FAHAMU CHANZO NA TIBA YA UGONJWA WA HERNIA(NGIRI KAVU)

HERNIA(NGIRI KAVU) NI NINI?FAHAMU  CHANZO NA TIBA YA HERNIA(NGIRI KAVU)


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul,mpendwa msomaji wetu
Ni matumaini yetu kuwa wewe na familia yako ni wazima wa afya,nasi tunafurahia uzima wako na tunakukaribisha katika makala yetu hii ya leo tuweze kufahamu ugonjwa wa hernia na matibabu yake.
Hernia(Ngiri Kavu) ni uvimbe uliotuna  kutokana na viungo vya ndani ya mwili kusukuma kuta za misuli inayozunguka au kushikilia viungo hivyo. Hernia hutokea wakati kuna udhaifu au kuna tundu kwenye kuta za misuli inayoshikilia na kuviweka viungo vya tumbo kwenye sehemu yake (peritoneum). Udhaifu huo unaweza kuviruhusu viungo vya ndani kusukuma na kupenyeza, na kujenga eneo lililotuna. Unaweza kuwa na hernia ikiwa unaweza kuhisi namna ya eneo laini lililotuna kwenye maeneo ya tumbo au kinena au kwenye kovu ambalo lilitokana na upasuaji. Eneo hili lililotuna linaweza likapotea ukiminya sehemu hiyo au ukijilaza. Unaweza kupata maumivu kwenye eneo hilo hasa ukikohoa, ukiinama au ikinyanyua kitu kizito.







Hernia ni tatizo linalowasumbua watu wengi katika nchi nyingi duniani. Hernia mara nyingi hutokea kwenye maeneo ya tumbo, lakini huweza pia kutokea kwenye sehemu ya juu ya mapaja, kwenye kitovu, na kwenye maeneo ya kinena. Hernia haihatarishi maisha mara moja, lakini haiwezi kuondoka yenyewe na inaweza kuhitaji kufanyika kwa upasuaji.

Hernia mara nyingi hupewa majina kutokana na sehemu ya mwili inapojitokeza, ingawa mara nyingine majina huweza kutolewa kutokana na sababu nyingine za kuitambulisha. Kila hernia hutibiwa tofauti na nyingine kutokana na sehemu iliyopo na sababu nyingine za kitaalamu. Kuwa na elimu ya kutosha ya kila aina ya hernia itakusaidia kujua namna ya kutoa maamuzi sahihi ya tiba yake.



Aina Za Hernia

Kuna aina nyingi za hernia kama zile ziitwazo kitaalamu
Inguinal hernia, umbilical hernia,femoral hernia,epigastric hernia, incisional hernia,diaphragmatic hernia nk
Pamoja na kuwepo aina nyingi za hernia watu wengi hukumbwa na inguinal hernia na umbilical hernia
Hivyo katika makala hii nitaelezea kwa kina aina hizo mbili za hernia zinazowasumbua watu wengi



1. INGUINAL (GROIN HERNIA)

Inguinal hernias au groin hernias hutokea pale utumbo au mafuta yanaposukuma na kupenya kwenye misuli ya eneo la kinena. Hii ndiyo aina ya hernia inayowasumbua watu wengi zaidi. Inguinal hernia inaweza kuonekana kwa wanaume na wanawake lakini huwapata zaidi wanaume kwa sababu tayari wana kijitundu kidogo kwenye misuli ya kinena kwa ajili ya kupitisha arteri, veni na mrija wa mbegu vinavyoelekea kwenye korodani. Asilimia 97 ya aina hii ya hernia huonekana kwa wanaume.







Hernia inaweza kuwa juu ya misuli ya tumbo (direct inguinal hernia) au inaweza ikafuata njia ya mrija wa shahawa pale unapoacha eneo la tumbo na kuelekea kwenye korodani (indirect inguinal hernia). Inguianal hernia huanza kama uvimbe mdogo ambao huongezeka na muda. Uvimbe unaoonekana ni utumbo au mafuta yanayosukuma misuli.


Uvimbe huweza kupotea kwa kulala na kurudi mwili ukianza shughuli. Uvimbe huu ukiwa mkubwa sana, huenea kutoka kwenye kinena hadi kwenye korodani zenyewe. Hernia ikiwa kubwa sana huleta matatizo kuiondoa.

2. UMBILICAL (BELLY BUTTON HERNIA)

Belly button hernia au umbilical hernia kama inavyoitwa mara nyingine, ni pale utumbo au mafuta yanapopenya kupitia sehemu dhaifu ya misuli iliyopo katikati ya tumbo chini ya kitovu. Sehemu hii ndiyo inayopata udhaifu mara nyingi kwa sababu ndiyo sehemu inayopata minyumbuko zaidi wakati tukifanya shughuli yo yote ya mwili.

Umbilical hernia inaweza kuwa moja kwa moja chini ya kitovu, lakini wakati mwingine inaweza kuwa juu kidogo au chini kidogo ya kitovu. Inaweza kuonekana kama kijikokoto kidogo chini ya ngozi, au ikikua inaweza kuonekana kama kijimpira cha gofu au hata kufikia kimpira cha tenisi kama kikiachwa bila tiba.




Kwa watoto wa kufikia hadi miaka 5, hernia hii kwa kawaida huondoka yenyewe. lakini kwa watu wazima hernia hii haipungui na huwa inazidi kuwa kubwa kila wakati. Wanawake kwa kawaida hupata umbilical hernia wakati wa ujauzito, na hupotea yenyewe baada ya kujifungua. Kwa baadhi ya wanawake, kijishimo hiki katika musuli hubakia baada ya kujifungua. Inashauriwa kuwa wanawake wasubiri kwa miezi 3-6 kuona kama hernia hii itafunga yenyewe.

Kama ilivyo kwa hernia nyingine, dalili za kawaida ni maumivu kwenye kitovu. Kutokana na mafuta au misuli kupita kwenye hernia hii, uvimbe utaonekana chini ya ngozi kwenye eneo hilo. Baada ya muda, kama hernia itakuwa kubwa sana, utumbo unaweza kunaswa kwenye hernia hiyo na kuleta madhara kwenye utumbo, vikiambatana na kichefuchefu, kutapika, na kufunga choo.

Kwa sababu hakuna hernia inayopona yenyewe, upasuaji unahitajika. Njia inayopendekezwa hapa ni open surgery kwa sababu tundu ni dogo.
3. Femoral (below the groin)
4. Epigastric (just below the breast bone)
5. Ventral (above the umbilicus)
6. Incisional (through a prior surgery site)
7. Sports


Namna nyingine za kuelezea Hernia:

1. Recurrent (after a prior hernia repair)
2. Unilateral (one side of the body)
3. Bilateral (both sides of the body)



CHANZO/SABABU YA HERNIA

Ukiondoa hernia inayotokana na upasuaji wa awali, mara nyingi hakuna sababu inayoeleweka ya kusababisha hernia. Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata hernia ni wenye umri mkubwa, na wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake.

Hernia inaweza kujitokeza mtoto anapozaliwa au kwa watoto waliozaliwa na dosari kwenye kuta za matumbo yao.

Shughuli au madawa yanayosababisha mgandamizo kwenye kuta za tumbo vinaweza kusababisha hernia. Vitu hivi ni pamoja na:

. Kujikamau kwa nguvu wakati wa haja kubwa kutokana na choo kuwa kigumu
. Kikozi cha mara kwa mara
. Kuwa na tatizo la cystic fibrosis
. Kuvimba kwa tezi dume
. Unene wa kupindukia
. Kukojoa kwa shida
. Kunyanyua vitu vizito
. Maji tumboni
. Lishe duni
. uvutaji wa tumbaku
. Korodani zisizoshuka
. Uchovu wa mwili



DALILI ZA HERNIA



Mara nyingi, hernia ni uvimbe unaoonekana usio na mauvimu na usiohitaji tiba ya haraka. Lakini wakati mwingine, inaweza kukukosesha raha na kuwa na maumivu, dalili zikiongezeka wakati umesimama au wakati unanyanyua vitu vizito. Watu wengi huona uvimbe ukizidi na hatimaye humwona daktari.

Kuna wakati ambapo hernia inahitaji huduma ya haraka ya upasuaji, kwa mfano, pale sehemu ya utumbo inapokuwa imezibwa na hernia ya tumbo (inguinal hernia).

Hatua za haraka za uchunguzi zinatakiwa zichukuliwe wakati inguinal hernia inapoanza kuonyeza dalili kali za:

. Maumivu
. Kusikia kichefuchefu
. Kutapika

Uvimbe wa hernia yenye dalili hizi mara nyingi ni mgumu na huleta maumivu na hauwezi kusukumwa urudi ndai ya tumbo.

Hiatal hernia inaweza kuleta dalili za acid kama kiungulia, kinachotokana na tindikali za tumboni kupanda kwenye koromeo.



MATIBABU YA HERNIA



Hernia isipokuwa na dalili mbaya, njia bora ni kuiacha na kusubiri, ingawa hii inaweza kuwa njia sahihi kwa hernia za ina fulani, kama femoral hernia.

Madaktari bado hawajafikia kukubali ama wote kuhusu faida za kufanya upasuaji kwa inguinal hernia ambayo haijaanza kuleta usumbufu ambayo inaweza kusukumwa ndani ya tumbo. Madaktari wengi wa nchi ya Marekani wanashauri kusubiri badala ya kufanya upasuaji. Wengine wanashauri kufanya upasuaji ili kuiwahi kabla haijaweza kuziba sehemu za utumbo.

Uamuzi wa kufanya upasuaji unategemea hali iliyopo, pamoja na sehemu hernia ilipo, ambapo kuna upasuaji wa aina mbili unaoweza kufanyika:

. Open surgery
. Laparoscopic operation (keyhole operation).

Open surgery huziba hernia kwa kutumia nyuzi (sutures), mesh au vyote na kidonda juu ya ngozi kuzibwa kwa nyuzi, staples au surgical glue.







Laparoscopic repair hutumika kwa upasuaji wa kujirudia ili kukwepa makovu, igawa ni ghali zaidi, inapunguza uwezekano wa kuleta madhara hasa ya maambukizi ya vijidudu.

Kwa kulinganisha upasuaji huu wa aina hizi mbili, asilimia za uwezekano wa hernia kujirudia zinalingana, ingawa open surgery inaweza kusababisha madhara zaidi, kama maambukizi ya vijidudu.

NOTED:Mpendwa msomaji wetu nadhani umejifunza na kufahamu kuwa matibabu ya hernia (ngiri kavu) ni Upasuaji hivyo usije ukadanganyika na kupoteza pesa zako kutafuta Dawa ya kukutibu hernia pasipo kufanyiwa upasuaji hapo utakuwa unajidanganya maana ni hivi utumbo umetoka unawezaje kutumia Dawa utumbo ukajirudisha tumboni?!!
Pia mpendwa msomaji Wetu naimani utakuwa umejifunza pia kuwa ugonjwa wa ngiri  kavu (hernia) ni tofauti sana na ugonjwa wa tezi dume
Wasiliana nasi kupata ushauri wa matibabu zaidi
+255746465095/+255657041420
Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

FAHAMU CHANZO NA TIBA YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE





CHANZO na TIBA ya tatizo la WANAWAKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Mpendwa msomaji ni matumaini yetu kwamba wewe pamoja na familia yako ni wazima karibu tena katika blog yetu tuweze kufahamu Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au kukosa nyege kwa lugha ya mitaani.
Tatizo hili ambalo huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume lakini ni wanaume wanaokerwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake. Wakati takwimu inaonyesha  ni asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni mara mbili ya hii ya wanaume. Huku takwim ikionyesha  ni asilimia 23 ya wanaume wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.
Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa sababu kuna mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana na hili tatizo.
Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalibali yanayomtokea katika maisha yake. Baadhi ya matukio yanayoathiri hamu ya mwanamke kufanya mapenzi ni pamoja na kuanza na kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme, kupata ujauzito, na magonjwa. Kama wewe mwanamke umepatwa na hali hii unaweza kukabiliana nayo kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayo badilisha hali hii au kutumia baadhi ya dawa zinazosaidia kuondoa tatizo hili.

SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA

Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika makundi manne:
1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme                                     Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.
2. Matatizo Katika Maisha                                                                              Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:
Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa. Kama mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo ya afya. Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni Kansa,maambukizi katika via vya uzazi(pelvic inflammatory disease,shinikizo la damu, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili 
Matumizi ya madawa. Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mtindo wa maisha. Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.
Upasuaji. Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneno ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.
Uchovu. Uchovu unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.
3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni.                                                           Kukoma Hedhi. Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.
Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
4. Matatizo Ya Kisaikolojia                                                                                             Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:
  •  Waswasi na kuwa na msongo wa mawazo
  •  Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
  •  Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
  •  Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa   au kubakwa
  •  Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi

MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA MWANAMKE

Hakuna dawa ya moja kwa moja toka hospitalini kwa sasa hivi kwa ajili ya kuondoa tatizo hili, hata hivyo wanawake wengi wanaweza kurudi kwenye hali zao za kawaida kwa kushirikiana na waume zao waelewa.
Katika nchi zilizoendelea, kila siku wamekuwa wakija na dawa na vifaa vipya vya kuondoa tatizo hili na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida. Vipo ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni Suction Vibrators, Desire Creams na Erection Drugs..

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE

Utafiti umeonyesha pasi shaka kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi. Baadhi ya chakula na virutubishi vimehusishwa na hamu ya kufanya mapenzi (nyege). Virutubishi ndani ya chakula ambavyo vinasaidia hali hiyo ni antioxidants, vitamin C, vitamin E, potassium na zinc. Kirutubishi cha zinc ambacho hupatikana ndani ya  vitunguu swaumu, mbegu za maboga, ufuta na mbegu za matikitimaji, kinaongeza mbegu kwa mwanamme (sperm count) hivyo humsaidia kuongeza hamu ya kufanya Ma ndoa. Chakula cho chote chenye virutubishi hivi kikiliwa, humfanya mlaji asikie hamu ya kufanya mapenzi au kwa maneno ya mtaani, chakula hiki kinasaidia kuongeza nyege. Baadhi ya chakula cha kuongeza nyege ni:
TIKITIMAJI


Hili linachukuliwa kuwa ndilo tunda bora katika kuboresha afya ya mapenzi. Tunda hili lina asilimia 92 ya maji na asilimia 8 zinazobakia zina phytonutrient citrulline ambayo hugeuzwa kuwa arginine. Arginine ni amino acid ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa kwenye hali ya ubora wake na kusadia damu kupita vizuri zaidi. Tikitimaji kwa hiyo husaidia damu ifike kwa kiwango kizuri zaidi kwenye sehemu ambazo hutakiwa kutanuka wakati mtu akipata hisia za kufanya tendo la ndoa ambazo ni viungo vya ndani ya kisimi cha mwanamke

PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakul ambacho kimeungwa pilipili hufanya hat mapigo ya moyo kuwa tofauti na waka mwingine hata jasho kutoka au kama kutoka. Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mgusu wa hisia za raha
Pia pilipili husisimua mfumo wa ufaham (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu 
NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na suka ngumu (complex sugar) ambazo kusaidi kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidi katika kuzalisha homoni za testosteron kwenye damu. Na pia nafaka huwezesh mtu kuwa na nguvu hatimaye kwend masafa marefu wakati wa tendo. Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya njema na mahusian mazuri ya ndoa yako 

MATUNDA NA MBOGAMBOGA ZA MAJANI
Mlo wenye matunda na mboga za maja una matokeo makubwa sana katika ham ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol kuongezeka kwa mafuta mwilini huzui mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu. 
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwa unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha home za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na libido kidogo. Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia na kutaka au hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. 

TANGAWIZI
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa na kuanikwa na kuwa kama unga. 

ASALI

Asali ina madini yanayoitwa boron, ambay husaidia mwili kutumia homoni ya estroge ambayo ni homoni inayohusika na viung ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke. Pi kuna utafiti unaoonesha kwamba asa huongeza nguvu, kitendo ambach kitapelekea mwanamke kuwa uwezo n hamu ya tendo la ndoa au libido. 

KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja n kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system). Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapen haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri 
Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume. 

OYSTERS
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zai na uzalishaji wa homoni ya testosteron kwa wanaume. Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinakuwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa. 

SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo san cha fat na pia kuwa na kiwango kizuri ch protein, soya zina phytoestrogens ambay husaidia sana wanawake ambao wamefiki menopause kutengeneza homoni estrogen y ziada. Husaidia uke kuwa laini (we lubricated) mwanamke akisisimliwa waka wa tendo la ndoa. 

CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemika ambayo husababisha hisia (feelings) z furaha wakati wa mwanamke na mwanaume kufika kileleni (orgasm)


MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na umejaribu njia hizo hapo juu bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255623026602/+255746465095)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuongeza hamu ya tendo la ndoa na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255623026602/+255746465095(Dr Naytham S Masoud )

1 comments:

FAHAMU CHANZO NA TIBA YA TATIZO LA MWANAUME KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA







CHANZO NA TIBA YA TATIZO LA MWANAMME KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA



Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul mpendwa msomaji wetu ni matumaini yangu kwamba wewe na familia yako mnaendelea vizuri kiafya leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, kwa maneno lugha ya mitaani linaitwa tatizo la kukosa nyege. Tutajadili sababu zinasababisha mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, madhara yanayotokana na hali hiyo na kisha kuona ni nini cha kufanya ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa au kuongeza nyege. Bahati nzuri ni kwamba kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa. Watu wengine wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka. Wakati ni kweli kwamba hilo huwatokea wengi,ila sio lazima kwamba hamu ya kufanya mapenzi ipungue umri unapoongezeka. Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili.

UKUBWA WA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA

 Wanaume wengi hawapenzi kulizungumzia tatizo hili waziwazi na hata wanawake pia. Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, kwa lugha nyepesi kuna mwanamme mmoja mwenye tatizo hili baina ya kila wanaume sita au saba. Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali kama sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hunyongea wanapoona wana mapungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake.Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake. Hata hivyo tatizo la mwanmme kukosa hamu ya kufanya mapenzi limebainika kuwa ndilo linaloongoza katika kuleta migogoro ya unyumba kuliko matatizo mengine yote.
 NAMNA UNAVYOWEZA KUGUNDUA KAMA UNA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA
Tatizo hili halitokei ghafla kama vile umelala halafu ghafla asubuhi unaamka una mafua, la hasha. Ni kitu kinachotekea pole pole na pengine mwenyewe usijigundue. Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita au miezi kadhaa iliyopita. Vile vile kutofanya tendo la ndoa kwa kipindi fulani haimaanishi kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, pengine una hamu thabiti lakini mazingira hayakukuruhusu. Lakini iwapo hakuna kikwazo cho chote na upo na mwenzi wako halafu inapita wiki bila kufanya tendo la ndoa au unalifanya tendo hilo mara moja au mbili tu kwa mwezi, inabidi uanze kujiuliza maswali. Lakini ieleweke pia kuwa kuhesabu umefanya tendo la ndoa mara ngapi katika kipindi fulani si kipimo pekee cha tatizo hili. Mawazo yako kwa ujumla kuhusu tendo hili ni muhimu pia – jinsi unavyolichukulia na kuliwazia tendo hili kabla, wakati wa tendo na baada ya kumaliza tendo ni muhimu katika kujipima.
Viashiria vingine vyaweza kuwa: kumtomasa mkeo mkiwa ndani tu – chumbani na si penginepo. Iwapo tendo hili unalifanya pale tu mwezi wako anapokuanza na huwa unalifanya kama mazoea bila kuwa na mawazo ya kushiriki kikamilifu. Kama humwazii mpenzi wako anapokuwa hayupo kwamba angekuwapo ungeweza kufanya naye tendo la ndoa. Vitu hivi kama vinakutokea basi kuna dalili za kuwa unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na kwamba inabidi utafute suluhisho.

VISABABISHI VYA TATIZO LA KUKOSA HAMU  YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme linaweza kusababishwa na vitu vingi sana. Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.

Mahusiano Baina Ya Mwanamme Na Mwanamke
Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi. Jee, unapata raha na una amani katika mahusiano yako na mpenzi wako? Huna wasiwasiwo wote na mahusiano yenu? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza.
Kama mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.
 Kama kuna mambo yanasababisha tendo la ndoa lisifanyike kwa urahisi, ufanisi na kufurahia, hamu ya kufanya tendo hilo inaweza kupungua. Kwa mfano, kama mwanamme anawahi kufika kileleni au kama ana matatizo ya kushindwa kusimamisha uume tendo zima la ndoa halitakuwa la kukufurahisha sana hivyo unaweza kupoteza hamu ya kulifanya. Hebu fikiria tunda linalokufurahisha sana ukilila, ukilikosa kwa siku kadhaa, utalikumbuka na kulitafuta lakini ambalo halikufurahishi sana ukilila hutalikumbuka na kulitafuta.
 Mawazo Mengi Na Uchovu
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia. Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani. Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.
 Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi. Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.
Matumizi Ya Madawa Na Pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na:
– madawa ya high blood pressure
– madawa ya kuondoa msongo wa mawazo
– madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone
– na mengineyo
 Umri Kuwa Mkubwa
Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanammme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. Kama thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.
Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.
Matatizo Ya Kiafya
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.
 MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME
 Kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya kuongeza na kudumisha hamu ya kufanya tendo la ndoa. Tatizo hili halijapatiwa dawa za kwenye mahospitali isipokuwa pale unapogundulika kuwa una kiwango kidogo cha testosterone ambapo utaandikiwa namna ya kukiongeza kiwango chako. Fanya yafuatayo kuongeza hamu yako ya kufanya mapenzi.
1. Tafuta mchezo ambao unaweza kushiriki au fanya mazoezi kama vile ya kutembea au kukimbia. Kila siku ufanyapo mazoezi yako jaribu kila siku kufikia kiwango cha juu zaidi ya kile ulokwisha kifikia.
2. Inasaidia kufahamu kuwa ni asilimia 40 hadi 50 ya matendo ya ndoa mnayoyafanya yatawaridhisha wote wawili. Kukosa kumridhisha mwenzio iwe changamoto ya kukufanya ufanye utafiti na utundu wa kuboresha tendo mtakapokutana tena.
3. Kama nilivyodokeza hapo juu, jaribuni kwa pamoja kujadili jinsi ya kuboresha namana yenu ya kushiriki katika tendo la ndoa kila mmoja akieleza kile ambacho angependa afanyiwe. Inasaidia kusoma maandishi kutoka sehemu mbalimbali na kutazama mikanda mbalimbali.
4. Kufanya tendo kwa kushitukiza inapendeza wakati fulani. Lakini hili kidogo linaweza kuwa si zuri ukizingatia majukumu ya kila siku ya maisha ya sasa, si rahisi kupata muda wa kutosha wa kustarehe na mpenzi wako. Kuwa na mpango na ratiba ni bora zaidi na inasaidia kuleta hamu mtu anapokisubiri kitu kilichopangwa siku fulani na muda fulani – fikiria unaposubiri mechi kubwa ya timu yako. Mletee zawadi mpenzi wako, weka muziki mororo ulikuwa unaupenda siku zile, zimisha simu na hakikisha kuna mazingira ya utulivu na ukimya.
5. Hamu huongezeka inapoona kitu kipya. Ukienda na mwenzi wako kwenye sherehe nje ya nyumba yenu, utapata fursa ya kumwona mkeo kwa namna nyingine. Utaweza kuuona uzuri wake na yeye pia atakuona wewe kwa namna nyingine. Wote mtakumbuka vitu ambavyo kila mmoja wenu vilimvutia kwa mwenzie

MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME KUPITIA VYAKULA ASILI

Historia yetu inaonesha kuwa kwa kipindi kirefu, wanawake na wanaume wamekuwa wakitumia chakula kumvutia mpenzi. Mara nyingine chakula hicho kinakuwa kinaongeza hamu ya kujamiiana na kuna wakati ni harufu au ladha ya chakula hicho ndiyo inayokufanya kupata hisia hizo. muonekano wake, ladha yake unapokila, uhaba wake.

ASALI

Pamoja na utamu wake, asali ina nafasi kubwa ya kuongeza hamu ya kujamiiana kwakuwa ina aina zote za madini ya Vitamin B, ambayo ndio yanasaidia sana kuupa mwili nguvu.

Unaweza kula vijiko kadhaa kila siku, wengine huichanganya wakiwa wanaotengeneza keki, kuipaka kwenye mkate au chakula chochote.

SHAYIRI

Maji ya shayiri asubuhi au jioni yanasaidia kuongeza hamu ya kujamiiana. Shayiri madini ya L-arginine yanayoongeza homoni za testosterone, pia ina wingi wa kundi la Vitamin B. Shayiri huuzwa bei nafuu na ni njia rahisi sana ya kuongeza msukumo wa damu, jambo ambalo hutokea unapofanya mapenzi. Shayiri inapotumiwa kwa muda mrefu inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya kusimama kwa uume.

PARACHICHI

Wataalamu wa masuala ya mapenzi wanasema kuwa parachichi linaingia kwenye kundi hili kwakuwa umbo lake linafananishwa na maumbile ya mwanaume au mikunjo katika mwili wa mwanamke na kwamba ulaini wake na jinsi linavyotoa majimaji huongeza hisia za mapenzi. Yanaweza kuliwa yenyewe au kwa kuchanganywa kwenye vyakula vingine.

Yana kiwango kikubwa cha mafuta na vitamin E vyenye kazi ya kuongeza msukumo wa damu, hivyo kuongeza kiwango cha utengenezwaji wa testosterone. Kama hutaki kutumia parachichi kwa kazi hii, basi litakusaidia kwa kung’arisha ngozi kutokana na madini ya vitamin E.

MBEGU ZA MABOGA

Mbegu za maboga zina wingi wa madini ya tyrosine (aina mojawapo ya asidi aina ya amino inayosaidia kuchangamsha mwili). Mbegu hizi pia zina virutubisho vingi vinavyosaidia kuongezeka kwa msukumo wa damu mwenye viungo vya uzazi.

Unaweza kuzioka kwenye oveni, kuzisaga au kula kwa kuzichanganya na vyakula vingine, ikiwamo asali pia – ili kuongeza faida zaidi.

TIKITI MAJI

Wataalamu wanasema kuwa watu wengi hawajui jambo moja kuhusu tiketi: kwamba kama ambavyo tiketi linaweza kukata kiu yako kwa wingi wa maji yaliyomo, ndio hivyo hivyo inavyoweza kukusaidia kwenye maswala ya kujamiiana. Utafiti umeonesha kuwa tunda hilo lina kiwango kikubwa cha viambata aina ya citrulline, ambayo ina kazi sawa na dawa aina ya Viagra kwa mwanaume.

TANGAWIZI
Tangawizi inafanya damu iende kwa kasi jambo linaloweza kusababisha mwili uweze kupata msisimko wa kimapenzi kirahisi sana. Pia inasaidia kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula, jambo linalosaidia sana kukufanya ubaki kuwa na hamu ya kufanya mapenzi kama umekula chakula kingi.

CHOCOLATE

Wataalamu wanasema kuwa dawa pekee ya ukweli kwenye maswala ya mapenzi ni cocoa. Cocoa inachochea uzalishaji wa homoni zinazofanya ujisikie vizuri aina ya serotonin na dopamine, na ina kemikali aina ya phenylethylamine, inayotengenezwa kwa wingi kwenye ubongo unapoingia mapenzini. Cocoa inafanya kazi hii hasa inapochanganywa na chokoleti kwakuwa inayeyuka kirahisi na kuleta hamasa ya kimapenzi mdomoni. Kwakuwa chokleti ni nzuri unapoila—na inafanya tujisikie vizuri baada ya kuila—zawadi inayomfanya mtu apate hisisa nzuri siku zote lazima itapendwa.

MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji Kama una tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na umejaribu njia hizo hapo juu bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu  ili upate maelezo na ushauri zaidi (+255623026602/+255746465095)
(nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com)
Green health consultation center tuna Dawa za kuongeza hamu ya tendo la ndoa na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako
Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

0 comments:

FAHAMU TIBA YA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI(GENITAL WARTS)

 FAHAMU TATIZO LA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI (GENITAL WARTS)



Asalaam Alaykum warhmatullah wabarakatul,Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wa blog hii karibu darasani kwa mara nyingine tena leo tunazungumzia tatizo la kuota vinyama,chanzo chake na namna ya kutibu tatizo hili


Ugonjwa wa kuota Vinyama sehemu za siri/Masundosundo/vigwaru au Genital warts ni tatizo la kuota vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri. Vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo [urethra], vulva, shingo ya kizazi [cervix], au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.
Huu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana [sexually transmitted infection (STI)].
VISABABISHI VYA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI {GENITAL WARTS}
Ugonjwa wa masundosundo husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa Human papilloma virus (HPV). Kuna zaidi ya aina 70 tofauti za virusi wa HPV ingawa si wote wanaosababisha masundosundo kwenye maeneo ya siri [genital warts]. Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha masundosundo kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyngine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi [carcinoma of the cervix] kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer] kwa jinsia zote mbili. Aina hii ya virusi hujulikana pia kama high-risk HPV.
Pamoja na kwamba ugonjwa wa masundosundo kwenye maeneo ya siri umejitokeza kwa kasi kubwa hasa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI, watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile. Kwa mfano, kwa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi [cervix] bila kuonekana wala kuhisiwa kwa urahisi.
Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni. Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yeyote ile. Aidha imeonekana pia kuwa si kila mtu anayejamiina na aliye na maambukizi ya HPV au mwenye masundosundo anaweza naye kupata ugonjwa huu.
MAKUNDI YALIYO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI{GENITAL WARTS}
Watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupatwa na masundosundo kwenye maeneo ya siri
• Wenye wapenzi wengi
• Kufanya ngono isiyo salama/ ngono zembe
• Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo
• Watumiaji wakubwa wa sigara pamoja na pombe
• Kupatwa na maambukizi ya virusi wa herpes na wakati huo huo kuwa na msongo mkali wa mawazo
• wajawazito
• kuwa na upungufu katika mfumo wa kinga mwilini kwa sababu ya magonjwa mbalimbali au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani fulani kwa watoto wadogo, ukiona mtoto amepata masundosundo basi ni vema kufanya uchunguzi ikiwa amewahi kubakwa au kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
DALILI ZA KUOTA VINYAMA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI[GENITAL WARTS}
Masundosundo [genital warts] huonekana kama vioteo laini vinavyojitokeza juu ya ngozi ingawa wakati mwingine vinaweza kuwa vidogo mno kiasi cha kutoweza kuonekana vizuri kwa macho ya kawaida.
Kwa wanaume, vioteo hivi hutokea zaidi kwenye uume, ngozi ya pumbu, eneo la mitoki, mapajani pamoja na maeneo ya kuzunguka nje ya njia ya haja kubwa au ndani yake; wakati kwa wanawake hutokea ndani ya uke au njia ya haja kubwa, nje ya uke au ngozi ya nje kuzunguka njia ya haja kubwa, au ndani ya uke kuzunguka eneo la shingo ya kizazi.
Kwa wale wanaopenda kufanya ngono ya mdomoni [oral sex], wanaweza kupatwa na masundosundo/genital warts kwenye maeneo ya kuzunguka mdomo, lips, kwenye ulimi na hata kwenye utando unaozunguka koo.

Dalili nyingine ni kama vile mgonjwa kujihisi kukosekana kwa hisia [kufa ganzi] maeneo yaliyozungukwa na masundosundo, kwa wanawake kuongezeka kwa utoko/ uchafu sehemu za siri, kuwashwa sana maeneo ya siri na wakati mwingine kutokwa na damu ukeni mara baada ya tendo la ngono. Hata hivyo dalili hizi hutokea mara chache sana.
Wanawake wengi vijana wanaojihusisha na vitendo vya ngono [sexually active] huambukizwa sana ugonjwa huu lakini wengi wao hupona bila hata kuhitaji matibabu, wakati wanaume wanaoambukizwa, wengi wao huwa hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa ingawa wanaweza kuwaambukiza wenzi wao bila ya wao kujua.
UCHUNGUZI NA VIPIMO

Kwa wanawake, uchunguzi wa ugonjwa wa masundosundo/genital warts hujumuisha uchunguzi wa maeneo ya nyonga [pelvic examination] ambapo daktari huchunguza eneo hilo kwa kutumia vifaa maalum vinavyomuwezesha kuona uwepo wa masundosundo na wapi vilipo. Wakati fulani, kunyunyizia dawa yenye tindikali ya acetic acidhusaidia kufanya masundosundo kuonekana kwa urahisi zaidi. Wakati mwingine daktari anaweza pia kufanya kipimo cha pap smearkwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi [kwa vile kama tulivyoona hapo awali, zipo aina fulani fulani za HPV ambazo husababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake].
Kwa wanaume, uchunguzi wa maeneo ya siri ni muhimu sana ili kufahamu kama kuna masundosundo au la.
MATIBABU
Ni vema genital warts zitibiwe hospitali na daktari; haishauriwi kutumia dawa za kununua kujitibu mwenyewe kwa vile kuna uwezekano mkubwa wa kuchanganya aina ya dawa zinazotumika maalum kutibu aina nyingine za warts kwa ajili ya kujitibu genital warts.
Matibabu ya genital warts hufanyika hospitali kwa mganga kuondoa vioteo juu ya ngozi iliyoathirika au kwa kutumia dawa utakazoandikiwa na daktari na kuelekezwa namna ya kuzitumia mwenyewe nyumbani kwa siku kadhaa mpaka majuma kadhaa. Dawa zinazotumika ni pamoja na Podophyllin na podofilox, Trichloroacetic acid (TCA) au Imiquimod .
Ukiachilia mbali matumizi ya dawa, masundosundo yanaweza pia kutibiwa kwa njia ya upasuaji mdogo kama vile kwa kuvikata, au kuvimaliza kwa kutumia njia ya baridi/barafu [cryosurgeryLaser therapy].
Kama yalivyo matibabu ya magonjwa mengine yanayosambaa kwa njia ya ngono, ni lazima yahusishe pia tiba kwa mwenza wa mgonjwa. Wakati mwingine hata kama utajihisi huna dalili za waziwazi, ni vema kumuona daktari ili uchunguzwe na kutibiwa kuepusha kusambaza ugonjwa kwa watu wengine au kuachia ugonjwa mpaka ukakuletea madhara zaidi. Aidha matibabu yanaweza kuhitaji kurudiwa rudiwa mara kadhaa mpaka masundosundo yatakapokuwa yametoweka kabisa.
Kwa wanawake ambao wametibiwa genital warts na kupona au wale ambao wamewahi kuwa na wenza waliowahi kuugua ugonjwa huu, wanashauriwa sana kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa shingo za kizazi [pap smear ni vema kufanya pap smearwalau kila baada ya miezi 3 mpaka 6 tangu kupata matibabu ya awali ya genital warts. Na kwa wale watakaonekana kuwa na dalili za awali za saratani ya shingo ya kizazi, hawana budi kufanyiwa uchunguzi na tiba zaidi li kuepusha uwezekano wa kupata saratani kamili ya shingo ya kizazi..
MPENDWA MSOMAJI WA MAKALA HII WASILIANA NASI +255746465095/+255657041420 IKIWA WEWE AMA NDUGU YAKO ANASUMBULIWA NA UGONJWA HUU WA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI (GENITAL WARTS) TUNAWAPA POLE SANA NA TUNAWAKARIBISHA OFISINI KWETU ILALA,DAR ES SALAAM KWA AJILI YA USHAURI NA MATIBABU YA UGONJWA HUU 


Baadhi ya nchi zilizoendelea zina utaratibu wa kuwapatia chanjo ya kuwakinga wanawake vijana au wasichana wadogo wenye umri kati ya miaka 10 mpaka 25 dhidi ya maambukizi ya HPV. Chanjo hii hutolewa hata kwa wale ambao wamewahi kuugua genital warts ingawa imeonekana kuwa ufanisi wa chanjo ya HPV dhidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wale waliowahi kupatwa na genital warts zilivyosababishwa na high risk HPV huwa ni mdogo ukilinganisha na wale ambao hawajawahi kuugua lakini wapo katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huo.
Hata hivyo, pamoja na kuwa umetibiwa, bado unaweza kuwaambukiza wengine virusi hawa wa HPV hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kujikinga wakati wa kujamiiana.
MADHARA YA KUOTA VINYAMA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI {GENITAL WARTS}
Kama tulivyoeleza hapo awali, baadhi ya aina fulani za HPV wameonekana kusababisha saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya vulva. Kiujumla, HPV ndiyo kisababishi kikuu cha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wengi. Tofauti na wanawake, ifahamike pia kuwa aina za HPV zinazoweza kusababisha genital warts kwa wanaume ni tofauti kabisa na zile zinazoweza kusababisha saratani ya uume [cancer of the penis] au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer].
Kwa baadhi ya wagonjwa, masundosundo yanaweza kuwa mengi na makubwa sana kiasi cha kuhitaji matibabu ya muda mrefu na ghali zaidi pamoja na ufuatiliaji wa kina.
NAMNA YA KUJIKINGA|KUJIDHIBITI NA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI {GENITAL WARTS}
Njia mojawapo ya uhakika kabisa ya kujiepusha na ugonjwa wa genital wartspamoja na magonjwa mengine ya ngono/zinaa ni kujiepusha na matendo ya ngono na zinaa kabisa. Lakini kwa wale ambao ni ngumu kufanya hivyo, wanaweza kupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huu kwa kujihusisha kingono na mwenza mmoja tu ambaye una uhakika kuwa hajaambukizwa wala hayupo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa haya.
Tofauti na magonjwa mengine ya zinaa, matumizi ya condom hayana uhakika wa asilimia mia moja katika kukukinga dhidi ya HPV kwa sababu virusi wa HPV au hata masundosundo yanaweza kuwa nje nje kwenye ngozi ambayo uwezekano wa kugusana ni mkubwa. Pamoja na hayo, bado condom inaweza sana kupunguza hatari ya kuambukizwa masundosundo ikiwa tu itatumika vema na inashauriwa kuitumia mara zote unapokutana kingono na mwenza usiye na uhakika naye.
Tukumbuke kila wakati kuwa HPV inaweza bado kuambukizwa kwa mtu hata kama mwenza hana masundosundo yanavyoonekana au hana dalili zozote zile.
Ikiwa kuna uwezekano, ni vema kwa wanawake wote wenye umri wa miaka kati ya 9 mpaka 26 kupata chanjo dhidi ya virusi wa HPV ili kuzuia uwezekano wa kuambukizwa virusi hao ambao hatimaye husababisha saratani ya shingo ya kizazi

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE  KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM

 Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420(Dr Naytham S Masoud )

3 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre