FAHAMU CHANZO CHA CHUNUSI,AINA ZA CHUNUSI NA MATIBABU YAKE

FAHAMU CHANZO CHA CHUNUSI NA JINSI YA KUZUIA CHUNUSI

Asalaam Alaykum warhmatullah wabarakatul,Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wa blog hii karibu darasani kwa mara nyingine tena leo tunazungumzia tatizo la chunusi chanzo chake na namna ya kutibu tatizo hili

Chunusi ni ugonjwa unaowapata watu wa mataifa yote na wa umri wote. Ugonjwa uliozoeleka zaidi ni ule unaowapata vijana wakiwa kwenye umri wa balehe. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa umri huu hupata chunusi. Chunusi huwapata vile vile watu wenye umri mkubwa na, vichanga wengine hupata chunusi kutokana na mama zao kuwarithisha homoni kabla tu ya kuzaliwa. Ukurasa huu utajadili chanzo cha chunusi katika mwili wa binadamu, aina za chunusi na hatua zinazoweza kuchuliwa ili kuepukana na chunusi.
Katika mwili wa binadamu, chunusi huonekana zaidi maeneo ya usoni, mgongoni, kifuani, mabegani na shingoni. Kutegemeana na uwingi wa chunusi hizo, mwathirika huweza kunyanyasika kimawazo na kupata makovu juu ya ngozi yake. Kuna dawa za kutibu chunusi ingawa ni ugonjwa unaoweza kujirudiarudia. Chunusi huondoka polepole sana na wakati mwingine chunusi mpya huanza kujitokeza kabla nyingine kupona kabisa. Ni ugonjwa unaotakiwa kupewa tiba ya mapema ili kuepuka kupata madhara ya kudumu.
CHANZO/VISABABISHI VYA CHUNUSI
Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu vya vinyweleo (hair follicles). Picha hapa chini inaonyesha muundo wa kitengo kimoja cha kinyweleo (pilosebaceous unit).



Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. vitengo hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.
Tezi za mafuta hutoa sebum ambayo huvisaidia ngozi na vinyweleo kutokuwa vikavu.
Mtu anapokuwa kwenye balehe, tezi hizi za mafuta hupanuka na kuwa kubwa na hutoa sebum (aina ya mafuta) kwa wingi zaidi, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa homoni za androgens. Baada ya umri wa miaka 20, utengenezaji wa sebum hupungua.
Sebum hii iliyotengenezwa na sebacious gland huchanganyikana na seli za ngozi zilizokufa na kwa pamoja hutolewa nje ya mwili kupiti vijitundu vya vinyweleo. Vijindu hivi vikijaa mchanganyiko huo, humwaga ziada juu ya ngozi na na kuifanya kuwa laini. Hali hii ikiendelea bila dosari, ngozo hubaki laini na yenye afya.
Chunusi za aina mbalimbali hutokea pale kunapotokea dosari katika ufanyaji kazi wa vijitengo hivi vya kwenye ngozi. Tutaelezea dosari mabilimbali zinazoweza kutokea, na nini kitaonekana juu ya ngozi ya mtu huyu. Kuna dosari ambazo zitaleta vijipele vya kawaida na nyingine kuleta mapele makubwa, mara nyingine yaliyotunga usaha.
Kuna hali mbalimbal ambazo zinaweza kutokea kwa chunusi kwenye ngozi. Kwa kawaida chunusi huanza kwa sababu zifuatazo:
. Seli za ngozi zilizokufa (corneocytes) hugeuka na kuwa nzito na katika kutembea kwenye kijitundu cha kinyweleo
huganda badala ya kutoka nje ya tundu
. Seli nyingi za ngozi kutokea sehemu ya juu ya tundu kuliko sehemu ya chini ya tundu la kinyweleo
. Uzalishaji wa mafuta (sebum) kuongezeka
Kuongezeka kwa vitu hivi ndani ya kijitundu cha kinyweleo, huziba sehemu ya juu ya kijitundu na kuzuia vitu hivi visitoke nje, hali ambayo kiutaalamu huitwa microcomedone. Bakteria waitwao Propionibacterium acnes, huishi ndani ya vijitundu hivi vya vinyweleo na hutumia sebum kama chakula chao. Kuongezeka kwa sebum hufanya bacteria hawa kuongezeka ndani ya vijitundu hivi lakini hawaleti madhara yo yote kwa sababu hadi sasa wanaishi ndani ya vijitundu tu – hawana madhara kwenye ngozi.
WHITEHEAD– CLOSED COME DONE
Kuongezeka kwa sebum na seli zilizokufa kutajaza vijitundu vya vinyweleo na kuufanya mchanganyiko huu kuwa mzito. Endapo vijitundu vitakuwa vidogo au vimeziba hali inayoitywa closed comedone au whitehead itajitokeza.
Kuendelea kujazana kwa mafuta kutasababisha eneo linalozunguka kijitundu hicho kuvimba. Whiteheads huweza mara nyingine kuambatana na mashambulizi ya bacteria – P.acnes bacteria – kutegemeana na kama bakteria hao waliweza kushambulia seli zinazolizunguka tundu.
BLACKHEAD– OPEN COME DONE
Kama katika kuongezeka huku kwa sebum na seli za ngozi zilizokufa, kijitundu cha kinyeweleo kitakuwa wazi, hali inayoitwa open comedone au blackhead itatokea.
Kuzidi kuongezeka kwa mafuta kutoka sebacious glands, kutalifanya eneo linalokizunguka kijitundu cha kinyweleo kuvimba. Blackheads zinaweza kuambatana na mashambulizi ya bakteria wa P.acnes endapo wataweza kushambulia eneo linalozunguka kijitundu cha kinyweleo.
CHUNUSI – PIMPLES
Kuzidi kuongeka kwa sebum kutoka kwenye sebacious glands na seli zilizokufa kutajenga msukumo kwenye seli zinazokizunguka kijitundu cha kinyweleo. Msukumo ukiwa mkubwa wa kutosha, kuta za kijitundu hupasuka na mafuta kupenya kwenye ngozi ya karibu. Kwa sababu mafuta haya yana uwingi wa bakteria wa P.acnes, ngozi hii inayozunguka kijitundu hushambuliwa na bakteria hawa na kuifanya ngozi hiyo kuwa na uvimbe nwekundu (pimples). Hali hii
kiutaalamu huitwa inflammatory papule.
CHUNUSI – PUSTULE

Chunusi za aina ya pustule hutofautiana na pimples au papules kwa kuwa na chembechembe nyeupe za damu (usaha). Wakati mwili unapambana na bakteria wa P.acnes, chembechembe nyeupe za damu ambazo ni sehemu ya kinga za mwili, hujazana na kutunga usaha katika vijitundu vya vinyweleo. Kwa sababu ambazo bado hazijafahamika vizuri kisayansi, chunusi nyingine hutunga usaha wakati nyingine hazitungi.
CHUNUSI – CYST (NODULE)
Wakati mwingine mafuta na bakteria wanaposambaa kwenye ngozi inayozunguka kijitundu, maambukizi husambaa eneo kubwa na huelekea chini zaidi ndani ya ngozi na kusababisha vijinundu (nodules or cysts) na makovu. Vijinundu hivi huleta maumivu makali na haviponi kwa urahisi.
MAMBO YANAYOCHANGIA UONGEZEKAJI WA CHUNUSI
Chunusi ni kitu cha kurithi, endapo wazazi wako walikuwa na chunusi basi uwezekano wa wewe kuwa na chunusi ni mkubwa sana. Chunusi pia hushambulia watu wakiwa katika umri wa barehe na ujanani wakati homoni kama za testosterone zinaongezeka mwilini. Wanawake hupata chunusi zaidi wanapofikia umri wa kuanza kupata siku za mwezi. Wanawake wengi huota chunusi siku chache kabla ya kuingia mwezini.
Kuna vitu vinavyoweza kuchangia kupata chunusi:
. Kuvaa vitu vinavyobana, vinavyosugua juu ya ngozi, kama, helmets, mikanda ya sidiria, sweta za kukaba shingo n.k.
. matumizi ya vipodozi vya ngozi au nywele vyenye vitu vibaya
. Kuosha uso mara nyingi au kuusugua uso kwa nguvu. Matumizi ya sabuni zisizofaa au maji ya moto sana huongeza makali ya chunusi.
. Kuwa na msongo wa mawazo mara kwa mara.
. Kugusa uso mara kwa mara.
. Kuvuja jasho.
. Kuacha nywele zining’inie juu ya uso na kuufanya uso kuwa na mafuta zaidi.
. matumizi ya baadhi ya madawa.
. Kufanya kazi kwenye mazingira ya mafuta au kemikali kwa muda mrefu.
MATIBABU YA CHUNUSI

Tiba ya chunusi itazingatia zaidi aina ya chunusi iliyotokea. Lakini kwa ujumla tiba hizo zinalenga kufanya yafuatayo:
. Kupunguza kunata kwa seli za ngozi zilizokufa ili ziliweze kutiririka kiurahisi na kutoka nje ya vijitundu vya kwenye ngozi. Lotion kama salicylic acid 2% zinaweza kutumika.
. Kuua bakteria wa P.acnes kwa kutumia antibiotics za aina mbalimbali, kwa mfano, benzoyl peroxide


MATIBABU YA CHUNUSI KWA NJIA ZA ASILI

Kuna njia nyingi za matibabu za kupunguza chunusi zikijumuisha kubadili hali ya maisha, taratibu na dawa. Kula kabohidrati chache na zinazomeng’enywa kwa urahisi, kama vile sukari, kunaweza kusaidia. Usijaribu kuviminya au kuvisugua kwa nguvu viupele kwasababu hufanya ngozi kuuma na kutengeneza makovu ya kudumu. Jiepushe kutumia manukato au vipodozi kwenye ngozi yenye chunusi. Tumia bidhaa za urembo zisizoziba matundu madogo madogo ya ngozi yako.
Chunusi pia huweza kutibiwa kwa matumizi ya tiba asili kama matumizi ya matunda na viungo kama vitunguu swaumu, mdalasini na vingine. Hii ni njia nzuri ya kupatia ngozi unafuu na tiba mbadala na rafiki kwa ngozi yako. Zifuatazo ni baadhi ya tiba asili za chunusi na salama kwa ngozi yako:

MDALASINI WA UNGA NA ASALI

Kwa wale ambao wanasumbuliwa sana na chunusi iwe, usoni, kifuani, mgongoni n.k wanaweza tumia mchanganyiko mzuri wa asali na mdalasini wa unga kwa kupaka angalau mara moja kwa siku. AsaliI na mdalasini  zinasaidia kuponyesha kwasababu zina tabia za ANTI-BACTERIAL (zinaua na kuzuia mazalia ya bacteria) Jinsi ya kufanya:
  1. Chukua vijiko vitatu (3) vya chai vya asali
  2. Chukua nusu kijiko cha chai cha mdalasini wa unga safi
  3. Changanya pamoja kupata uji uji mzuri
  4. Paka sehemu yenye chunusi na kisha kaa nayo kwa angalau dakika 10-30 kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.
ANGALIZO: MDALASINI unaweza kuwasha kwenye ngozi hivyo unashauriwa ujaribu kupaka kidogo kwenye kiganja cha mkono kwanza ili kupata uhakika kua haitakusumbua.
MATANGO
Unaweza kutumia tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia. Matango ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kisha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Acha likae kwa muda wa dakika 15 hadi 20 hivi, kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu hadi utakapopona.
ASALI
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi. Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.
PAPAI
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili. Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.
LIMAO
Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limao. Limao linajitokeza kwenye vyakula vingi tunavyokula kila siku mathalani limao halikosekani pakiwepo supu au mapishi yoyote ya samaki.
Limao lina kiasi kingi cha vitamini C ambayo inaweza kutumika kama antibiotiki inayozuia kuongezeka na kukua kwa bakteria wanaosababisha chunusi.
Limao pia ina tindikali maalumu inayohamasisha chunusi kutoka katika ngozi.
Unachotakiwa kufanya ni kukata limao pande mbili au nne na upake majimaji yake moja kwa moja kwenye chunusi pole pole kwa dakika 10 hivi kasha jisafishe na maji safi.
Tindikali katika limao inaweza kuzidhuru seli zilizopo juu ya ngozi yako hivyo tumia dawa hii mara 1 au 2 tu kwa wiki na siyo kila siku.
Vitamini C iliyomo kwenye limao husaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mengi sababu ndiyo vitamini inayosaidia kuongeza kinga ya mwili.
Kinga ni bora kuliko tiba!
Hivyo tumia vitamini C mara kwa mara au kunywa juisi ya limau kila siku ili kuweka mwili wako katika afya bora zaidi muda wote.
 BAKING SODA
Moja ya sababu za kutokea chunusi katika ngozi yako ni kuwepo kwa takataka au uchafu juu ya ngozi yako na njia rahisi ya kusafisha taka hizo ni kwa kutumia baking soda hivyo kuifanya ngozi ipumuwe vizuri.
Kwahiyo ukiwa na chunusi hebu fikiri kuhusu baking soda. Baking Soda husaidia kubandua seli za ngozi zilizokufa na kufanya mafuta yaliyozidi kuondoka.
Ni rahisi zaidi kutumia baking soda kutibu chunusi. Chukua baking soda na uchanganye kidogo na vijiko vinne vidogo vya maji au vya maji maji ya limau na upake uji huo moja kwa moja kwenye chunusi. Subiri kwa dakika 10 na ujisafishe na maji ya moto.

MATIBABU YA CHUNUSI CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER
Mpendwa msomaji wa blog yetu hii tunakukaribisha ofisin kwetu iliyopo ilala, machinga Complex, Lindi Street  Dar es salaam kwa ajili ya ushaur nasaha pamoja na matibabu ya Dawa za Asili
Matibabu ya chunusi  katika ofisi yetu ni matibabu ya Dawa pamoja na sabuni ya kijani ya mzaituni (green olive soap)
matibabu haya Utapatiwa baada ya kuonekana  hali ya tatizo lako lilivyo 

SABUNI YA KIJANI YA MZAITUNI (GREEN OLIVE SOAP)KIBOKO YA CHUNUSI


sabuni ya kijani ya mzaituni ni sabuni nzuri iliyotengezwa kutokana na mafuta ya mzaituni,Asali pamoja na Vitamin E 


KAZI NA FAIDA ZA SABUNI HII YA KIJANI YA MZAITUNI


~kutengeneza uzuri wa ngozi iwe na ubora wake
~Inaimarisha uasili wa ngozi
~Inaondoa mafuta na jasho na kuifanya ngozi kubaki kavu na safi.
~Inasafisha na inaondoa sumu ndani ya ngozi
~Inaondoa chunusi,mabaka na upele
~Huponya muendelezo wa tishu zilizo haribika ndani ya ngozi
~Huondoa mafuta yaliyoganda na kuziba vinyweleo na kuifanya ngozi ipumue vizuri
~Inang'arisha ngozi na  kuifanya ngozi ing'ae
~Inazuia uharibifu wa ngozi unaotokana na miali ya jua na kemikali nyingine kupitia ngozi.
~Inaondoa mba wa shingoni, mwilini na hata kichwani,
~Inaondoa Fungus za aina zote hata kwa wanaonuka miguu wameliwa vidole wakivua viatu
~Inaondoa harara kwa wanaokaa maeneo ya joto kali


NI SABUNI NZURI KWA WANAWAKE,WANAUME,WATOTO,VIJANA NA WAZEE


MATUMIZI YA SABUNI HII
1.loweka ngozi kwa maji..
2.paka sabuni juu ya ngozi..
3.sugu kwa dakika 1-3.....
4.suuza kwa maji safi.
5.tumia mara 2 kwa siku kupata matokeo mazuri
Ina harufu nzuri na isiyoumiza pua zako,harufu salama ya maua ya Zaituni


ANGALIZO
sabuni hii haijatengenezwa kwa kemikali za viwandani ni Tiba mbadala, hivyo unashauriwa kuitumia na kutokupaka vipodozi vya kemikali, hasa Lotion zenye hydroquinone, ina maana unatibu Kisha unajeruhi tena, Tumia Lotion zisizo na hizo kemikali Kwa matokeo mazuri ya utunzaji wa ngozi yako 

SABUNI HIZI ZINAPATIKANA OFISINI KWETU ILALA DAR ES SALAAM TU KWA BEI YA SHILINGI 10,000/= KWA REJAREJA PIA ZINAPATIKANA KWA SHILINGI 8,000/=KWA BEI YA JUMLA 

Mpendwa msomaji wetu tunashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili au lolote lile iwe wewe au ndugu/jamaa yako msisite kututafuta kwa msaada zaidi wa ushaur na matibabu PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YETU HII
      GREENHEALTHC.BLOGSPOT.COM 

Makala hii  imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation center
E-mail nsalum998@gmail.com/nmasoud998@gmail.com
+255746465095/+255657041420 (Dr Naytham S Masoud)

0 comments:

Copyright © 2017 Green health consultation centre