwa na diary utakayoandika majibu ya maswali utakayoulizwa na daktari wako ili kusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo
Maswali utakayoulizwa ni ÷

Ni mara ngapi na kwa wakati gani huwa unajikojolea (je,ni usiku au mchana)?

Kiasi gani mkojo hukutoka (mwingi au kidogo)?

Ni kiasi gani cha vinywaji ulikunywa kabla ya kupanda kitandani?

Dalili zingine zozote ambazo umekuwa nazo(unahisi maumivu baada ya kutokwa na mkojo)?

Iwapo daktari wako atahitaji zaidi Kukufanyia uchunguzi ataagiza vipimo vifuatavyo÷

Urine culture and urine analysis: Vipimo hivi hutumika kuangalia maambukizi, damu isiyohitajika na vitu vingine kwenye mkojo.

Blood tests : kipimo hiki cha damu hutumika kuangalia figo na tezi, kiwango cha cholesterol iliyopo katika damu na iwapo kama Kuna shida ya upungufu wa damu au ugonjwa wa kisukari na homoni.

Bladder scans: hiki ni kipimo cha ultrasound ambacho mgonjwa atatakiwa kupima ili tujue ni kiwango  gani cha mkojo hubakia katika kibofu mara baada ya kukojoa.

Urodynamic tests: kipimo hiki kitahitajika kupimwa ili kuangalia au kuona jinsi sehemu ya chini ya mkojo huhifadhi na kutoa mkojo kiwango gani

Cystoscopy: kipimo hiki pia kitahitajika kuhitimisha uchunguzi ambapo daktari ataingiza bomba nyembamba na lens ndogo ndani ya kibofu cha mkojo ili kuangalia iwapo kuna dalili ya uvimbe,kansa na matatizo mengine.

MATIBABU 


Mpendwa msomaji napenda kuhitimisha somo langu hili kwa kukusihi iwapo una hili tatizo au ndugu yako analo tafadhal fahamu kuwa tatizo hili lina matibabu mengi ambayo matibabu haya hutofautiana kwani mengine hufanya kazi vizuri zaidi ya matibabu mengine.
Kadhalika matibabu ya kukojoa kitandani kwa watu wazima yamegawanyika  katika aina kuu tatu:

1) MATIBABU YANAYOHUSU MFUMO WA MAISHA(LIFESTYLE TREATMENT)


Aina hii ya matibabu inajumuisha kubadilisha ama kudhibiti baadhi ya mambo yaliyopo katika maisha ya muhusika ili kuweza kupona  tatizo hili,miongoni mwa hayo mambo ni

°Kudhibiti utumiaji wa vinywaji:Unashauriwa kupunguza unywaji wa vinywaji vyako wakati wa mchana na jioni.
Lakini pia unaruhusiwa kunywa vinywaji vingi zaidi wakati wa asubuhi ya mapema wakati unaweza kwenda chooni kwa urahisi, unatakiwa kuepuka matumizi ya vinywaji wakati wa jioni.

°Kuwa na ratiba ya kuamka usiku: unashauriwa kuweka kengele katikati ya usiku itakayoweza kukusaidia Kuamka mara moja au mara mbili kwa usiku ili kwenda kukojoa chooni hata kama Hauna mkojo hii itasaidia kujenga mazoea ya kuweza kushtuka unapohisi mkojo

°Kuwa na ratiba ya kwenda chooni mara kwa mara wakati wa mchana; hii itasaidia kuwa sehemu ya utaratibu wako. Hata ukilala wakati wa mchana weka kengele itakayokuamsha ili kuweza kuamka na kwenda kukojoa  lakini pia hakikisha unakojoa kabla ya kulala.

°Epuka vitu vinavyofanya kibofu cha mkojo kujaa kwa haraka; unapaswa kuacha matumizi ya kahawa,pombe,vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi kwani husababisha kibofu chako cha mkojo kujaa na kusababisha mkojo wa mara kwa mara.

2) MATIBABU YANAYOHUSISHA DAWA (MEDICINE)

Aina hii ya matibabu imegawanyika katika sehemu nne kulingana na sababu au chanzo cha tatizo kilichogunduliwa ambapo ni
°dawa za antibiotics hizi hutolewa kutibu maambukizo ya njia ya mkojo(urinary tract infection)

°dawa za anticholinergic hizi hutolewa kwa ajili ya kutibu na kutuliza tatizo la misuli ya kibofu cha kibofu

°dawa za desmopressin acetate hizi hutolewa kwa ajili ya kuongeza viwango vya ADH ili figo zako ziache kutoa mkojo mwingi usiku

°dawa za 5-alpha reductase inhibitor hizi hutolewa kwa ajili ya tatizo la tezi dume na hutumika pia kutibu tatizo hili la kukojoa kitandani pia
Mfano wa dawa hizo ni finasteride


3) MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI (SURGERY)

Aina hii ya matibabu huamuliwa kufanyika kutokana na ukubwa wa tatizo na chanzo au kisababishi cha tatizo hili kuwa kubwa

1)SACRAL NEUROMODULATION THERAPY


Hii ni moja wapo ya chaguzi kadhaa za matibabu ya oparesheni  kwa ajili ya kutibu tatizo la kukojoa kitandani kwa mtu mzima ambapo tatizo hilo limetokana na kuwepo kwa matatizo katika kibofu cha mkojo kushindwa kudhibiti au kuzuia mkojo kutoka (overactive bladder)

2) AUGMENTATION CYSTOPLASTY


Haya ni matibabu ya upasuaji katika kibofu cha mkojo ambapo upasuaji hufanyika kwa ajili ya Kuongeza ukubwa wa kibofu cha mkojo kutokana na tatizo la kibofu kuwa kidogo (Small bladder)
Lengo la utaratibu huu ni kuongeza ukubwa na uwezo wa kibofu cha mkojo

3) PELVIC ORGANS PROLAPSE FIX

Haya ni matibabu yanayoweza kuhitajika ikiwa kuna viungo vya uzazi vya kike ambavyo havipo kwenye nafasi iliyokusudiwa nikimaanisha viungo hivyo kutoka mahali na kushinikiza  uzito wote katika kibofu cha mkojo.

4) DETRUSOR MYECTOMY


Huu ni upasuaji ambao unajumuisha kuondoa sehemu au safu zote za nje za misuli ambazo huzunguka kibofu cha mkojo. Hii inalenga kupunguza kiwango na nguvu ya msukumo/shinikizo katika kibofu cha mkojo ambayo husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea pasipo ridhaa yake

NOTED
Mpendwa msomaji wetu ni muhimu kukumbuka kuwa waathirika wenye tatizo hili wataacha kukojoa kadiri wanavyopata matibabu  na ikiwa utamsaidia inavyotakiwa, utamsaidia kuacha mapema zaidi kujikojolea kitandani.
Dharau,kejeli,masimango,kumpiga, au kumchapa mtu mwenye tatizo hili awe mkubwa au mdogo unamuongezea tatizo na kufanya tatizo lizidi au kuchelewa kuisha.
 Ni muhimu sana kumstiri,kutomtisha au kumsema vibaya mwenye tatizo hili. Kufanya hivyo sio tu kama kutazidisha tatizo bali pia humfanya kuwa katika hatari ya kupata matatizo mengine ya kisaikolojia kwa wakati huo na hata baadae katika maisha yake.
Ili kumsaidia mtu mwenye tatizo hili ni muhimu na inashauriwa kumhakikishia na kumfariji  kwa kumuonesha kua anapitia hatua ya kawaida ya maradhi na kuwa kadiri siku zinapita tatizo hilo litaisha. Hii itamsaidia mgonjwa kutopata msongo(stress) na kuusaidia mwili kufanya kazi yake vizuri ambayo hatimaye humsaidia kuondokana na tatizo hili mapema zaidi.


MATIBABU YA TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI (ADULTS NOCTURNAL BEDWETTING/ENURESIS )NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER



Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la kukojoa kitandani ( adults nocturnal bedwetting/enuresis) na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia huduma na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako


Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud ) 

0 comments:

FAHAMU MATIBABU YA UGONJWA WA TUMBO KUJAA MAJI (EXCESS ABDOMINAL FLUIDS/ASCITES)

UGONJWA WA TUMBO KUJAA MAJI EXCESS ABDOMINAL FLUIDS/ASCITES


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, mpendwa msomaji wetu tuna dhana njema juu yako tunaimani unaendelea vyema,tunakuombea afya njema zaidi wewe na familia yako
MWENYEZIMUNGU MTUKUFU AZIDI KUKUJAALIENI AFYA, HIFADHI NA USALAMA
Ameen!

Katika mada yetu ya leo ninakumbushia ugonjwa ambao nimekwishauzungumzia miaka ya nyuma ugonjwa ambao husababisha maji kujaa ndani ya tumbo na mara nyingine husababisha mgonjwa apate matatizo katika kupumua.
 Ni ugonjwa ambao baadaye huweza kusababisha maambukizi ya bakteria katika tumbo – spontaneous bacterial peritonitis (SBP) na kushusha kinga za mwili katika eneo hilo lililojaa maji. Ugonjwa huu huitwa excess abnominal fluids au Ascites


JE, TATIZO LA TUMBO KUJAA MAJI (EXCESS ABDOMINAL FLUIDS/ASCITES) NI UGONJWA GANI?


Ascites/excess abnominal fluids ni ugonjwa wa kujaa maji kupitiliza ndani ya tumbo. Maji haya hujaa ndani ya nafasi iliyopo katikati ya tabaka mbili za utando laini ambazo kwa pamoja hujenga peritoneum(mfuko laini)ambao hushikilia viungo vya ndani ya tumbo.
Kawaida tumboni kunakuwepo maji kiasi ndani ya nafasi hiyo (hadi mililita 20 kwa mwanamke na pungufu ya hapo kwa mwanamme). Kitaalamu maji hayo yanapozidi mililita 25, mgonjwa hutajwa kuwa ana ascites yani tumbo limejaa maji kupitiliza.
Kadhalika tatizo hili limegawanyika katika aina mbili.


AINA za TATIZO lA TUMBO kujaa maji(excess abnominal fluids/ascites

Tatizo hili limegawanyika katika aina kuu 2, yani transudative na exudative.
Mgawanyo huu hutegemea kiwango cha protini kinachoonekana ndani ya maji hayo. Namna bora zaidi iliyotumika ni kutazama kiasi cha albumin kilichopo ndani ya maji (ascitic fluid) kikilinganishwa na kiasi kilichopo ndani ya albumin iliyopatikana ndani ya damu. Hii huitwa Serum Ascites Albumin Gradient au SAAG. Tatizo la tumbo kujaa maji lilotokana na sababu ya pressure kwenye mishipa mikubwa ya damu ya ini (portal hypertension) huwa juu ya  wastani wa 1.1, na ukilinganisha sababu nyingine zilizosababisha tatizo hili  huwa chini ya wastani wa 1.1

CHANZO CHA TATIZO


Kuna vyanzo vingi vya kujaa maji tumboni, ikiwa ni pamoja na kusababishwa na uwepo wa ugonjwa wa kifua kikuu(tuberculosis) magonjwa ya figo(kidney diseases) maambukizi katika kongosho(pancreatitis) na udhaifu wa utendaji kazi wa tezi ya thyroid.
Lakini pia vyanzo vikuu vilivyo bainishwa kwa tatizo la maji kujaa ndani ya tumbo ni magonjwa ya ini yaliyo katika hali mbaya (cirrhosis).
 Pamoja na kwamba haijajulikana kwa hakika ni vipi tatizo la tumbo kujaa maji linatokea, nadharia nyingi zinaamini kuwa kuongezeka kwa msukumo katika mishipa ya kupeleka damu kwenye ini (portal hypertension) kuna mchango mkubwa zaidi kuliko sababu nyinginezo ambazo zimeorodheshwa.

Kanuni ya msingi inafanana na ile inayosababisha kuvimba (EODEMA) kwenye maeneo mengine ya mwili ambapo kunakuwa na utofauti wa msukumo kwenye sehemu mbili zinazopakana, sehemu moja ya ndani ikiwa ya msukumo mkubwa na ya nje, kwa hapa ni uwazi wa tumbo, ikiwa na msukumo mdogo.
Kadhalika Kuongezeka kwa pressure kwenye mishipa inayolilisha ini na kupungua kwa albumin (protini iliyopo ndani ya damu) vinaweza kuwa visababishi vya tofauti hizi za msukumo na kusababisha maji kujaa ndani ya tumbo kupitiliza (Ascites)

Pia visababishi vingine vinavyochangia tatizo la maji kujaa tumboni ni chumvi na kuzuiwa kwa maji.
Kadhalika damu iliyopo ndani ya mzunguko inaweza kuchukuliwa kuwa ni ndogo ikitazamwa na figo kwa sababu tatizo hili  linapoanza, hupunguza ujazo wa damu kwenye mzunguko. Hii huzifanya figo kuhifadhi chumvi na maji zaidi kufidia upungufu huo wa damu.

Matatizo mengine yanayohusiana na utofauti wa pressure ya pande mbili ni congestive heart failure na uharibifu wa figo ulio mkubwa ambao huzuia maji ndani ya mwili.

Kadhalika ni Mara chache sana mwongezeko wa pressure kwenye mishipa ya damu ya ini hutokana na kuzibwa kwa ndani au nje kwa mishipa hiyo, hivyo kusababisha portal hypertension bila uharibifu wa ini (cirrhosis). Mifano ya hali hii ni kama uvimbe kugandamiza juu ya mishipa hiyo kutoka kwenye uwazi wa tumbo au damu iliyoganda kuziba ndani ya mishipa hiyo na kusababisha mwongezeko wa pressure (mfano, Budd-Chiari syndrome.)

Pia tatizo hili huweza kujitokeza vile vile kwa sababu ya kansa, ambayo huitwa malignant ascites,aina hiyo mara nyingi ni ishara ya kansa zilizokomaa ndani ya tishu zilizomo kwenye uwazi wa tumbo, kama saratani ya utumbo mkubwa, saratani ya kongosho, saratani ya tumbo, saratani ya matiti, lymphoma, saratani ya mapafu, au saratani ya ovari.

Dalili 

Mpendwa msomaji wetu fahamu kua kunaweza kusitokee dalili zozote za kukujulisha kua una tatizo la kujaa maji tumboni hasa wakati tatizo ni dogo (maji pungufu ya mililita 100-400 kwa mtu mzima). Kadiri maji yatakavyoongezeka, kipimo cha mzunguko wa tumbo na ukubwa wa tumbo vitaongezeka na kuonekana kwa macho.
Kadhalika dalili hizi zitakua ni zenye kujitokeza yani
Kupata maumivu ya tumbo
Kukosa raha
Kuvimba au kuwamba kwa tumbo kutaonekana.
Kukosa pumzi kutajitokeza pale tumbo litakapojaa sana kutokana na kuongezeka kwa pressure kwenye diaphragm na majimaji kuvuka diaphragm na kusababisha maji kuingia kwenye mapafu.
Kuhisi kichefuchefu,
kutosikia njaa,
uchovu, kuziba choo na kupata haja ndogo ya mara kwa mara.


VIPIMO na maTIBABU

Daktari anaweza kubaini tatizo hili kwa kuangalia tumbo la mgonjwa kadhalika vipimo vifuatavyo hutumika kubaini tatizo hili vipimo hivyo ni
Blood tests, fluids sample analysis, abdominal ultrasound,MRI,na X-RAYS.
Matibabu ya tatizo hili la maji kujaa tumboni kwa kiasi kikubwa hutegemea kuangalia chanzo halisi cha ugonjwa huu.
 Kwa mfano, ikithibiti mgonjwa ana peritoneal
 carcinomatosis au malignant ascites to atatibiwa kwa kufanyiwa  upasuaji kuondoa eneo lililoathirika na saratani au kupatiwa tiba ya mionzi (chemotherapy), wakati ascites iliyotokana na matatizo ya moyo itadhibitiwa kwa dawa za kutibu chanzo cha moyo kushindwa kufanya kazi vizuri au  mgonjwa atapatiwa ushauri wa vyakula.

Kadhalika endapo maji kujaa tumboni kumetokana na kuharibika kwa ini (cirrhosis), mgonjwa atasaidiwa kwa kushauriwa kupunguza matumizi ya chumvi na kumeza vidonge vya kutoa maji yaliyozidi mwilini. Vidonge hivyo vitamfanya atoe haja ndogo mara nyingi zaidi huku vikizuia utunzwaji wa maji mwilini. Pamoja na kuwa hii ni njia bora, aina nyingine za ugonjwa huu hazisikii tiba hii.

Hali ikiwa mbaya sana, operesheni ya kubadilisha ini inaweza kuwa ndiyo uamuzi wa mwisho.
Kadhalika tiba nyingine zinazotumika kutibu tatizo hili ni kama ifuatavyo:

Paracentesis

 Hii ni tiba ambayo hutumika kama tiba nyingine hazikutoa msaada mkubwa au kama maji ni mengi sana, tiba ya abdominal paracentesis hutumika. Hii ni njia ambapo daktari huingiza sindano tumboni na kutoa maji yaliyozidi nje ya mwili.
Lengo ni kupunguza msukumo ndani ya tumbo, na kumfanya mgonjwa ajisikie vizuri. Maji yanayotolewa yanaweza kufika lita 5, ingawa kuna wagonjwa wenye hali mbaya zaidi ambao hutolewa maji zaidi ya lita 10.

shunts

Kadhalika tiba hii hutumika endapo maji yamejaa tumboni kutokana na kansa hivyo daktari anaweza kutumia mpira kuondoa maji kutoka kwenye tumbo na kuyaingiza kwenye mtiririko wa damu.
Daktari huchoma sindano kwenye neva ya shingoni na kuweka shunt kupitia
kifuani. Shunt hiyo huunganisha uwazi wa tumbo na shingo, na kuingia kwenye veni. Na hivyo maji hutiririka kupitia mrija huo hadi kwenye mzunguko wa damu.

chemotherapy

Matibabu ya chemotherapy yanaweza kutumika kudhibiti saratani. Inaweza kufanywa kutumia mpira unaoingizwa tumboni, ingawa hakuna ushahidi wa kuwa njia hii ina matokeo bora.



HATUA ZA KUFATA KUTIBU/KUPUNGUZA UKUBWA WA TATIZO LA TUMBO KUJAA MAJI (EXCESS ABDOMINAL FLUIDS /ASCITES)

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kukusaidia kuweza kutibu au kupunguza ukubwa wa tatizo hili ambalo hukuweka katika hatari ya kupata tatizo la ini na saratani au matatizo ya figo,mapafu na magonjwa mengine mbalimbali

Unashauriwa kuacha kunywa pombe.

Kupunguza uzito uwe na uzito stahiki katika afya(usiwe na uzito mdogo sana au mkubwa Sana)

Dumu kufanya mazoezi mara kwa mara.

Acha kuvuta sigara,bangi na kula mirungi

Punguza matumizi ya chumvi katika vyakula vyako

Kama umeoa au kuolewa unashauriwa kushiriki tendo la ndoa mara kwa Mara ili kupunguza nafasi ya kupata ugonjwa wa hepatitis (epuka ngono zembe kuepusha kuambukizwa ugonjwa wa hepatitis)

Epuka kutumia dawa hovyo hovyo pasipo kupata ushauri kutoka kwa daktari

Pata usingizi wa kutosha na ondoa msongo wa mawazo

VIFAHAMU VYAKULA VYENYE KUSAIDIA KUPUNGUZA MAJI YALIYOJAA TUMBONI

1)KITUNGUU SAUMU(GARLIC)
Vitunguu saumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kuponya tatizo la tumbo kujaa maji (ascites). Chukua punje 20 za vitunguu saumu na maji kiasi cha 125 mls visage kwa pamoja
Kisha kunywa mchanganyiko huo mara kwa mara kwa siku moja uwe umeumaliza
Kadhalika ili kupata matokeo mazuri tengeneza mchanganyiko huo kila siku na uwe unafululiza kunywa angalau kwa siku 14 utaona matokeo.

2) MBEGU ZA UWATU(FENUGREEK SEEDS)

Ili uweze kutumia mbegu za uwatu kutibu tatizo la tumbo kujaa maji loweka mbegu za uwatu kiasi cha gram 25 usiku kisha unywe maji hayo asubuhi
Unashauriwa kuendelea na zoezi hili kwa muda usiopungua wiki mbili ili kupata matokeo mazuri

3) VITUNGUU MAJI(ONIONS)

 ni miongoni mwa viungo vyenye nguvu katika kutibu magonjwa mbalimbali. Kwa hivyo, unashauriwa  kuvijumuisha katika lishe yako  kwa kuvitafuna vibichi kila siku.
Hii itasaidia kuyatoa maji yaliyokusanywa tumboni  kupitia njia ya mkojo
Unashauriwa kutafuna walau vitunguu maji vikubwa vitatu kila siku


4) MAFUTA YA UFUTA (SESAME OIL)NA MAFUTA YA MNYONYO(CASTOR OIL)
Unashauriwa kulikanda kanda tumbo kwa kutumia mafuta ya ufuta(sesame oil) au mafuta ya mnyonyo (castor oil) kwakua kulikanda tumbo inasaidia kuondoa maji kupita kiasi kutoka ndani ya mwili

NOTED
Mpendwa msomaji wetu fahamu kua tatizo hili la tumbo kujaa maji ni tatizo la hatari lisipotibiwa mapema linaweza kusababisha madhara makubwa kwa mgonjwa kama vile kupata maradhi ya KANSA,INI, MAPAFU NA FIGO pia huweza kupata magonjwa ya moyo.
Iwapo wewe au ndugu yako ana tatizo hili mshauri apate kufika hospital iliyo karibu naye kwa msaada wa huduma ya matibabu zaidi.

MATIBABU YA TATIZO LA TUMBO KUJAA MAJI(EXCESS ABDOMINAL FLUIDS/ASCITES NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER



Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la tumbo kujaa maji na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia huduma na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako


Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud ) 

0 comments:

FAHAMU TATIZO LA KUWA NA HOFU NA WASIWASI KUPITILIZA (ANXIETY DISORDERS) NA MATIBABU YAKE

FAHAMU TATIZO lA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,
Tunakuombea afya njema zaidi wewe pamoja na familia yako na wote unaowapenda
MWENYEZIMUNGU MTUKUFU AZIDI KUWAHIFADHI NA KUWAJAALIA REHMA ZAKE 
AMEEN!

Naam leo nimeona ni khery tukaongelea juu ya mada hapo juu kutokana na athari tunayoiona katika jamii zetu kwa watu wengi kuathirika kisaikolojia kwa kukosa uwezo wa kujiamini kwa kuathirika kwao kwa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza,mathalani ni kitu cha kawaida mtu kupata wasiwasi au hofu pale anapopatwa na changamoto za kimaisha kwa kushindwa kupata ajira, kushindwa kufaulu shuleni, kusalitiwa ama kukosana na mpenzi wake,kufiwa,kufilisika,kuhofia usalama wa maisha yake na kadhalika  lakini endapo wasiwasi na hofu vikakufanya ushindwe kumudu maisha yako ya kawaida kama unavyopenda, hapo ndipo tunasema mhusika Ana tatizo la wasiwasi na hofu kupitiliza ( anxiety disorder/ugonjwa wa hofu na wasiwasi)

Kuna aina nyingi za tatizo la kuwa na wasiwasi na hofu kupitiliza (anxiety disorders)  na njia nyingi za kutibu au kumfanya mtu ajisaidie. Ukishakuwa umelijua tatizo lako hili la wasiwasi na hofu kupitiliza (anxiety disorder) kuna hatua za kuchukua ili kupunguza dalili zake au kurudisha udhibiti wa maisha yako hivyo usijali sana iwapo unasumbuliwa na hill tatizo


JE, TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS) NI NINI?


Wasiwasi au hofu unaweza kuelezewa kuwa ni mwitiko wa mwili wako kwa vitu hatarishi kwa maisha yako vinavyokuja au unavyofikiria vinaweza kuja.
Wasiwasi unahusiana sana na hofu ambayo ni mwitiko wa mwili wako kukujulisha kuhusu hatari halisi (hatari iliyo mbele yako) au inayofahamika kuja siku za karibuni.
Hivyo Hofu na wasiwasi uliopitiliza ni hali ya ugonjwa wa kiakili ambao unamfanya muhusika kua na hofu muda wote na kukosa utulivu wa akili na hata kushindwa kutoa maamuzi.

Mfumo wa ubongo hudhibiti mwitiko huu wa mwili wa kupambana au kuyakimbia mazingira hatarishi, na mara nyingi huambatana na kupanuka kwa mboni za macho, kuongezeka kwa kasi ya mapigo ya moyo, na kuongezeka kwa jasho/uhemaji.

Mwitiko wa wasiwasi unaweza kuambatana na uangalifu zaidi wa mazingira na kukaza kwa misuli tayari kuikabili hatari.
Wasiwasi unaweza kuwa na manufaa, kama kuongeza ufanisi na kufanya vizuri zaidi kwenye michezo, au kuzungumza mbele ya kadamnasi. Pamoja na kuwa hii ni miitiko ya kawaida ya mwili na mara nyingi ni miitiko yenye manufaa wakati wa hatari, wasiwasi unaweza kuwa na athari endapo utazidi kiwango au ukiendelea kuwepo bila ya kuwepo kwa hatari
Wasiwasi mwingi uliokithiri(kupitiliza) unaweza kukukosesha raha, na kuharibu utendaji wako wa kazi, na huu ndio huitwa ugonjwa wa hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder)
Lakini pia tatizo hili lipo katika namna au aina nyingi.

Aina ZA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY disorders)

Tatizo la hofu na wasiwasi mwingi uliopitiliza (anxiety disorders)hutofautishwa kufuatana na aina ya kitu au mazingira yanayosababisha woga na wasiwasi, pamoja na namna ya fikra anazokuwa nazo mtu akishikwa na hofu au wasiwasi.
Lakini Kusudi mtu aitwe ana tatizo hili, hofu na wasiwasi lazima viwe vya muda mrefu, vilivyodumu miezi 6 au zaidi.
Matatizo ya kuwa na wasiwasi kwa kawaida huanza utotoni lakini hudumu ukubwani.

Aina ya tatizo la kuwa na hofu na wasiwasi kupitiliza (anxiety disorder ni ;

Specific PHOBIAS ANXIETY DISORDERS
 Hii ni hali ya kuwa na hofu na wasiwasi uliokithiri kwa kuhofia kitu au mazingira fulani, mfano;kama buibui kuwa juu ya nyumba yako,kupanda ndege, au kukaa sehemu zilizofungwa Katika mambo ya kijamii.

SociAL PHOBIA/PERFORMANCE ANXIETY DISORDERS

Hii ni hali ambayo mtu anakuwa na wasiwasi na hofu kubwa kwa kuogopa kushiriki shughuli za kijamii, au mazingira yanayomfanya watu wamwone au kumjadili.

GENERALIZED ANXIETY DISORDERS(GAD)

 ni aina ya tatizo linalojitambulisha kwa mtu kuwa na wasiwasi na hofu kubwa inayodumu kwa kipindi kirefu inayotokana na maeneo tofauti ambayo ni vigumu kuyadhibiti.
Woga unaoendana na aina ya tatizo la wasiwasi aina ya GAD huathiri uwezo wa mtu wa kufikiri, kupata usingizi, au kufanya shughuli fulani.
 Dalili zake hujionyesha kwenye hisia na tabia na namna ya kufikiri ambavyo ni matokeo ya hali ya mwili kufikiria kuwa kuna hatari.
Ukiwa na aina hii ya wasiwasi GAD, utapata wasiwasi kutokana na vitu vinavyowapa wasiwasi watu wote, lakini wewe utaupeleka wasiwasi huo kwenye ngazi nyingine, ya juu zaidi
Mfano;
Mfanya kazi mwenzako akitoa maoni yake kuhusu hali ya uchumi kwako shida utaanza kufikiri sana na kuwa na hofu
rafiki yako asipotoa majibu kwa simu yako haraka, unaanza kufikiri kuwa mahusiano yenu si mazuri.
Wakati mwingine hata wazo tu la kuwa utashinda kazini kwako ni mwanzo wa wasiwasi. Unaendesha shughuli zako ukiwa umejaa hofu isiyobainika, na hata kama hakuna kitu cha kuanzisha hofu hizo.

Waweza kuwa unatambua kuwa wasiwasi wako unazidi hali halisi, au unaamini kuwa wasiwasi wako unakulinda kwa namna fulani, mwisho wake ni ule ule. Huwezi kuyafuta mawazo yanayokuletea wasiwasi. Yanazidi kutembea kichwani mwako, yakijirudiarudia  bila kufika mwisho.

SEPARATION ANXIETY DISORDERS
Imezoeleka kuona watoto wadogo ndio wao  pekee ambao huhisi hofu au wasiwasi wakati mtu wanayempenda anaondoka,lakini kumbe Mtu yeyote anaweza kupata hofu na wasiwasi na kujitenga kwa kuwaza au kuhofia juu ya mtu wao wa karibu kua kuna tatizo linaweza kumtokea.

SELECTIVE MUTISM ANXIETY DISORDERS
Hii ni aina ya hofu na wasiwasi wa kijamii ambao watoto wadogo au watu wakubwa ambao huongea kawaida na familia zao lakini wanakua na hofu na wasiwasi yani hawawezi kuzungumza hadharani kama shuleni,kazini nk
Yani kushindwa kuzungumza kwenye baadhi ya mazingira ya watu wengi kama shuleni,kazini nk

AGORAPHOBIA ANXIETY DISORDERS
Hii ni aina ya hofu au wasiwasi uliopitiliza ambao humfanya mtu kuogopa sana kuwa katika mahali ambapo inaonekana kuwa ngumu kutoroka au kupata msaada ikiwa dharura itatokea.
Mfano:
Unaweza kuwa na hofu au kuhisi kuwa na wasiwasi unapokuwa kwenye ndege, usafirishaji wa majini nk

PANIC ANXIETY DISORDERS
Hii ni aina ya wasiwasi au hofu kubwa ambayo inaleta shambulio la hofu Sana kwa ghafla linapotokea jambo unaweza kutokwa kwa jasho kuwa na maumivu ya kifua na kuwa na maumivu ya pigo la moyo wakati mwingine unaweza kuhisi ni kama unavunja au kuwa na mshtuko wa moyo kutokana na hofu kupitiliza

MEDICATION INDUCED ANXIETY DISORDERS
Baadhi ya dawa huweza kusababisha dalili fulani za hofu na wasiwasi
uliopitiliza


CHANZO CHA TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)

Hadi sasa hakujaweza kupatikana chanzo cha moja kwa moja kinachosababisha tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza,ila kuna mambo kadhaa yanaweza kuelezwa kuwa ni chanzo kutokana na ufuatiliaji wa chanzo kwa muda mrefu imeonesha kuwa tatizo la hofu na wasiwasi inaweza kurithiwa kutoka  katika familia yako pia vyanzo vingine vyenye kufikiriwa ni 
Baadhi ya magonjwa: Utafit unaonyesha kuwa kuna magonjwa yanayohusishwa kuwa ni chanzo cha mtu kupata tatizo la hofu na wasiwasi kupitiliza baadhi ya magonjwa hayo ni
KISUKARI, MAGONJWA YA MOYO, MAGONJWA YA MAPAFU,PUMU, MAGONJWA SUGU YA TUMBO, MAGONJWA YA TEZI YA THYROID nk

Matatizo ya ubongo. Utafiti unaonyesha tatizo la hofu na wasiwasi zinaweza kuhusishwa na mzunguko mbaya katika ubongo unaodhibiti woga na hisia

Mazingira. Hii inahusu matukio yanayomusumbua mtu ambayo ameona au kuishi kupitia matukio ya maisha mara nyingi huweza kuhusishwa na tatizo la hofu na wasiwasi ni pamoja na unyanyasaji wa watoto na kutelekezwa, kifo cha mpendwa, au kushambuliwa au kuona vurugu na kushuhudia baadhi ya matukio ya ajali yenye kuogopesha

Matumizi ya dawa. Dawa zingine zinaweza kutumiwa kuficha au kupunguza dalili fulani za wasiwasi. Shida ya wasiwasi mara nyingi huambatana na ulevi na matumizi ya sigara

Ni muhimu kupata uchunguzi kamili wa mwili ili kudhibiti hali zingine za matibabu wakati wa kuzungumza na daktari wako juu  tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza


DALILI ZA TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)
Dalili za kawaida kwa mtu mwenye tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorders) ni pamoja na:

. Kutotulia yani kukukosa utulivu na kujaa wasiwasi
. Kuchoka kirahisi, kuwa mchovu;
. Hupata shida kutuliza mawazo kwenye kitu ambacho kinaweza kuonekana kuwa ni tatizo la kumbukumbu au la kawaida tu
. Kuwa na hisia dhaifu yan kuhisi kuwa ubongo unakuwa mtupu yani unashindwa kupata mawazo mazuri muda wote unajihisi kuhofu hatari 
. Kuwa na hasira za haraka
. Kukakamaa kwa misuli
. Kuumwa kichwa na kuwa na hofu kubwa
. Mapigo ya moyo kwenda mbio kupata shida kupumua
. Matatizo ya usingizi (kukosa usingizi)
. Kupata vidonda vya tumbo na kiungulia
. Kukosa ujasiri wa kupambana na changamoto
Wasiwasi unaohusiana na hofu ya kitu fulani (specific or simple phobia) au wasiwasi wa mambo ya kijamii (social phobia) unaweza kusababisha kuyakwepa mazingira fulani au kukuza dalili zinazoleta panic attack – hofu kubwa ya ghafla inayofikia kilele katika muda mfupi.

VIPIMO NA MATIBABU

Hatua ya kwanza ni kuonana na daktari wako ili kuhakikisha kuwa hakuna shida ya kiafya inayosababisha dalili za hofu na wasiwasi uliopitiliza.
Si kila mtu anayekuwa na wasiwasi sana ana tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder) Unaweza kuwa na wasiwasi kwa sababu ya kuwa na majukumu mengi,ratiba kali ya kazi, kukosa usingizi au mazoezi, msongo wa mawazo au majukumu ya ulezi wa familia  nyumbani, au kunywa kahawa kupita kiasi.
Lakini pia kama maisha yako si ya furaha na ni ya msongo wa mawazo na huzuni kila wakati, ni ishara tosha kuwa una tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza hivyo unahitajika kufika hospital kwa uchunguzi zaidi.
Kadhalika matibabu ya tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza hutegemea asili au chanzo cha tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza hivyo hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine
Mara nyingi matibabu ya tatizo hili huchanganywa kutegemeana na hali ya mgonjwa jinsi ilivyo ambapo kuna matibabu ya dawa na ushauri nasaha ambao mgonjwa akipatiwa anaweza kupona pasipo kuhitajika kutumia dawa
Walakini, ikiwa njia ya ushauri haipunguzi athari za dalili za wasiwasi, au ikawa ni chanzo cha kuongeza mashambulizi ya mshtuko na wasiwasi wa ghafla yani dalili kuwa kali daktari wako atawajibika kukupatia huduma ya matibabu mengine yatakayojumisha dawa na ushauri nasaha.
Kadhalika Kuna matibabu ya tabia ya utambuzi (CBT) ambayo ni aina ya tiba ya kuongea, inaweza kumsaidia mtu kujifunza njia tofauti za fikra na kusaidia kuondoa wasiwasi pia dawa zinazotumika sana ni dawa za kupunguza wasiwasi (kwa ujumla zinatumika kwa kipindi kifupi tu) ambazo ni Antidepressants,anxiolytics,beta-blockers ambazo hutumiwa kwa matatizo ya moyo, wakati mwingine hutumiwa kudhibiti dalili za mwili za wasiwasi na mfadhaiko.


HATUA ZA KUFATA KUPAMBANA NA TATIZO LA HOFU NA WASIWASI ULIOPITILIZA (ANXIETY DISORDERS)
Mpendwa msomaji nina imaani ya kwamba umejifunza mambo mengi kuhusu tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorders)
Napenda nihitimishe kwa kukupatia ufumbuzi wa kuweza kupambana na tatizo hili ukiwa una shaka au kuhofia kuwa unalo hili tatizo
Kwa kufanya yafuatayo unaweza kupunguza wasiwasi na kudhibiti dalili za hofu na wasiwasi uliopitiliza na kupunguza ukubwa wa tatizo


EPUKA KUKAA PEKE YAKO,JICHANGANYE NA WENGINE.
Upweke unaweza kukuletea au kukuongezea wasiwasi, jitahidi kuwa muwazi zungumzia matatizo yako kwa watu wako wa karibu na changamana nao ili uweze kujipunguzia hofu na kupata matumaini na kuwa ni mwenye kujiamini
Jitahidi kila wakati kukutana na marafiki zako, jiunge na vikundi vya kusaidiana, au mshirikishe mambo yanayokusumbua mtu umpendaye.
 Kama huna mtu wa namna hii, hujachelewa kuanza kujenga mahusiano mapya yenye kukujenga


DHIBITI MSONGO WA MAWAZO
Kama unasumbuliwa sana na msongo wa mawazo jitahidi kupata ushauri wa kuondokana na msongo wa mawazo au dawa zitakazokusaidia kuondokana na msongo wa mawazo kadhalika Unaweza pia kuona ni majukumu yapi ya kuyaacha, kuyapunguza au kuwaachia wengine ili yasiushughulishe ubongo wako kiasi cha kupata hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder)

JENGA TABIA YA KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU
Kufanya mazoezi ya mwili ni njia ya asili ya kupunguza msongo wa mawazo na kuondoa wasiwasi pamoja na mfadhaiko
Ili Kupata matokeo bora kabisa, lenga kufanya mazoezi ya kuongeza mapigo ya moyo na kutoa jasho (aerobic exercises) kwa muda wa dakika 30 kila siku.
Mazoezi au shughuli za kuifanya mikono na miguu kuwa katika mwendo kwa wakati mmoja (rhythmic activities) ni ya manufaa sana. Jaribu kutembea, kukimbia, kuogelea, kucheza,kurukaruka nk itasaidia Kupunguza hatari na dalili za hofu na wasiwasi uliopitiliza

PATA USINGIZI WA KUTOSHA
Kukosa usingizi wa kutosha kunaweza kukuza tatizo la kuwa na wasiwasi kwa hiyo jitahidi kupata wasaa wa kulala masaa 8 hadi 9
Kulala usingizi mzuri ni miongoni mwa mambo yanayouweka mwili katika hali nzuri ya afya


JIAMINI NA PINGA(UKATAE) WASIWASI
Unapopatwa na hali ya  kuhofu au kuwa na wasiwasi uliopitiliza ikatae hiyo hali kwa kuamua kutoogopa kitu chochote jipatie ujasiri jiamini na ishinde hofu uliyonayo tena jitengenezee mkakati wa kufanya mambo yote ambayo unayapatia hofu hii itakusaidia kupambana na tatizo hili ambalo ni hatari kwa afya ya akili na mwili

EPUKA POMBE, SIGARA, MADAWA NA KAHAWA
Ikiwa unapambana na tatizo la kushinda wasiwasi, unatakiwa kupunguza au kuepuka kabisa matumizi ya pombe, kahawa,sigara na madawa ya kulevya kwasababu vitu hivi hasa pombe inafanya hali ya wasiwasi kuongezeka tofauti na kule kudhania kuwa inapunguza wasiwasi. Kadhalika na sigara inaonekana kama ni kitulizo bila ya kujua kua kuna sumu ya nikotini ambayo ndio kichocheo kikubwa cha kusababisha ongezeko la wasiwasi.
Unashauriwa iwapo una nia ya kupona tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorders) epukana na matumizi ya vitu hivyo.


VIFAHAMU VYAKULA VYENYE KUSAIDIA KUONDOA WASIWASI
Ni vyema ukafaham kuwa kuna vyakula ambavyo ukila kwa wingi vinakusaidia kupunguza ukali wa dalili za tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza kutokana na uwezo wa vyakula hivyo kusaidia  ubongo kufanya kazi ipasavyo
Baadhi ya vyakula hivyo ni ÷
1)MAFUTA YA SAMAKI (FISH OIL)

Mafuta ya samaki yana faida nyingi sana katika mwili wa mwanadamu na yanasaidia kupunguza hofu na wasiwasi.
Hii ni kutokana na kua yana virutubishi ambavyo vinakuza afya ya ubongo, pamoja na vitamini D na asidi ya asidi ya omega-3 eicosapentaenoic acid (EPA) na asidi ya dosahexaenoic (DHA) 

EPA na DHA zinaweza kusaidia kudhibiti homoni na kemikali za neurotransmitters  na serotonin kuondoa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza.


2)BINZARI NYEMBAMBA (TUMERIC)
 Unaweza ukastaajabu kusikia kiungo hiki kina uwezo wa Kupunguza na kuondoa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza
Ukweli ni kwamba binzari nyembamba ina uwezo wa kupambana na Kupunguza dalili za hofu kwa Kusaidia ufanyaji kazi katika ubongo

3) CHOCOLATE NYEUSI
4)MAZIWA MGANDO
5)MBEGU ZA CHIA(CHIA SEEDS)
6)KOROSHO NA LOZI(CASHEWS NUTS&ALMONDS)
7) MATUNDA YENYE VITAMIN C NYINGI
8)MAYAI NA NYAMA



 TATIZO HILI LA ANXIETY DISORDERS NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder) na magonjwa mengine mbalimbali na mmejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia ushauri au dawa za kuondoa tatizo la hofu na wasiwasi uliopitiliza (anxiety disorder)na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako

NOTED;
Mpendwa msomaji iwapo wewe au ndugu yako ana tatizo hili fanya haraka ya kupata ufumbuzi wa Matibabu kwakua tatizo hili lina athari nyingi katika mfumo wa mwili 
Miongoni mwa madhara ya kuwa na tatizo hili la hofu na wasiwasi uliopitiliza ni kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa mengine makubwa kama
KUPATA SHINIKIZO LA DAMU, MFADHAIKO,MATATIZO KATIKA MFUMO WA UPUMUAJI,KINGA YA MWILI HUSHUKA,KUKOSA USINGIZI,KUPATA MATATIZO KATIKA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA NK

Tunamuomba ALLAH HIFADHI NA SALAMA TUWE WENYE KUNUSURIKA NA MARADHI MAKUBWA 
AMEEN


Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre