MZUNGUKO WA HEDHI,NAMNA YA KUFAHAM UREFU WA MZUNGUKO WA HEDHI NA SIKU ZA KUPATA UJAUZITO( MENSTRUATION CYCLES)
FAHAMU MAANA YA MZUNGUKO WA HEDHI,NAMNA YA KUFAHAM UREFU WA MZUNGUKO WAKO NA SIKU ZAKO ZA HATARI
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Ni matumaini yetu sote tunaendelea vyema kwa uwezo wake mwenyezimungu,walio wagonjwa na wenye matatizo Allah awajaalie wepesi katika matatizo na awape afya njema Ameeen.
Mpendwa msomaji wetu leo tunaangalia na kujifunza maana ya mzunguko wa hedhi na kuangalia namna gani tunaweza kujua siku bora ya kupata ujauzito,
Nianze kwa kusema wengi tunafahamu kuwa mzunguko wa hedhi wa mwanamke ni siku 28 na misemo mingi imekuwa ikitumika ikihusisha mzunguko huo na mwezi wa kalenda wa mwaka. Misemo kama kwenda mwezini, kuingia mwezini n.k. ni ya kawaida kuisikia. Jee, ulishawahi kudadisi uhusiano wa siku 29.5 za mwezi na mzunguko huu wa hedhi unaochukua siku 28? Tupate nadharia fupi:
Kama inavyojulikana kuwa jua na mwezi vina mchango katika maisha ya mimea na binadamu, homoni za binadamu hutolewamwilini kulingana na kiwango cha mwanga wa mwezi. Kabla ya ugunduzi wa umeme, utendaji kazi wa miili ya binadamu ulitegemea sana kiwango cha mwanga wa mwezi. Na akina mama wote walipata hedhi kwa wakati mmoja. Maisha ya sasa ambapo kuna vyanzo vingi vya mwanga usiku na mchana, mizunguko ya hedhi ya akina mama haiendani tena na uwepo wa mwanga wa mwezi.
Lakini hedhi ni nini na kuna uhusiano gani kati ya mzunguko wa hedhi wa mwanamke na siku za kubeba mimba mwanamke au kwa maneno mengine, katika mzunguko huo ni zipi siku ambazo mwanamke anaweza kupata mimba? Hayo ndiyo maswali ambayo yanawasumbua watu wengi kichwani nasi leo tutajaribu kuyajibu katika makala hii
Mzunguko wa hedhi ni mfululizo wa mabadiliko katika mwili wa mwanamke katika kujiandaa kwa mimba ambayo inaweza ikatungwa. Kila mwezi ovari zinaachia yai moja lililokomaa (ovulation) na homoni katika mwili hubadilika kila wakati ili kuiandaa nyumba ya uzazi (uterus) kwa mimba itakayotungwa. Endapo yai lililoachiwa halitarutubishwa, ile ngozi nyororo inayotanda juu ya nyumba ya uzazi hujinyofoa na kutoka nje ya uke, na tendo hili ndilo linaloitwa hedhi yani mwanamke kutokwa na damu ya mwezi ukeni(menstruation).
Kuwa na mzunguko wa hedhi unaoeleweka ni ishara kuwa viungo muhimu katika mwili wa mwanamke vinafanya kazi vizuri.
Mzunguko wa hedhi huhesabiwa kutoka siku ya kwanza ya kuanza kutoa damu (period) hadi siku ya kwanza ya kutoa damu ya mwezi unaofuata.
Mzunguko wa hedhi huchukua wastani wa siku 28 lakini kila mwanamke ana tofautiana na mwingine. Mizunguko ya mwezi
huweza kuchukua kati ya siku 21 hadi 35. Msichana anapoanza kupata hedhi mizunguko yake huwa mirefu, isiyotabirika – na si ajabu akakosa kupata siku zake kwa kipindi fulani. Kadri umri wake unavyoongezeka, mizunguko yake hupungua siku na kuwa mifupi na inayotabilika zaidi.
Mzunguko wa mwezi wa mwanamke unaweza kujirudia kwa vipindi vilivyo sawa au vilivyo na urefu wa siku tofauti, damu inaweza kutoka kwa wingi au kidogo, ikaambatana na maumivu au isiwe na maumivu. Vyote hivi ni vitu vya kawaida kwa mwanamke, – “mzunguko wa kawaida kwa mwanamke ni ule aliouzoea.” Tunasema kuna mabadiliko au kuna matatizo katika mzunguko wa hedhi wa mwanamke pale mambo yanapokwenda tofauti na alivyoyazoea mwanamke mwenyewe katika mwili wake. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kuvurugika kwa mzunguko wa mwezi wa mwanamke. Baadhi ya sababu hizo ni kama zifuatazo:
Kubadili Njia Ya Mpango Wa Uzazi:Kubadili njia ya mpango wa uzazi kutoka moja hadi nyingine kunaweza kuvuruga mzunguko wa hedhi.
Kukosa Uwiano Wa Homoni: Ni kawaida kwa mwanamke kukosa uwiano mzuri wa homoni za estrogen na progesterone miaka michache baada ya kuvunja ungo na kabla ya kukoma hedhi. Hali hiyo huweza kusababisha mzunguko wa hedhi kuwa mrefu au mfupi na kutokwa na damu kidogo au nyingi kupita kiasi wakati wa hedhi.
Ujauzito Au Kunyonyesha: Kuchelewa kupata au kukosa hedhi ni dalili ya awali ya ujauzito. Kunyonyesha kwa kawaida humzuia mwanamke kurudia kuanza kupata siku zake baada ya mimba.
Matatizo Ya Ulaji, Mazoezi Mazito Au Kupungua Mwili: Matatizo katika ulaji wa chakula, kupungua uzito kwa kiwango kikubwa na kuongezeka kwa shughuli nzito za mwili huweza kusimamisha mzunguko wa hedhi.
Polycystic Ovary Syndrome (PCOS): Hii ni hali inayoweza kutokea ambapo vifuko vidogo vilivyojaa majimaji (cysts) huota kwenye ovari. Dalili ya Polycystic ovary syndrome ni kupata hedhi zisizotabilika au hedhi fupi au kukosa kabisa hedhi. Hii ni kwa sababu mwanamke mwenye PCOS hawezi kutoa yai (ovulation) kila mwezi kama inavyotakiwa. Utengenenezaji wa homoni zake unaweza kuwa hauna uwiano unaotakiwa, na pengine kukawa na kiwango kikubwa mno cha testosterone.
Ovari Kuacha Kufanya Kazi Mapema – Premature Ovarian Failure: Hili ni tatizo ambapo ovari huacha kufanya kazi kama inavyotakiwa kwenye umri unaopungua miaka 40. Wanawake wenye tatizo hili huweza kuwa na siku ambazo hazitabiriki kwa kipindi kirefu cha maisha yao.
Pelvic Inflammatory Disease (PID):Maambukizi ya wadudu kwenye viungo vya uzazi huweza kumsababishia mwanamke apate hedhi zisizotabirika.
Uterine Fibroids: Uvimbe ulioota katika nyumba ya uzazi husababisha damu kutoka kwa wingi wakati wa hedhi na
kutokwa damu katikati ya hedhi.
Matatizo Ya Tezi Ya Thyroid: Tezi ya thyroid ambayo hupatikana katika eneo la shingo la binadamu hutoa homoni za kusimamia mwenendo wa kemikali zinazobadili chakula na kuleta nguvu katika mwili. Mabadiliko ya kiwango cha thyroid – kuwa na kiwango kidogo cha thyroid (hypothyroidism) katika mwili – huweza kusababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi.
Kipindi hiki cha mzunguko huu wa hedhi kinagawanyika katika awamu nne zinazoongozwa na kupanda na kushuka kwa homoni katika mwili. Mwanamke kwa wastani hupitia mizunguko ya hedhi 450 katika maisha yake. Hapa chini tutaziona awamu hizo nne na kuelezea ni nini kinachotokea katika mwili wake katika kila awamu. Hapa chini tunazijadili awamu hizo nne za mzuguko wa hedhi:
HEDHI-KUMWAGA DAMU (THE BLEEDING PHASE)
Hedhi (menstruation) ni tendo linalotokea kila mwezi kwa mwanamke ambalo linahusisha utokwaji wa damu na vitu
vingine vilivyokuwa vinajijenga kwenye tumbo la uzazi, kupitia sehemu ya uke.
Msichana wa kawaida huanza kupata siku zake akiwa na umri wa miaka 12, hii ni wastani na haina maana wote wataanza kupata siku katika umri huo. Wapo wasichana wanaoanza kuona siku zao kwenye umri mdogo sana wa miaka 8 na wapo wanaochelewa hadi kwenye umri wa miaka 15. Mara nyingi wasichana huanza kuona siku zao miaka 2 baada ya maziwa (matiti) kuanza kuota.
Mwanamke anapoingia mwezini, utando uliokuwa umejijenga kuzunguka nyumba ya uzazi (uterus) pamoja na damu ya ziada
hutoka nje ya mwili kupitia sehemu ya uke. Utokaji huo wa vitu hivi unaweza kuwa unaolingana kila mwezi au ukawa tofauti mwezi hadi mwezi. Utokaji huo huweza kuwa tofauti kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine. Damu inaweza kutoka kwa kiasi kidogo au nyingi na urefu wa hedhi (siku za kutoka damu) zinaweza kuwa tofauti kutoka mwezi mmoja hadi mwingine. Kwa kawaida mwanamke hutokwa damu kwa siku 3 hadi 5, lakini siku 2 hadi 7 bado inachukuliwa kuwa ni kawaida.
THE FOLLICULAR PHASE
Hormone Releasing Factor (FSH-RF) ambayo itaiamuru tezi ya pituitary kutoa homoni iitwayo Follicle Stimulating Hormone (FSH) na kiasi kidogo cha homoni ya Leutenizing Hormone (LH). Utolewaji wa homoni hizi katika damu husababisha vifuko vya mayai (follicles) kukomaa.
Vifuko vya mayai vikianza kukomaa vitatoa homoni nyingine iitwayo estrogen. Kadiri vifuko hivi vinavyozidi kukomaa katika siku saba, homoni ya estrogen hutolewa zaidi na zaidi. Pamoja na estrogen, testosterone homoni ya aina nyingine huongezeka katika damu. Kuongezeka kwa homoni hizi mbili huufanya mwili kupata nguvu na ufanyaji kazi wa ubongo huboreshwa. Mwanamke atasikia hali ya kujiamini na mwenye kupenda kuthubutu. Kuongezeka kwa testosterone kutamfanya ajisikie kupenda kufanya mapenzi wakati oestrogen itamfanya apende kuwa mtu wa kutoka na kuonekana
wakati huo hamu ya kula ikipungua. Ni kipindi cha kusikia ukamilifu na bora kwa kufanya maamuzi na kuthubutu mipango mikubwa na migumu.
Homoni ya estrogen huifanya ngozi nyororo inayotanda juu ya nyumba ya uzazi (uterus) kuwa nene na kuleta mabadiliko kwenye ute wa mwanamke (cervical mucous). Kiwango cha estrogen kikifikia kiasi fulani, hypothalamus hutoa Leutenizing Hormone Releasing Factor (LH-RF) ambayo itaifanya tezi ya pitutary kutoa kiasi kikubwa cha Leutenizing Hormone (LH). Tendo hili hukifanya kifuko cha yai kilichokomaa kupita vyote kupasuka na kuachia yai.
THE OVULATORY PHASE
Yai linapokaribia kuachiwa, kiwango cha damu kinachopelekwa kwenye ovari huongezeka na misuli inayoshikilia ovari hujikunja ili kusogeza ovari karibu na mrija wa uzazi (fallopian tube), kulifanya yai litakaloachiwa kuingia kirahisi ndani ya mrija wa uzazi. Muda mfupi kabla ya yai hili kuachiwa, mlango wa uke (cervix) hutoa ute kwa wingi. Ute huu unaonata huasidia mbegu za kiume kusafiri kuelekea kwenye yai. Baadhi ya wanawake hutumia ute huu
kama ishara ya siku ambazo wanaweza kupata ujauzito.
Yai likiwa ndani ya mirija ya uzazi husafirishwa kwa kutumia namna ya vijinywele viitwavyo “cilia” kuelekea kwenye nyumba ya uzazi (uterus). Yai hili litarutubishwa endapo kutakuwa na mbegu za kiume.
Tofauti na mwanamme ambaye hutengeneza mbegu za kiume kila siku na kwa karibu muda wote wa maisha yake, mwanamke
anazaliwa na mayai yake ndani ya vikapu vyake miwili – ovari. mwanamke huzaliwa na mayai yake haya machanga yapatayo milioni moja hadi mbili ndani ya ovari. Katika maisha yake mayai mengi hufa, kuanzia anapokuwa mchanga, na hubakia na mayai yapatayo 400,000 anapofikia kuvunja ungo. Kila anapoingia mwezini, mayai yapatayo 1,000 hupotea na ni moja tu linalofikia kukomaa (ovum) na kuachiwa liingie ndani ya mrija wa uzazi. Katika mayai yake yote milioni moja au ambili aliyozaliwa nayo, ni mayai kama 450 tu yatakayofikia kukomaa.
Ni kiasi kidogo sana cha follicles kitakuwa kimebakia mwanamke huyu anapofikia kukoma hedhi hali ambayo kwa wanawake wengi hutokea kwenye miaka kati ya 48 na 55. Hata hivyo follicles hizi si rahisi kukomaa tena na kutoa mayai kutokana na mabadiliko ya homoni yanayoendana na kukoma kwa hedhi.
The luteal pHASE
Siku 2 hadi 3 baada ya yai kutolewa, viwango vya estrogen na testosterone vitaanza kushuka katika damu na homoni ya progesterone kuanza kutengenezwa. Progesterone ni homoni inayopunguza wasiwasi katika mwili hivyo kuufanya mwili kuwa tulivu. Katika siku zinazofuata, wanawake wengi hujisikia vibaya kutokana na Premenstrual Syndrome (PMS), tatizo ambalo limejulikana kwa miaka mingi.
Premenstrual Syndrome ni jumla ya matatizo yanayowapata wanawake na kuwafanya wajisikie vibaya kutokana na viwango
vya homoni kuwa juu kabla, na wakati mwingine, wakati wakiwa katika hedhi.
Aina moja ya PMS hujionyesha kwa mwanamke kuwa na wasiwasi, kuna na hasira na asiyetabirika. Mara nyingi hali hiyo hupotea mara baada ya kuingia kwenye siku zake. Hii inaweza kutokana na uwiano wa estrogen na progesterone. Estrogen ikizidi, wasiwasi hutanda na progesterone ikizidi, hali ya kuwa na mfadhaiko hujionyesha.
Aina nyingine ya PMS ni kupenda sana sukari (chocolate, mikate , wali mweupe n.k.), uchovu wa mwili na maumivu ya kichwa. Hii inaweza kuwa inatokana na mwili kuongeza usikivu wa insulin unaotokana na kuongezeka kwa viwango vya homoni kabla ya hedhi.
Wakati huu kuna mabadiliko yanayotokea kwenye uterus na ovari. Kile kifuko kilichotoa yai hubadilika rangi na kuwa cha njano “corpus luteum.” Kifuko hiki kinavyoendelea kupona, kinatoa homoni ya estrogen na kiwango kikubwa cha progesterone, homoni muhimu katika utunzaji wa mimba. Hapo baadaye endapo mimba haikutungwa, kifuko hiki hubadilika rangi na kuwa cheupe ” corpus albicans”.
Homoni ya progesterone huifanya ngozi laini inayotanda juu ya uterus (endometrium) kufunikwa na ute, unaozalishwa na tezi zilizopo katika ngozi hiyo. Kama yai halikurutubishwa na mimba kutungwa, arteri za kwenye ngozi nyororo ya juu ya uterus hujifunga na damu kusitishwa kuelekea kwenye ngozi hiyo. Vijibwawa vya damu katika veni hupasuka, pamoja na utando wa endometrium, hutoka nje ya mwili na kuwa ndiyo mwanzo wa hedhi. Urefu wa hedhi hutofautiana baina ya wanawake na hubadilika katika maisha yao.
JINSI YA KUFAHAMU UREFU WA MZUNGUKO WAKO NA SIKU ZA KUPATA UJAUZITO(SIKU ZA HATARI)
Ili kufahamu vizuri ni siku zipi ni hatari kwa mwanamke kupata mimba, unahitaji kwanza kujifunza jinsi mzunguko wa hedhi (menstrual cycle) unavyofanya kazi.
Kwa wastani, mzunguko wa hedhi huwa ni siku 28.
Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa siku ya kwanza wakati mwanamke anaanza kuona siku zake (kublidi) na tunaiita ni siku ya Kwanza.
Mzunguko wa hedhi wa kawaida huwa una sifa madhubuti zifuatazo:
1. Idadi ya siku katika mzunguko mmoja (cycle length)
Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 (na ni hapo ndipo tunapata wastani wa siku kuwa 28 yaani [(21+35)÷2].
Hivyo mpendwa msomaji wangu usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke ni siku 28. Wapo wanawake wana mzunguko wa siku 27, wengine 25, wengine 35, wengine 29.
2. Sifa ya pili ni uwiano wa idadi ya siku za mzunguko kati ya mzunguko mmoja na mwingine
Hili nalo ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la tendo la ndoa kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatari kwa mwanamke kubeba ujauzito.
Ili tuhitimishe kwamba mwanamke ana mizunguko ya hedhi iliyo sawa (regular cycles), idadi ya siku za mizunguko ya hedhi haitakiwi itofautiane kwa zaidi ya siku 7.
Mfano, kama mwezi wa kwanza uliona siku zako baada ya siku 28, mwezi wa pili ukaona baada ya siku 30, mwezi wa tatu ukaona baada ya siku 35 na mwezi wa nne ukaona baada ya siku 21, bado mzunguko wako uko kwenye uwiano mzuri (regular cycle) kwa kuwa mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.
Hivyo usikariri kwamba siku za mzunguko wa hedhi kwa kila mwanamke ni siku 28, hilo halipo. Hizi siku 28 ni wastani tu.
Wengine wanaona siku zao kila baada ya siku 21, wengine kila baada ya siku 25, wengine 29, wengine 35 na bado tunasema mizunguko yao bado ni mizunguko ya kawaida.
Pia fahamu ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyo huyo. Mfano usitarajie kuwa kama mwezi wa tatu (march) ameona siku zake baada ya siku 28 na mwezi wa nne (april) pia ataona siku zake baada ya siku 28. Si lazima itokee hivyo lakini pia huwa inaweza kutokea.
Mfano, mwanamke mmoja mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28, mzunguko unaofuata baada ya siku 27, mzunguko mwingine baada ya siku 30, mzunguko mwingine baada ya siku 29, mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa kwakuwa tofauti si zaidi ya siku 7 kama nilivyoeleza pale juu.
3. Idadi ya siku za kuona siku zake
Usichanganye kati ya siku za hedhi (menstrual period) na mzunguko wa hedhi (menstrual cycle) kwani hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.
Siku ya kwanza ya kuona siku zako ndiyo siku tunaanza kuhesabu mzunguko wako wa hedhi (day one) na siy siku ya kumaliza kuona siku zako (kublidi) kama wengi wanavyodhani.
Kawaida idadi ya siku za siku zako ni kati ya siku 3 mpaka 7. Kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo. Mwingine anaenda siku 3 amemaliza, mwingine siku 4, mwingine 5 mwingine 6 mpaka 7. Chochote zaidi ya siku 7 si cha kawaida na unahitaji kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
4. Wingi wa damu
Hii ni Sifa ya mwisho ya mzunguko wa hedhi na inaangalia kiasi cha damu inayotoka wakati wa hedhi. Hapa kuna wanawake wa aina mbili ambapo mwanamke anaweza kutoa damu ya kawaida (normal bleeding) na mwingine akatoa damu nyingi sana (heavy bleeding).
NAMNA YA KUKOKOTOA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
Soma kwa umakini maelezo haya ili uweze kukokotoa mzunguko wako wa hedhi
Ikiwa ulipata bleed tarehe 12/10/2018
Basi tarehe 12/10/2018 inakuwa siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi,
Na tarehe 13/10/2018 inakuwa siku yako ya pili ya mzunguko wa hedhi
Na teherhe 14/10/2018 inakuwa siku ya tatu kadhalika
tarehe 15/10//2018 ni siku ya 4
tarehe 16/10/2018 ni siku ya 5
.
.
Nakuendelea, utakoma kuhesabu mzunguko wako wa hedhi mara tu unapopata hedhi ingine.
Ikiwa Utapata bleed ingine tarehe 10/11/2018 Basi siku ya mwisho ya mzunguko wako wa hedhi kwa mwezi wa kumi inakuwa tarehe 09/11/2018 Na tarehe 10/11/2018 inakuwa ni siku yako ya kwanza ya mzunguko wa mwezi wa 11
ZINGATIA mwezi unaweza kuwa na siku 31,28,29 au 30 - kwa hiyo kama hujui ukubwa mbalimbali wa miezi lazima utumie kalenda yako vizuri.
Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14, kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kubleed ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa.
Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14 (luteal phase) =16, kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30, ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14 (kuwa makini hapo).
Yule mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation day ni 35-14 = 21, kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.
Sasa baada ya kuijua siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani nazo ni siku hatari pia kwasababu Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagwe[ejaculation] na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24 [one day] tangu lilipotoka kwenye ovary.
Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovary, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya ovulation ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.
Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.
Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani,siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation[narrow but dangerous window].
Kwa kuongezea,kipindi cha ovulation mwanamke anapata nyege kali sana kwasababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani[androgens] ambazo huchochea nyege huzalishwa kwa wingi. Pia kipindi hicho cha ovulation au karibia ovulation joto la mwili la mwanamke hupanda,anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.
Sasa, kwa vile nimesema kuwa hatuwezi kuwa na uhakika kwa asilimia 100 wa siku ya kushika mimba, basi tunalazimika kutumia kanuni ya kuepuka tendo la ndoa kwa muda wa wiki nzima. Ambazo ni siku zilizo karibu sana na siku ya kushika mimba (ovulation days) kwa wale wanaotumia njia ya kalenda.
Mfano, kama una mzunguko wa siku 30, kuipata siku ya ovulation chukua 30- 14=16, kwa hiyo siku ya ovulation ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza. Sasa kama ni siku ya 16, ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya ovulation.
Kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo, usishiriki tendo la ndoa.
Pia jumlisha siku 3 mbele, ambapo mwanamke atatakiwa kuanza tendo la ndoa kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba..
JEDWALI LINALOONYESHA SIKU ZA HATARI KWA MIZUNGUKO TOFAUTI
MATIBABU YA MATATIZO YA HEDHI NA MAGONJWA MBALIMBALI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER
Mpendwa msomaji Kama una tatizo lolote linalohusu hedhi,uzazi na magonjwa mbalimbali na umejaribu njia hizo kadhaa kupata tiba bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255746465095/+255657041420)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuondoa tatizo la hedhi mbovu,matatizo ya uzazi,kutoka harufu mbaya ukeni na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako
Mpendwa msomaji nina imaani umejifunza katika makala yangu hii ninashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA
GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )
4 comments: