FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA TATIZO LA WANAWAKE KUTOKWA NDEVU NA VINYWELEO MWILINI(HIRSUTISM)


MATIBABU YA TATIZO LA WANAWAKE KUTOKWA NDEVU NA VINYWELEO MWILINI (HIRSUTISM) 



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji
Kwa upande wangu namshukuru Allah kariim kwa kunikirimu afya njema mimi pamoja na familia yangu na kuniwezesha kupata wasaa wa kuwajibika katika majukumu yangu

Naam ni jambo la kumshukuru Allah kuiona siku mpya kila siku haijalishi unaumwa ama una magumu unapitia USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE hivyo mshukuru Allah kwa kila kitu katika maisha yako

Leo ninakumbushia kuelezea suluhisho la tatizo ambalo nilishawahi kulielezea miaka ya nyuma kidogo ambalo hadi sasa limekua likiendelea kusumbua vichwa vya wanawake wengi juu ya upatikanaji wa tiba sahihi


TATIZO LA HIRSUTISM NI NINI?


Ni tatizo ambalo huwatokea  wanawake kwa kupatwa na mabadiliko ya  kuotwa manyoya/vinyweleo sehemu ambazo kikawaida wanawake huwa hawaoti au hawapendezi kuwa na manyoya/vinyweleo maeneo hayo.

mfano wa maeneo hayo ambayo mwanamke hafai kuotwa na vinyweleo ni kupata manyoya kidevuni yani anaonekana kuwa na ndevu kama mwanaume,au kuotwa na manyoya kifuani, usoni, na mgongoni wakati mwingine manyoya magumu kama ya kiume miguuni na mikononi kitu ambacho sio cha kawaida kutokea kwa mwanamke

Kikawaida wingi wa manyoya mwilini mwa binadamu hutegemea sana vimelea vya ukoo husika, kitaalamu kama genetics lakini mwanamke anapokua na manyoya mengi sehemu ambazo haifai au haipendezi  kwa mwanamke kua vinyweleo mfano mwanamke kuwa na ndevu kuna mambo makuu mawili kwamba anaumwa au ukoo wake uko hivyo japokua waathirika wengi wa shida hii wengi ni wagonjwa wa matatizo ya homoni.

Kuna imaani nyingi zimejengeka juu ya mwanamke kuota ndevu na manyoya mwilini lakini sio katika uhalisia kuwa eti mwanamke akiotwa na ndevu ATAKUA TAJIRI NA MANENO MENGINE MENGI MENGI YASIYO NA UKWELI


CHANZO CHA TATIZO



Kawaida mwanamke akibaleghe huanza kutengeneza homoni za kiume na za kike ndio maana manyoya huota kwapani na maeneo ya uke lakini sasa inapotokea homoni za kiume zikiwa nyingi kitaalamu kama adrogens mwanamke hupata hali hii ya kuota manyoya sehemu ambazo hazihusiki kama nilivyotaja hapo juu
 lakini pamoja na hali hii ugonjwa huu una vyanzo vingine kama vifuatavyo.

POLYCYSTIC OVARY SYNDROME: 
huu ni ugonjwa unaowasumbua wanawake kwa kutokuwa na uwiano sawa wa homoni za kike ambapo kitaalamu tunasema mwanamke kuwa na tatizo  la homornal imbalance hivyo mwanamke hupata mzunguko wa damu ambao sio wa kawaida, kua mgumba,  kunenepa na kupata uvimbe kadhaa kwenye ovari za kutengeneza mayai yake na kupata shida mbalimbali za kuhusu uzazi

MATUMIZI YA DAWA NA VIPODOZI VYENYE KEMIKALI
Chanzo hiki huenda pia ndio kikawa chanzo kikuu cha wanawake wengi kuota ndevu na manyoya  kwa tabia ya kutumia dawa fulani bila maelekezo ya daktari pia siku hizi kuna maduka ya urembo yanauza dawa hizi na kuzigeuza dawa za urembo wakati ni hatari  sana kiafya kwa watumiaji.
kuna dawa kitaalamu zinaitwa steroids huingilia mfumo wa kiungo kinachohusika na utengenezaji wa homoni (Adrenal gland) hivyo zikitumika kwa muda mrefu huleta manyoya ambayo sio ya kawaida kwa wanawake
mfano wa dawa hizi za steroids ni PREDINISOLONE vidonge na cream, SONADERM, CANDIDERM, GENTALINE, na dawa zingine zote zenye mchanganyiko huu kwani zipo nyingi ila mchanganyiko ni uleule ila majina tofauti ya viwanda.
 Dawa hizi hutakiwa zitumike kwa angalau wiki moja tu kutibu ugonjwa wa ngozi lakini wengine wamezigeuza kama mafuta ya kujipaka hivyo kama na wewe unapaka hizo aina za dawa ujue Umejitengenezea mazingira hatarishi ya kuweza kupatwa na tatizo hili la kuotwa vinyweleo

UVIMBE WA KANSA
kansa za kiungo hichi kilichopo juu ya figo[adrenal gland] huongeza wingi wa homoni hizi kwenye mfumo wa binadamu na kuleta ndevu na manyoya magumu ya mwili.

CONGENITAL ADRENAL HYPERPLASIA:
huu ni ugonjwa wa tezi ya adrenal ambao mtu huzaliwa nao na kuanza kutoa homoni nyingi za uzazi na matokeo yake mtu huota ndevu na manyoya mengi mwilini..

CUSHING SYNDROME:
hali hii hutokea baada ya mgonjwa kupata matibabu ya dawa zenye homoni ya  cortisol mwilini mwake kwa muda mrefu. Mfano matumizi ya dawa ya prednisolone vidonge  kwa wagonjwa wa allergy na asthma.

Wakati mwingine ugonjwa huu hutokea bila sababu yeyote hasa kwa jamii za kiarabu na kihindi




DALILI ZA TATIZO


Kawaida mgonjwa wa hirsutism huwa na dalili za kua na manyoya mengi kama nilivyotaja hapo juu lakini pia mgonjwa huweza kua na sauti nzito kama mwanaume, kuota kipara, kinembe kua kikubwa, chunusi na kupungua ukubwa wa matiti


VIPIMO


Mgonjwa anashauriwa kufika hospital kuonana na daktari na kupata vipimo kuangalia wingi wa homoni mwilini wake hasa testosterone kama zitakua zipo juu Au kupiga picha ya ultrasound ya ovary kuangalia kama kuna tatizo lolote au kupima kuangalia uvimbe wa adrenal gland  mara nyingi ni moja ya vyanzo vikuu.


MATIBABU

Matibabu ya tatizo hili hujulikana mara baada ya kutafuta chanzo cha ugonjwa na ni moja ya matibabu bora zaidi kutibu kwa kudhibiti chanzo cha tatizo lakini pia pale ambapo  chanzo hakionekani dawa za uzazi wa mpango na zinginezo hutumika kutatua tatizo hilo kwa hisia ila jambo lenye ubora ni kujua chanzo cha tatizo
Baadhi ya dawa zingine ni zifuatazo ;

SPIRONOLACTONE
Dawa hizi hutumika kuzuia homoni za kusababisha manyoya lakini ukitumia dawa hizi lazima utumie uzazi wa mpango kwani zinasababisha madhara makubwa sana kwa mtoto ikitokea  ukibeba  mimba wakati unaendelea na dozi hiyo.

DAWA YA KUPAKA YA EFLORNIRITHINE;
 Dawa ya  Eflornithine  kitaalamu hutumika kupakwa maeneo yalioathirika na nywele nyingi kuzuia kasi ya kukua lakini hazitoi manyoya yaliyopo.

LASERS THERAPY
 hii ni miale ya mwanga ambayo inapita ndani ya ngozi kuzuia vyanzo vya ngozi{hair follicles} kuota tena mara nyingi hufanya kazi vizuri lakini gharama yake ni kubwa mno na huenda haipatikani kirahisi.

VEET CREAM :
 hii ni cream inayopatikana madukani kwa bei za kawaida ukipaka inanyoa manyoya yote japokua baada ya muda yataota tena lakini inasaidia sana hasa ukipaka mara mara kwa mara au mara moja au mbili kwa wiki.

 ELECTROLYSIS:
hii inahusisha kuweka sindano ndogo  maalumu kwa kila shimo la unywele na kuharibu chanzo chake ni moja ya matibabu mazuri ila ina maumivu makali sana na dawa za nganzi za kupakwa hutumika kupunguza maumivu hayo.

NOTED; kama wewe ni mwanamke una ndevu au manyoya ambayo sio ya kawaida na huenda mwanzoni hayakuepo angalia kwa makini vipodozi vyako huenda ndio vinasababisha lakini pia nenda hospitali ukachunguzwe wingi wa homoni na upigwe picha ya viungo vya uzazi kama viko salama. ushauri wa bure ni kwamba serikali imekua ikipiga marufuku baadhi ya vipodozi na kuvichoma moto lakini watu wanahisi wanaonewa na kuvitafuta kwa magendo, ukiona kitu kimepigwa marufuku acha kutumia kiepuke



HATUA ZA KUFATA KUTIBU NA KUDHIBITI KUENDELEA KWA TATIZO LA WANAWAKE KUOTWA NDEVU NA VINYWELEO

Kuna hatua kadhaa za kiasili ambazo zimethibitishwa kuonyesha matokeo baada ya watumiaji kuleta mrejesho wa matokeo mazuri
Hatua hizi zimegawanyika katika utaratibu mzuri ambapo ukizingatiwa na kutekelezwa ipasavyo inaleta matokeo mazuri na kudhibiti kuendelea kuota kwa ndevu na vinyweleo
Hatua za kufuata ili kudhibiti tatizo ni

1) BADILISHA MFUMO WAKO WA CHAKULA

Utafiti unaeleza waathirika wengi wanaopatwa na tatizo hili ni wale waliothirika na lishe mbovu ambao wanasumbuliwa na uzito mkubwa sana na uzito mdogo sana hali inayopelekea watu hao husumbuliwa na tatizo la homoni kutokua katika uwiano sawia PCOS.
kama yalivyo magonjwa mengine yanayohusiana na lishe bora hivyo hivyo ili mtu aweze kujitibia na kudhibiti kuendelea kuota ndevu na vinyweleo na chanzo cha tatizo lake ni kutokua na uwiano sawa wa homoni atatakiwa kubadilisha mfumo wake wa chakula ili kuweza kutatua matatizo hayo kwa kupungKup uzito mkubwa au kubalansi uzito wake kuwa katika uwiano wa usawa na umri wake

Hapa chini kuna vidokezo vichache vya lishe bora ili kupambana na tatizo hili

Unashauriwa kujitahidi kula mboga mboga za majani kwa wingi na vyakula vilivyomo katika kundi la PROTEINS kama vile nyama,kuku,samaki,mayai,karanga,korosho nk kila siku itasaidia kusawazisha sukari iliyopo katika damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini na hivyo kusaidia kurekebisha mfumo wa homoni

Epuka kabisa kula vyakula vilivyopo katika kundi la Carbohydrates kama vile ugali,wali,viazi,chips,chapati,maandazi,mihogo nk 

Pendelea kunywa maji na maziwa kwa wingi na Epukana na sukari sababu sukari ndio adui yetu namba moja katika kusababisha magonjwa mengi

 Ukizingatia hiyo lishe utapungua mwili wako ikiwa wewe ni mnene na itakusaidia kupambana na tatizo la PCOS na kudhibiti kuendelea kuota kwa ndevu na vinyweleo.


2)ONDOA NA EPUKANA NA MAWAZO AU MFADHAIKO

Huenda ukashangaa hili ukajiuliza  mawazo yanahusiana vipi na tatizo la kuota ndevu, lakini ukweli ni kwamba tezi zetu za adrenal hushughulika Sana kuzalisha homoni ya adrenal mtu anapopatwa na mfadhaiko pia. Tunapokuwa na mawazo sana kuhusu watoto, mambo ya kifedha au mahusiano na hata kitu kingine chochote, tunaunda homoni za mfadhaiko zaidi.
Homoni za mfadhaiko kama cortisol huathiri vibaya udhibiti wa sukari katika damu ambapo huathirika katika hali tofauti na mfadhaiko usio dhibitiwa huweza kusababisha kuongezeka kuzalishwa kwa  homoni za androjeni, haswa DHEAS.
Homoni za Adrojeni kama hizi zinaweza kubadilishwa kuwa DHT, fomu yenye nguvu zaidi ya homoni ya testosterone katika kiwango cha tishu ambayo huchochea chunusi, kuotwa na ndevu na vinyweleo na kupuputika kwa nywele kichwani

Mambo unayoweza kufanya kuondokana na mfadhaiko na mawazo

Fanya mazoezi ya yoga ya kila siku

Pendelea kutafakari na kutambua utukufu na ukubwa wa mwenyezimungu ambaye amekuumba wewe na viumbe vyote vilivyopo ulimwenguni.

Kunywa chai ya kutuliza mfadhaiko na mawazo kama lavender, chamomile, lemon, tulsi nk
Changanyikana na marafiki zako epuka kujitenga
Shiriki tendo la ndoa mara kwa mara ikiwa tayari umeolewa
Pendelea kula vyakula vyenye Omega 3 na vitamins nyingi

3)EPUKA KUJIDHURU NA KEMIKALI TUMIA VITU VYA ASILI KUDHIBITI VINYWELEO

Badala ya kuhangaika kutafuta dawa zenye kemikali  kuondoa ndevu au vinyweleo usoni
Faham tiba rahisi na nzuri za nyumbani zinazoweza kukusaidia kuondoa vinyweleo usoni

1)PAPAI NA MANJANO


Tengeneza mchanganyiko wa papai na manjano ili kudhibiti kuendelea kuota kwa ndevu na vinyweleo mwilini
Chukua bakuli andaa vipande vinne vya papai,vijiko viwili vya unga wa manjano(tumeric powder) vichanganye vizuri upate uji mzito wa mchanganyiko huo kisha jipake mahali palipoota vinyweleo visivyohitajika
Acha kwa dakika 20 hadi ukauke na kubakia mkavu kisha jibandue kwa kusugua ili kuzuia kuota kwa vinyweleo tena
Kupata matokeo mazuri fanya hili zoezi kwa week mara 3

2)LIMAO NA ASALI

Kamua juisi ya limao changanya na asali  vijiko viwili koroga hadi upate uji mzito kisha paka sehemu iliyoota vinyweleo na kaa kwa dakika 15_20 ujibandue kwa kusugua ili kuondoa nywele zilizopo na kudhibiti kuendelea kuota vinywele
Kupata matokeo mazuri fanya hili zoezi kila siku kabla hujaingia kulala

3) KITUNGUU THAUMU NA CHUMVI

Chukua punje kumi za kitunguu thaumu ziponde pamoja na kitunguu thaumu kisha jisugulie mahali penye vinyweleo na kaa kwa dakika 15 kisha nawa na maji safi na jikaushe kwa kitambaa
Kitunguu thaumu kinasaidia kuzuia kuendelea kuota kwa vinyweleo na kufanya ndevu na vinyweleo kupotea
Kupata matokeo mazuri fanya zoezi hili kila siku

4)MSHUBIRI (ALOE VERA) NA PAPAI

 Chukua vipande vinne vya papai liloiva kisha changanya na ute ute wa mshubiri (aloe vera)
Visage hadi upate uji mzito kisha paka sehemu iliyoota vinyweleo na sugua taratibu ili kuzuia kuendelea kuota vinyweleo hivyo kisha kaa kwa dakika 15 nawa na maji safi kisha jifute kwa taulo safi
Kupata matokeo mazuri fanya zoezi hili kila siku kabla hujaingia kulala

Mpendwa msomaji hizo hapo juu ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kujitibia au kudhibiti kuendelea kuota ndevu na vinyweleo mwilini

Noted;

Matibabu ya tatizo hili huchukua muda mrefu kidogo takriban miezi 3 hadi miezi 6 kulingana na vyanzo vya tatizo hili kutofautiana uzito katika matibabu


MATIBABU YA TATIZO HILI LA HIRSUTISM NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER


Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la hirsutism na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)


Green health consultation center tutakufanyia uchunguzi kujua chanzo cha tatizo kisha tutakupatia dawa za kuondoa hirsutism na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana ofisini kwetu tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud ) 

0 comments:

FAHAMU SULUHISHO LA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA KWA KUHOFIA KUNENEPA (ANEROXIA NERVOSA) NA MADHARA YAKE

TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA KWA KUHOFIA KUNENEPA (ANEROXIA NERVOSA)





Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,
Tunakuombea afya njema zaidi wewe pamoja na familia yako na wote unaowapenda
MWENYEZIMUNGU MTUKUFU AZIDI KUWAHIFADHI NA KUWAJAALIA REHMA ZAKE 
AMEEN!

Naam leo nimeona ni khery tukaongelea juu ya mada hapo juu kutokana na athari tunayoiona katika jamii zetu kwa watu wengi kuathirika kisaikolojia kwa kukosa hamu ya kula kwa kujinyima kwao kula kwa hoja ya kuhitaji kuwa wembamba zaidi kwa kujiona kua wao ni WANENE WENYE UZITO MKUBWA Jambo ambalo sio la kweli isipokua fikra zao ndio zenye kuwatuma kujiona hivyo.



Je, TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA KWA KUHOFIA KUNENEPA (ANEROXIA NERVOSA) NI TATIZO GANI?

Hili ni tatizo la kukosa kabisa hamu ya kula na kumfanya mtu apungue sana uzito kutokana na kuathirika kisaikolojia kwa dhana ya kuogopa kula kwa kuhofia kunenepa au kuongezeka uzito na kujihisi au kujiona kuwa yeye ni MNENE wakati kiuhalisia ni mwembamba.
Watu wanaopata zaidi tatizo hili ni wale waliokusudia hasa kwa dhati kujinyima kula ili wapungue uzito na mwili kuwa mwembamba hivyo hujinyima kula kwa kiasi kikubwa kwa kujihisi kuwa wana uzito au miili mikubwa au kujihisi wanene
Hali ambayo huwapelekea kujibiidiisha au kuhangaika kwa kila njia kwa kujinyima kula na kunywa,kutumia dawa za Kupunguza mwili na hamu ya kula,kwa kujitapikisha baada ya kula,kufanya mazoezi makali ili mradi tu wapungue mwili bila ya kujali au kutambua ni kiasi gani cha uzito alionao yeye bado huhofu kuhusu uzito wake

Tatizo hili la kujihisi unene ni tatizo la kuathirika kisaikolojia zaidi kwani tunaposema fulani ni mnene lazima upime “BMI” ambayo ni uwiano wa uzito na urefu.
Hivyo ni vema ukajifahamu ‘BMI’ yako ikoje kabla ya kuanza kupanga utaratibu wa kupunguza uzito.


Ifahamike kuwa Uzito mkubwa kupita uwezo wa mwili wako ni tatizo, na uzito mdogo kuliko mwili wako unavyostahili pia ni tatizo hasa katika mfumo wako mwilini na taswira yako kwa nje kimuonekano (appearance)



Chanzo Cha tatizo



Chanzo Cha tatizo hili hasa hakijajulikana kama yalivyo magonjwa mengine.
Isipokua tafiti zimeonyesha kua Kupoteza hamu ya kula kunasababishwa na mambo mbalimbali, mojawapo ni kutokana na muendelezo wa kuzoea kujinyima chakula, t,atizo la kiugonjwa na inaweza kuwa hali ya kurithi.
Lakini pia chanzo halisi mbali ya hilo la kukusudia kujinyima bado hakijulikani rasmi lakini inaweza kuwa matatizo ya kimwili, matatizo ya kisaikolojia na matatizo ya kijamii kutegemea na aina ya vyakula vinavyopatikana katika jamii husika.

Katika tatizo la kimwili ambapo kitaalam tunasema ‘Physiological’ hali ya kuvurugukika kwa mfumo wa kichocheo cha ‘Serotonin’ huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa

Tatizo hili pia hurithiwa endapo katika familia kuna watu wa aina hiyo wasiopenda kula.

Wanawake wajawazito huweza kuathirika na tatizo hili la kupoteza hamu ya kula kutokana na hali ya ujauzito na kusababisha apate tatizo la upungufu wa damu, kisukari, kifafa cha mimba, matatizo katika kondo la nyuma na matatizo kwa mtoto aliye tumboni na hata mtoto akishazaliwa.

Wengine wanaopatwa na tatizo hili ni wagonjwa hasa wale wenye homa kama malaria au wenye matatizo katika mfumo wa chakula. Watu wenye magonjwa sugu au wanaotumia dawa kwa muda mrefu pia hupatwa na tatizo hili.

DALILI ZITAKAZOKUJULISHA KUWA UNA TATIZO HILI


Dalili zitakazokujulisha kama una tatizo hili ni Mtu hupoteza hamu ya kula, wengine kupoteza hamu ya kula hata kwa kutumia dawa ili kupunguza mwili au kujipunguza uzito hali kuwa wala yeye si mnene au mwenye kuhitajika Kupunguza uzito
 Mtu anapojinyima kula lengo ni kujikondesha na kujikondesha pasipo kufuata maelekezo ya kitaalamu kuna madhara kiafya kama tutakavyokuja kuyabainisha huko mbele

Mtu anayejikondesha anaweza kuwa na dalili za utapia mlo kama vile ngozi kuzeeka na kunyauka, mifupa ya usoni, mabega kujitokeza na mbavu kuhesabika kirahisi, kuchoka mara kwa mara na mwili kukosa nguvu, misuli kukaza na baadhi ya viungo vya mwili kuathirika mfano ubongo, moyo na figo hata ini.

Tatizo hili la kujikondesha kwa makusudi au kutokana na maradhi humfanya mtu apate tatizo la kiafya liitwalo ‘Hypokalaemia’  na madini ya ‘potassium’ mwilini hupungua, hivyo hulalamika mapigo ya moyo kutokwenda vizuri, kufunga kupata choo kikubwa, uchovu wa mwili na wakati mwingine mwili kupooza.

Dalili nyingine ni kupoteza kabisa hamu ya kula, kufunga kupata hedhi, nywele kichwani kuwa nyepesi, shinikizo la damu hushuka na kuhisi moyo kwenda mbio wakati wa kuongea au kutembea, kuwa na msongo wa mawazo, tumbo kujaa gesi na kutoa harufu mbaya ya mwili, ngozi huwa kavu na ngumu.


UCHUNGUZI WA VIPIMO


Vipimo vya uchunguzi wa tatizo hili hufanywa pale daktari wako anapohisi kwamba una tatizo la anorexia nervosa, kwa kawaida atafanya majaribio kadhaa na uchunguzii kusaidia kubaini tatizo,ili atoe sababu za matibabu kwa kupoteza uzito, na huangalia shida zozote zinazohusiana kwa kufuata hatua zifuatazo za kiuchunguzi

Uchunguzi wa Kimwili.
Hii inaweza kujumuisha kupima urefu na uzito wa mgonjwa na kuangalia ishara zote muhimu, kama kiwango cha moyo, shinikizo la damu na joto; kuangalia rangi ya ngozi na kucha,kusikiliza mapigo ya moyo  na mapafu na kuchunguza tumbo lako.

Vipimo vya maabara.
Hatua hii inaweza kujumuisha kufatilia hesabu kamili ya damu (CBC) na vipimo maalum vya damu ili kuona wingi wa damu na protini na utendaji wa ini yako, figo na tezi.


Tathmini ya kisaikolojia.
Daktari au mtaalamu wa afya ya akili atauliza juu ya mawazo yako, hisia na tabia ya kula kwako. Unaweza pia kuulizwa kukamilisha maswali ya uchunguzi wa kisaikolojia ya kujitathmini.

Vipimo vingine.
Kipimo cha X ray kinaweza kuchukuliwa ili kuona uwiano wa mifupa yako, kuangalia kupunguka kwa mfadhaiko au mifupa iliyovunjika, au kuangalia shida ya pneumonia au ya moyo.


MATIBABU


Matibabu ya anorexia kwa ujumla hufanywa kwa kutumia mbinu ya timu, ambayo ni pamoja na madaktari, wataalamu wa afya ya akili na wale wa lishe, wote wenye uzoefu wa shida za kula. Kuendelea na matibabu na lishe ni muhimu sana kwa kuendelea kupona.

Kuna hatua nyingi za kufuata ili kuweza kupata tiba sahihi ya tatizo la aneroxia nervosa

1)Mipango ya hospital

Ikiwa maisha ya mgonjwa  yako katika hatari ya haraka, unaweza kuhitaji matibabu katika chumba cha dharura cha hospitali kwa maswala kama moyo kuvurugika, upungufu wa damu, ukosefu wa usawa wa umeme au dharura ya akili.
Kulazwa hospitalini kunaweza kuhitajika kwa shida za kimatibabu, shida kali za akili, utapiamlo mzito au kuendelea kukataa kula.

Kliniki zingine huratibu Mipango katika kutibu watu wenye shida ya kula. Wanaweza kutoa mipango ya siku au mipango ya makazi badala ya kulazwa hospitalini kamili. Programu maalum za shida ya kula zinaweza kutoa matibabu zaidi kwa muda mrefu zaidi.


2)Huduma ya matibabu

Kutokana na athari za tatizo la anorexia, mgonjwa anaweza kuhitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kutizama kiwango cha upumuaji, pamoja na mabadiliko mengine ya mwili. Katika hali mbaya, watu walio na anorexia hapo awali wanaweza kuhitaji kulishwa kupitia bomba ambalo limewekwa kwenye pua zao na huenda kwenye tumbo


3)Kurejesha uzito wenye afya

Lengo la kwanza la matibabu ni kurudi kwenye uzito wenye afya. Hauwezi kupona mwenye tatizo la aneroxia nervosa bila kurudi kwenye uzani mzuri na kujifunza lishe sahihi. Wale wanaohusika katika mchakato huu wanaweza kujumuisha:

Daktari wako wa huduma ya msingi, anayeweza kutoa huduma ya matibabu na kusimamia mahitaji yako ya kalori na kupata uzito

Mtaalam wa saikolojia au mtaalamu mwingine wa afya ya akili, anayeweza kufanya kazi na wewe kuunda mikakati ya tabia kukusaidia kurudi kwenye uzito wenye afya

Mtaalam wa chakula, anayeweza kutoa mwongozo wa kurudi kwenye hali ya kawaida ya kula, pamoja na kutoa mipango maalum ya chakula na mahitaji ya kalori ambayo hukusaidia kufikia malengo yako ya uzani

Familia yako, ambayo itahusika katika kukusaidia kudumisha tabia ya kawaida ya kula

4)Ushauri na tiba ya kisaikolojia

Aina hii za tiba za tiba zinaweza kuwa na faida kwa anorexia:

Tiba inayotegemea familia. Hii ndio matibabu ya msingi kwa ushahidi kwa vijana wenye anorexia. Kwa sababu kijana mwenye anorexia haiwezi kufanya maamuzi mazuri juu ya kula na afya wakati yuko katika hali hii mbaya, matibabu haya huwahamasisha wazazi kumsaidia mtoto wao kwa kulisha tena na kurejesha uzito hadi mtoto aweze kufanya uchaguzi mzuri juu ya afya.

Tiba ya mtu binafsi. Kwa watu wazima, tiba ya tabia ya utambuzi - tiba ya tabia ya utambuzi iliyoimarishwa - imeonyeshwa kusaidia. Lengo kuu ni kurekebisha mitindo ya tabia ya kula na tabia ili kuunga mkono kupata uzito. Lengo la pili ni kusaidia kubadili imani na mawazo yaliyopotoka ambayo yanadorora kula chakula

5)Dawa

Hospital hakuna dawa ya Moja kwa moja iliyopitishwa kutibu anorexia kwa sababu hakuna iliyopatikana kufanya kazi vizuri. Walakini, antidepressants au dawa zingine za akili zinaweza kusaidia kutibu shida zingine za afya ya akili ambazo unaweza kuwa nazo, kama unyogovu au wasiwasi na kukosa usingizi.

Madhara 


Tatizo la kukosa hamu ya kula kama tulivyoona mtu hukonda na unapofikia hali hiyo unaharibu mifumo mbalimbali ya mwili na hukufanya uwe mgonjwa. Mfumo ambao huathirika zaidi na kuonesha dalili za wazi ni mfumo wa uzazi kwa mwanaume na mwanamke.

Mwanaume hupoteza uwezo wa kufanya tendo la ndoa kutokana na matatizo mbalimbali ya mfumo wa mwili yanayotokana na upungufu wa lishe bora.

Mwanamke hupoteza hedhi, hupoteza uwezo wa kuzaa na hamu ya tendo la ndoa na hata wakati wa tendo.

Uwezo wa kuzaa unapotea ndipo tunaposema ugumba, hapa vichocheo au homoni za uzazi huvurugika na kupungua kwa kiasi kikubwa.

Madhara mengine ya anorexia ni pamoja na:

Mtu kupata ugonjwa wa Anemia

Matatizo ya moyo, kama prolapse of mitral valve, mitindo ya moyo isiyo ya kawaida au kufeli kwa mishipa ya moyo

Kupotea kwa mfupa (osteoporosis), na kuongeza hatari ya kupunguka mifupa

Kupoteza misuli

Kukosa usingizi na kupata mfadhaiko

Vidonda vya tumbo, kusumbuliwa na hali za kukera Kama kuvimbiwa kutokwa na damu au kichefuchefu

Kupungua kwa potasiam chini ya damu, sodiamu na kloridi

Matatizo ya figo


Noted

Epuka kujipunguza uzito bila ya kuwa na elimu fuata ushauri wa daktari kama unahisi uzito wako ni mkubwa na unataka kupungua ili kuepuka matatizo.

Mwanamke au mwanaume aliye katika mpango wa kuzaa inampasa azingatie kanuni bora katika uzito unaostahili ili aweze kupata mimba haraka au aweze kumpa mwanamke ujauzito katika kipindi muafaka.

Uzito mkubwa kupita uwezo wa mwili wako ni tatizo, na uzito mdogo kuliko mwili wako unavyostahili pia ni tatizo hasa katika mfumo wako wa uzuri

Je,unawezaje KUJIKINGA na tatizo la anorexia nervosa?


Huenda ukawa na shauku ya kujua jinsi unavyoweza kujikinga dhidi ya tatizo hili ambalo lina madhara makubwa lakin kwa bahati mbaya hakuna njia iliyohakikishwa ya kuzuia tatizo hili la anorexia nervosa. Madaktari wa utunzaji wa kimsingi (watoto, waganga wa familia na wafizi wa masomo ya ndani) wanaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kutambua viashiria vya mapema vya anorexia na kuzuia ukuaji wa ugonjwa uliopigwa kabisa. Kwa mfano, wanaweza kuuliza maswali juu ya tabia ya kula na kuridhika na kuonekana wakati wa miadi ya matibabu ya kawaida.

NOTED;

IWAPO utagundua kuwa mtu wa familia au rafiki yako ana tabia ya kutopenda kula na kuhofia kunenepa licha ya kuwa ni mwembamba ila anajiona ni mnene Fikiria kuzungumza naye kuhusu maswala haya na msaidie juu ya kupata matibabu



MATIBABU YA TATIZO LA ANEROXIA NERVOSA NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo hili au ndugu yako ana hili tatizo la ANEROXIA NERVOSA na magonjwa mengine mbalimbali na umejaribu njia kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tutakupatia dawa za kuondoa tatizo la anorexia nervosa na tutakupatia ushauri sahihi wa kupambana na ugonjwa huo na magonjwa yote yanayokusumbua karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )


0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre